×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Ukame wasababisha wizi wa mifugo, huku wafugaji wakikimbilia kilimo

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 2 April 2013 23:30 GMT

Former pastoralists Joseph and Pauline Elila and their family thresh sorghum harvested from their fields in Nambeyo village in Kenya's semi-arid Isiolo County. ALERTNET/Isaiah Esipisu

Image Caption and Rights Information

ISIOLO, Kenya (AlertNet) – Katika kijiji cha Nambeyo kilicho katika sehemu kame ya jimbo la Isiolo inchini Kenya, aliyekuwa mfugaji wa ng’ombe Bw. Joseph Elila pamoja na mkewe Paulina wanapigapiga mtama ili kutoa nafaka. Wawili hao wamebadilisha mtindo wao wa kimaisha kutoka ufugaji hadi ule wa kukuza mimea zinzazostahimili ukame baada ya mifugo yao kuibiwa miaka miwili pita.

Sehemu hiyo ya Isiolo inajulikana haswa kwa ufugaji. Lakini riziki hiyo inatishiwa na visa vya wizi wa mifugo, hali ambayo wataalam wanasema kuwa inasababishwa na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa.

Wafugaji wanaoishi katika sehemu ambazo wanyama wamekufa  kutokana na ukame ama maafa mengine yanayohusiana na ukame, kwa mara nyingi wanavamia jamii jirani wakiwa na lengo la kuiba mifugo ili kujaza pengo hilo. Lakini, majanga yanavyozidi, na hata wizi wa mifugo kuongezeka, jamii zilizoadhirika  pakubwa wanatupilia mbali ufugaji kwa pamoja,  ili kutafuta mbinu zingeine za kujikimu kimaisha Hayo ni kulingana na Hussein Abdullahi, mwanasayansi mtafiti wa maswala ya wafugaji katika Future Agricultures Consortium na mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Pwani nchini Kenya.

Huko Isiolo, mamia ya familia wamefanya badiliko hilo, kwa msaada kutoka kwa serikali na mashirika yasiyo ya serikali kwa kuwapa ujuzi wa ukulima na misaada mingine. .

Elila na familia yake wameamua kujaribu ukulima. Angalau kwa njia hiyo, bwana huyo asema kuwa atajiepusha na kukabiliana na majirani ambao ni wezi wa mifugo wa mara kwa mara.

Simon Edonga, ambaye ndiye chifu wa eneo la Burat katika jimbo la Isiolo magharibi awashukuru wenyeji wa sehemu hiyo walioamua kubadilisha mbinu za kutafuta riziki. Lakini, viongozi wa jamii kwa msaada wa serikali za mashinani wanaendelea kujadiliana na jamii jirani kuhusu swala hilo wakiwa na lengo la kurejesha usalama na hata kukomesha uvamizi.Hata hivyo, Chifu Edonga ameapa kuwa serikali itatumia mbinu zote zile kuhakikisha usalama umerejea katika sehemu ya Isiolo. Aliongezea kusema kuwa wezi kadhaa wamifugo wametiwa mbaroni na wanasubiri hukumu

Takwimu katika kamati ya usalama na utatuaji migogoro wilayani Isiolo yaonyesha kuwa watu 298 wameuawa na majambazi wa kuiba mifugo katika jimbo hilo tangu mwaka wa 2009, na zaidi ya wanyama wapatao 25,000 kuibiwa.

Elila anakumbuka mwezi wa septemba mwaka wa 2010, ambapo majambazi waliojihami kwa silaha hatari walivamia vijiji tofauti katika jimbo la Isiolo na kuiba mamia ya wanyama, huku wakiwadhuru wachungaji. Baadhi ya wanyama walioibiwa walikuwa ng’mbe ishirini, mbuzi kumi na nane na kondoo wanne waliomilikiwa naye pamoja na babaye.

Wanyama hao ndio mali yote waliokuwa wanamiliki. Hivyo basi, kuibiwa kwa wanyama hao ilimaanisha kuwa riziki yao ilikuwa imechululiwa. Baba huyo wa miaka 30 na mwenye watoto watatu alizidi kusema kuwa amewahi shuhudia watu wengi wakiteseka bila huruma katika mikono ya wezi wa mifugo. Anakiri kuwa ameshuhudia watu wakifa na nyumba zikiteketea. Na kutokana na sababu hiyo, hangetamani kufuga wanyama kamwe.   

