×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Vijiji vya Kenya vyavuna maji kutoka ukungu

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Monday, 9 September 2013 17:00 GMT

Paul Tomboi, 18, observes fog harvesting equipment at Olteyani village in Kenya's Kajiado County. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

Collector curbs the need for women to walk to find water in arid areas and could help families adapt to changing climate conditions

OLTEYANI, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Mawingu ya unyevu yanayoning’inia juu ya milima wa Ngong', ambayo ni miamba ya ardhi katika pindo za jiji la Nairobi, kwa muda mrefu yametolea jamii ya Wamaasai umande ambao huchipua nyasi kama lishe la mifugo yao.

Hata hivyo, hivi karibuni, Lucy Lotuno na wachache wa rika yake wamegundua kwamba ukungu pia unaweza kutoa maji safi ya kunywa hatua chache kutoka kwa manyumba yao.

Nyanya huyu wa wajukuu tisa, hivi karibuni alikuwa mwenye furaha alipoonyesha kifaa cha kuvuna ukungu katika kijiji chake cha Olteyani katika kata ya Kajiado, eneo kame lililo kusini-magharibi mwa jiji kuu la Kenya.  

Kifaa hiki ambacho kwa sasa hutumikia wachache, hukamata ukungu katika nyavu na kuzikusanya kama maji safi kwa mapipa ya maji yaliyowekwa hapo chini. Ikitegemea wiani ya ukungu, kitengo kimoja kinaweza kukusanya maji inayowatosha watu kama ishirini hadi arobaini kwa siku.

“Niko na furaha kwa sababu maji safi iko karibu na nyumbani mwangu badala ya kutembea mbali kutafuta maji,” asema nyanya huyu wa miaka arobaini na tano. “Naweza kupumzika na kufanya kazi nyingi za nyumba kuliko mbeleni.”

Kama wanawake wengine wengi katika maeneo makame ya Kenya, kutafuta maji ni changamoto la kila siku ambalo lachokesha kwa sababu ya kutembea mbali kutafuta maji, ambayo kwa mara mingi hutumiwa pia na mifugo na wanyama pori.

Kulingana na Lotuno, kuchota maji kutoka vyanzo vya mbali imekuwa ni desturi ya maisha yake tangu alipokuwa mtoto.

Hii ndiyo sababu anakuwa macho inapokuja kulinda kifaa hiki cha kuvuna maji, kilicho hatua chache kutoka kwa makaazi yake. Wageni hukabiliwa na nyanya huyu akitaka kujua sababu yao ya kutembea hapo.

Safu ya matundu ambayo imewekwa kwa milingoti miwili iliyopandwa ardhini hutega matone ya maji ambayo hukusanyika kwa kifaa cha ugavi, halafu maji yatiririka kwenye pipa.

Maji haya yako tayari kutumika, kwa mujibu wa Bancy Mati, profesa katika chuo kikuu cha kilimo na teknologia cha Jomo Kenyatta, ama JKUAT.

MAJI ENDELEVU

“Uvunaji wa ukungu ni njia endelevu ya kupunguza shinikizo za maji lakini bado haitumiki sana,” asema.

Yeye ni mkurugenzi wa utafiti wa maji huko JKUAT na ni mmoja wa waanzilishi wa teknolojia ya kuvuna ukungu nchini Kenya, akishirikiana na idara ya hali ya hewa ya Kenya (KMD), na PedWorld, shirika lisilo la kiserikali ambalo lilichangia nyavu za kutega maji.

Chuo kikuu cha JKUAT kilisaidia kufanya utafiti wa uwezekano wa kuvuna ukungu katika Olteyani, kikishirikiana na jamii vijijini, asema.

Mati asema teknolojia hii inatumika Ujerumani, Chile na Tanzania. Kifaa kimoja kinaweza kukusanya lita mia nne hadi elfu moja kwa siku, kulingana na ukubwa wa muundo wa matundu na anga wiani za ukungu, aliongeza.

