×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Mashamba , mabadiliko ya tabia nchi yaathiri bonde la mto wa Tanzania

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Friday, 7 June 2013 16:21 GMT

Local farmers struggle to keep crops and animals alive, as river flow falls and salt water intrudes upstream

PANGANI, Tanzania (Thomson Reuters Foundation) – katika kijiji cha Langoni, Ashura Kilinga huamka saa kumi za alfajiri kila siku anaungana na wanawake wengine  kuchota maji kisimani juu ya mto uliokauka.

“Nisipoamka mapema, siwezipata maji ya kutosha kwa matumizi ya familia yangu,” alisema mama wa miaka 37 mwenye watoto wanne.

Maji yamepungua sana kwenye bonde la mto Pangani, linalohudumia  wakaazi takribani million 3.4 katika eneo  la zaidi yakilomita za mraba 48,000 kaskazini mwa Tanzania ikiwa ni pamoja na jiji la Arusha. Matokeo yake wakaazi  wanapata taabu kuhakikisha ustawi wa mazao na mifugo yao. Vilevile, migogoro inaongezeka kati ya wakulima, wafugaji na wafanya biashara.

Kilinga pia hukumbana na matatizo ya kifamilia. Mume wake anamshutumu kwa kuwa na mahusiano nje ya ndoa pindi anapoenda kuchota maji hivyo humpiga, licha ya jitihada za majirani kumzuia.

Awali Kilinga alikuwa akichota maji moja kwa moja kutoka mtoni, kama ilivyo sawia kwa wanawake wengine. Hata hivyo, kwa sasa si salama tena kufanya hivyo kwani kuna mamba wakali na maji yana chumvi sana. Mikondo mingi ya mto imekauka.

Kilinga ni miongoni mwa maelfu ya wakaazi katika bonde la mto Pangani ambao wanakabiliwa na uhaba wa maji. Walio wengi ni wakulima na wafugaji.

Wakaazi wengi wanaoishi kando ya mto huu  wenye urefu wa kilometa 500 wanakumbuka nyakati nzuri, ambapo hakukuwa na shida ya maji kabisa.

“Sijawahi kuona ukame kama huu,” alisema Saidi Ali, Mkulima na mfugaji mwenye umri wa miaka 57 kutoka kata ya mikunguni. Matatizo yote ya maji yameanza miaka michache iliyopita—kwa sasa ni vigumu kupata malisho ya mifugo.”

Wakulima wengine mkoani humo pia wanalalamikia kukauka chini ya mto na wingi wa mifugo kutoka maeneo ya jirani kutokana na wafugaji katika kutafuta malisho.

Baadhi yao wanashutumu wawekezaji wanaoendesha mashamba ya mkonge, zao ambalo nyuzi zake hutumiwa katika kutengeneza katani, kamba na mikeka.

“Hawa wakulima wakubwa ndiyo wanaleta chokochoko zote hizi,” alisema Rehema Mganga, ambaye ni mkulima mdogo katika kata ya Mikunguni ambaye kwa sasa analima muhogo na viazi baada ya mazao yake ya mahindi na maharage kuharibika. “Zao la katani linanyonya maji sana ardhini, lisiruhusiwe hapa” alisema.

ONGEZEKO LA JOTO, UPUNGUFU WA MVUA

Mamlaka za dola za Tanzania zingali zinatambua mambo mbalimbali yanayochangia upungufu wa maji katika bonde la mto Pangani, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa mashamba ya mkonge na mazao ya mifugo. Sababu nyingine ni pamoja na mabadiliko ya tabia nchi, ongezeko la watu na uharibifu wa misitu, wanasema.

“Hatuwezi kudharau tishio la mabadiliko ya tabia nchi, hata hivyo kuna ukinzani mkubwa wa rasilimali”, alisema Hamza Sadiki, afisa katika bonde la mto Pangani.

Alisema serikali inahitaji taarifa muhimu ili kutathmini matokeo ya mabadiliko ya hewa katika eneo hilo.

“Hamna tunaloweza fanya bila ya takwimu,” Alisema. “Tunajaribu kadiri ya uwezo kuwajengea uwezo wananchi. Ni lazima waelewe umuhimu wa kutunza mazingira kwa kubadilisha mwenendo wa maisha yao.

Wanasanyansi wanasema kwamba bonde la mto Pangani—lililotawanyika kuanzia mlima Kilimanjaro na Meru hadi bahari ya Hindi—huenda likaadhiriwa mno na ongezeko la joto na mabadiliko ya mfumo wa mvua, yanayohusishwa na mabadiliko ya tabia nchi.

Watafiti wanatabiri ongezeko la joto kati ya  nyuzi  1.8 na 3.6 kabla ya mwisho wa karne, vikiambatana na upungufu wa mvua  na ongezeko  la mvuke katika bonde hilo, kwa mujibu wa Pius Yanda, mkufunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam, pia ni mjumbe wa safu ya wataalamu wa mambo ya mabadiliko ya tabia nchi (IPCC). Mwenendo huu  unatarajiwa  kuwa na matokeo ya kupungua  kwa maji kutoka asilimia 6 hadi 10 katika kipindi cha miaka 10.

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Bonde la Mto Pangani, vituo vitatu vya umeme vilivyotegwa kwenye mto—na vyenye uwezo wa kufua megawati 91.3 za umeme au asilimia 17 ya mahitaji wa umeme nchini—kwa sasa vinazalisha asilimia 30 tu ya uwezo wake kutokana na upungufu wa maji.

MPENYO WA MAJI CHUMVI

Chini ya mkondo wa Mto Pangani, iliokuwa umesheheni bioanuai za bahari, unazidi kuwa na chumvi kwa kuwa mkondo wa maji ni dhaifu na unashindwa kusukuma maji chumvi kando.

Viongozi wa wilaya wanahusisha tatizo hilo na mabadiliko ya tabia nchi. “Ubora wa maji umeathirika sana,” alisema Mohamed Hamisi, Mhandisi wa maji wilaya ya Pangani. “Maji chumvi yamepenya zaidi ya kilometa 8 kutokana na kukua kwa kina cha bahari”

Maji safi yanasukumwa kwenda Pangani wakati wa kupwa kwa maji ili kuepuka kusukuma maji ya chumvi kutoka baharini,” alisema.

“Mikondo kadhaa iliyokuwa ikimwaga maji kwenye mto imekauka au imekuwa  ya msimu—kwa hiyo,mkondo wa mto Pangani umeathirika sana” Alisema Hamisi.

Wakazi wengi wilayani humo wanategemea visima kupata mahitaji ya maji, hata hivyo kujaa kwa maji ya bahari kumesababisha kuchumvika kwa maji hayo.

Viongozi wa bodi ya bonde la mto Pangani wamesema serikali imechukua hatua kadhaa kushughulikia tatizo la maji ikiwemo kutoa elimu kwa wakaazi juu ya umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji na kuzoea mabadiliko ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa ofisa wa bonde la mto Pangani, Sadiki, sera ya maji ya mwaka 2012 inataka ulinzi wa vyanzo vya mito na mazingira yanayozunguka ili kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya maji na matatizo mengine.

Hata hivyo wapinzania wanasema serikali bado haijaweka mfumo endelevu wa kutatua matatizo ya maji nchini.

Kizito Makoye ni mwandishi mwandamizi aliyepo Dar es Salaam, amebobea kwenye habari za mabadiliko ya tabia nchi na mambo ya uongozi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->