SHULE ZA WAKULIMA

Wafugaji hao wa zamani wameunda vikundi 16, ambapo kila kikundi kina wanachama 25 kuunda zile zinajulikana kama  Shule za Shamba za Wakulima.

Shule hizo hutoa elimu zikizingatia wazo kuwa “wakulima hujifunza vyema zaidi kwa kutizama kinachofanywa, pamoja na kujifanyia majaribio.” Hiyo ni kulingana na shirika la Umaja wa Mataifa la Chakula na Kilimo.

Nchini Kenya, hamu ya kielimu inaendeshwa na unaendeshwa na mashirika mbalimbali, ambayo yanasaidia wakulima kujifunza kwa kubadilishana mawazo wenyewe kwa wenyewe, haswa jinsi ya kuzalisha chakula katika mazingira tofauti. Kwa mfano, katika jimbo la Isiolo, elimu hiyo huendeshwa na shirika la ActionAid International Kenya kwa kusaidiana na serikali.

Hata hivyo, juhudi ya kwanza ya Elila ilikuwa kupanda mahindi pindi tu wanyama wake walipoibiwa. Lakini, mmea huo hungeweza kustahimili ukame wa mwaka wa 2011 ulioadhiri sehemu nzima ya Kaskasini Mashariki mwa nchi ya Kenya.

Hata hivyo, baada ya kupokea mafunzo kuhusu mimea zinazostahimili ukame kupitia Shule ya Shamba ya Wakulima ya Nekone, aliweza kupanda mtama ujulikanao kama gadam, na unaokomaa baada ya muda mfupi. Hivyo basi, alifanikiwa pakubwa.

Tayari, amevuna magunia 25 ya mtama yenye uzani wa kilo 90 kwa kila gunia. Sasa anatarajia kuuza mazao hayo.

Kampuni ya kutengeneza pombe ya Afrika Mashariki tayari imekubali kununua zao hilo kutoka kwa wakulima ilikuitumia katika kutengeneza pombe.

Waliokuwa wafugaji wengine wanajishughulisha na mambo mengine ya kilimo, ikiwemo ufugaji wa kuku na samaki.

KUNA ANAYEWEZA KUIBA SAMAKI

John Losunye, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Shule ya Shamba ya Wakulima ya Meritapen asema kuwa wanachama waliamua kuanza ufugaji wa samaki kwa sababu hakuna uwezekano wa magaidi kuvamia mtu yeyote, kutekeleza mauaji, ama kuchoma nyumba kwa lengo la kuiba samaki.

Bwana huyo asema kuwa hatarudia shughuli ya ufugaji hata kidogo. Anaonelea kuwa kuna usalama katika ukulima, na hivyo basi, atatumia raslimali aliyo nayo kutunza familia yake bila ya kuwa na wasiwasi dhidi ya wezi wa mifugo.

Kikundi chake kimeweka samaki wachanga elfu moja katika bwawa lao la kwanza. Wanatarajia kuuza samaki hao baada ya miezi minne.

Katika kipande chake cha ardhi hekta tatu, Losunye pia ameanza kukuza mimea zinazostahimili ukame kama vile uwele, maharagwe na pia vitunguu.

Mabadiliko hayo yanaambatana na maono ya serikali ya Kenya yajulikanayo kwa lugha ya kimombo kama Vision 2030. Maono hayo yameundwa ili kukuza uchumi wa nchi kwa kuhimiza wakulima kuekeza katika kilimo kisichotegemea mvua, kama mojawapo ya njia za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.

Vikundi vya wakulima vyaweza kujipatia usaidizi wa kifedha kupitia mpango huo, ingawa kikundi cha Losunye bado hakijawasilisha ombi la msaada.

Isaiah Esipisu ni mwandishi wa kujitegemea,huripoti katika maswala ya taaluma ya kilimo na mazingira, mkaazi wa Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->