Kifaa hiki cha Olteyani ni cha kwanza Kenya na kilifadhiliwa na KMD. Lakini wanaounga mkono teknolojia hii wana matumaini ya kuanzisha vifaa zaidi na kubwa kwa miaka mitano ijayo vijijini Kenya. Kulingana na KMD, kifaa cha Olteyani kiligharamiwa na dola mia tatu za marekani.

Ukungu hupatikana wakati hewa iliyochopozwa hushindwa kuweka mavuke ya maji, hivyo kutengeneza mawingu yaliyo karibu na ardhi.

Zinapatikana nchi tambarare zilizo na milima ya pekee ambayo hutega na kushikilia mawingu haya, au wakati pepo zenye nyevu zinaporushwa katika kanda za juu, kulingana na ripoti ya mpango wa kuhifadhi vyanzo vya maji nchini Kenya, iliyotayarishwa na serikali ikishirikiana na mpango wa umoja wa mataifa wa mazingira, UNEP.

“Ukungu hupatikana usiku na asubuhi mapema,” aelezea Peter Ambeje, naibu mkurugenzi, KMD. “Inakuwa mingi katika miezi ya Mei na Septemba.”

KUPUNGUZA SHINIKIZO ZA VIFAA

Wingi wake katika maeneo kama Olteyani na maeneo mengine ya nchi inamaanisha maisha bora kwa wakenya kama Lotuno. Na kama kukusanya maji kutoka ukungu itaendelea kama wataalam wanavyoamini, inaweza kupunguza shinikizo za rasilimali nchini, wasema wataalam.

Kulingana na Umoja wa Mataifa, Kenya ni nchi yenye uhaba wa maji, wakati ripoti za mashirika kama vile UNEP husema tatizo hili limekuwa mbaya zaidi katika miongo ya hivi karibuni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa.

“Ujuzi wa kisayansi unaoweza kuleta maji safi ndio lengo la serikali kulingana na mpango mpya wa uhifadhi wa rasilimali,” asema Alice Kaundia, katibu wa mazingira Kenya. “Serikali itasaidia uvunaji ukungu kwa kutenga fedha za utafiti kupitia KMD.”

Utafiti unaonyesha Kenya yazidi kuwa maskini kwa sababu ya kutumia vibaya mali asili, ikiwa ni pamoja na maji.

“Wingi wa umaskini Kenya ni kutokana na kutumia vibaya rasilimali ya asili,” alisema Achim Steiner, mkurugenzi mtendaji UNEP wakati wa mkutano wa waandishi wa habari mjini Nairobi mwishoni mwa mwezi Julai.

 Alitoa wito kwa watunga sera kuhakikisha usawa kwa maendeleo na haja ya kutoa huduma za msingi katika nchi ili “kuweka nchi kwa laini ya amani.”

UNEP inazidi kuonyesha ongezeko la shinikizo katika vianzo vya maji, licha ya onyo za mara kwa mara kuhusu udhaifu wa mazingira. 

Ripoti ya UNEP inayotoa ramani ya vianzo vya maji yaonyesha kuwa rasilimali iliyo karibu na maeneo ya mijini ina ongezeko la dhiki kutokana na makaazi mapya kwa sababu ya watu kuhama kutoka vijijini ili kujikimu kimaisha.

Kulingana na ripoti hii, zaidi ya asilimia sabini na tano ya wakaazi wa Kenya hujilimbikizia katika maeneo yenye uwezekano mkubwa kiuchumi. Maeneo haya yawakilisha tu asilimia ishirini ya ardhi ya Kenya.

“Haya maeneo huwa kwenye misitu na vyanzo vya mabonde ya mito mikubwa, hivi kusababisha shinikizo zaidi kwa rasilimali za asili,” yasema ripoti. “Hii husababisha hasara ya ardhi, kuongezeka kwa mahitaji ya malisho, kupungua kwa uzalishaji wa kilimo na kuongezeka kwa viwango vya uchimbaji maji.”

Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira na hufanyia kazi Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->