×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Mabadiliko ya hali ya hewa yahusishwa na ongezeko la magonjwa ya mifugo kwa binadamu

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 2 July 2013 15:37 GMT

Smallholder farmers attempting to adapt to climate change are facing new threat of animal diseases from their own livestock.

NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) – Wakulima wadogo wadogo ambao wamemiliki kilimo cha uhifadhi kama njia moja ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa wanakabiliwa na vitisho vya kiafya kutokana na magonjwa ya wanyama ambayo awali yalidhaniwa kuwa yameisha, wataalam waonya.

Kenya pia inakabiliwa na shinikizo hizi mpya, hasa watu maskini. Kulingana na wataalamu kutoka taasisi ya utafiti wa mifugo ya kimataifa (ILRI), magonjwa kama kimeta, homa ya Bonde la Ufa na homa ya kulala sasa ni kawaida katika mikoa inayokabiliwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Ripoti ya hivi karibuni ya ILRI yaonyesha ramani ya maeneo yenye magonjwa haya yanayojulikana kama zoonoses kwa kimombo, ama yale yanayoweza kuambukizwa binadamu kutoka wanyama.

Ripoti yaonyesha kuwa mikoa inayokabiliwa na mvua nyingi au ukame wa muda mrefu hasa, yamezindiwa na haya magonjwa, ikiwa asilimia sitini ni magonjwa ya binadamu na karibu asilimia sabini na tano ni magonjwa ya kujitokeza, yasema.

Hii ni kwa sababu binadamu na wanyama wa nyumbani wanazidi kuishi pamoja kwa sababu ya upungufu wa ardhi ya kilimo, wasema wataalam.

Wakati ardhi inapungua, “jamii zinalazimika kuishi pamoja na mifugo yao, hivyo kuongeza hatari ya magonjwa,” aelezea Jimmy Smith, mkurugenzi mkuu wa ILRI.

Ephantus Nkari kutoka kijiji cha Chiambaraga huko mashariki mwa Kenya ajiona mwenye bahati kuwa hai baada ya kuambukizwa ugonjwa wa kimeta kutokana na kula nyama ya moja wa ng’ombe wake.

Mwaka wa elfu mbili na kumi na moja, wakati Kenya ilikuwa yakabiliwa na ukame mbaya zaidi, yeye alipoteza ng’ombe arobaini, mbuzi kumi na nane na kondoo kumi na tano, kwa sababu ya kukosa kuwalisha.

Nilisikia uchungu kuona ng’ombe wangu aliyebaki akikufa,” asema baba huyu wa umri wa miaka sitini. “Niliamua afadhali nimchinje ng’ombe huyu niilishe familia yangu badala ya kuwaona wakikabiliwa na njaa. Nilichoma na kuila nyama lakini baada ya muda mfupi nikaanza kutapika na kuhara.”

Ugonjwa wa kimeta waweza kuua baada ya siku chache, lakini majirani wa Nkari walimkimbiza hospitali ambapo alipewa matibabu na akapona.”

Kwa bahati mzuri, mke na watoto wa Nkari walikuwa wameenda kuomba chakula kutoka kwa jamaa yao, kwa hivyo hawakuila ile nyama iliyoambukizwa.

Wataalam waonya kwamba sio tu kupitia lishe magonjwa haya yaweza kupitishwa kwa binadamu. Yengine yaweza kuambukizwa kupitia mimomonyoko ya mwili, aeleza Steve Kemp, mtaalam wa kisayansi katika chuo kikuu cha Liverpool nchini Uingereza.

Ugonjwa wa malale unaoathiri mifugo na kupitishwa kwa binadamu na mdudu unaoitwa inzi ya tse tse kwa kimombo, unahusishwa na mvua kubwa na makaazi ya kiasili kupungua, Kemp aeleza.

Kulingana na utafiti wa mwaka jana uliokuwa ukiangalia jukumu la mifugo katika nchi zinazoendelea, watafiti wa ILRI walihitimisha kuwa “magonjwa ya zoonoses yanaambukizwa wakati binadamu wanabadilisha jinsi wanavyolima na kutunza mifugo.”

“Kuna uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na magonjwa ya zoonoses kwa sababu upungufu wa ardhi unaongeza uwezekano wa magonjwa na wadudu kuenea,” asema Enos Esikuri, mtaalamu wa mazingira katika Benki ya Dunia.

Kulingana na Esikuri, magonjwa ya kuambukizwa ambayo hayakuwa ya kawaida muongo mmoja uliopita yaonekana kuongezeka katika maeneo nyevu na yale yanayokabiliwa na ukame katika Kenya na nchi zingine Pembeni mwa Afrika.

“Hii ni kwa sababu Afrika yaonekana kuwa suluhisho la mwisho la kilimo hivyo makampuni ya kimataifa yanang’ang’ania mashamba ili kukuza kilimo cha kuuza nje,” asema. “Lakini hii inaacha nchi zikiwa hatarini kwa mabadiliko ya hali ya hewa, uhaba wa chakula, mfumuko wa bei, gharama kubwa ya maisha na kukosekana kwa utulivu.”

Kusanyiko la maswala ya adhi Kenya, KLA, na ambalo silo la kiserikali, lateta kwamba jamii hutengwa wakati maamuzi ya kukodisha au kuuza ardhi kwa wawekezaji wa kigeni yajadiliwa, hivi kusababisha idadi kubwa ya watu kuhamishwa makwao.

Hata hivyo, si kila mtu akubali kuwa kuna uhusiano kati ya mabadiliko ya hali ya hewa na magonjwa ya zoonoses.

Wafanyakazi wa mtandao unaotumia teknolojia ili kulinda wanyama wabeba mizigo (KENDAT), na ambalo ni shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia ustawi wa wanyama wa nyumbani nchini Kenya, wasema kuenea kwa magonjwa haya ni kwa sababu ya kupungua kwa huduma za ugani na ukosefu wa madaktari wa serikali wa mifugo kuhudhuria wanyama.

“Sidhani kwamba kuongezeka kwa magonjwa haya ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa lakini pengine ni kukosekana kwa huduma za wanyama huko mashambani,” asema Pascal Kaumbutho, afisa mtendaji mkuu KENDAT. “Utafiti zaidi unahitajika ili kupata kiunganishi na mabadiliko ya hali ya hewa.”

Lakini Kaumbutho akubali kwamba wadudu wanaohamahama sasa wamekuwa wa kawaida zaidi kwa sababu ya kile anaamini ni mabadiliko ya hali ya hewa, na kwamba ni vigumu sana kutabiri jinsi wanavyoshambulia.

“Wakati hali ya hewa inakuwa joto wadudu waliokuwa wakinawiri sehemu za anga ya chini sasa wanapanda sehemu za juu na kusababisha majanga makubwa kwa wakulima,” asema.

Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira mjini Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->