×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Kenya kame yabadilisha uchomaji makaa na kilimo cha maembe

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 23 October 2013 14:45 GMT

Kawira Cianjira tends a flowering mango plot at her village in Mananja, Eastern Kenya. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

Planting mango trees can absorb carbon, cut deforestation and help farmers through the dry season, experts say

MASINGA, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Wakati Njeri Njoka alipoolewa miaka ishirini iliyopita, kuni haikuwa shida kupata. Siku hizi hata hivyo, yeye huchokora visehemu kwa mabanda ya kuchongea mbao huko katika kijiji chake cha Igoji. Kupatikana ni shida.

Kuni kwa muda mrefu imekuwa ikitumika kama nishati ya kupikia katika nyumba nyingi vijijini Kenya. Lakini mahitaji ya mbao imemaliza miti iliyokomaa, wakati makaa nayo imemaliza miti midogo. Majani chai - ambayo inahitaji joto kutengeneza - pia hutumia kuni. Kwa hivyo, Njoka mwenye umri wa miaka arobaini na mbili lazima atafute nishati mbadala yenye bei nafuu.

“Kuni si rahisi kupata siku hizi,” asema mama huyu wa watoto watatu.

Kwa bahati nzuri, aelezea, serikali inaingilia kumaliza ukataji wa miti wa magogo na kusimamia kiasi gani kinaweza kutumika kutengeneza chai. Lakini kumaliza uchomaji makaa, afikiria, ni jambo bado lasumbua.

Katika chini ya Mashariki Kenya peke yake, mifuko kama elfu kumi na mbili ya kilo tisini husafirishwa mji mkuu Nairobi kila siku, kwa mujibu wa kikundi cha kuzuia mabadiliko ya hewa, KCCN. Watu wengi hugeukia uchomaji wa makaa wakati ajira zingine kama ukulima unashindwa kuleta mapato ya kutosha.

Hata hivyo, idadi kubwa ya Wakenya imegundua njia mbadala ya kujiongezea mapato badala ya kuchoma makaa – kilimo cha maembe.

Wakati kama huu, Sila Mutisya, angekuwa akitayarisha shamba lake kwa musimu wa kupanda katika shamba lake huko Masinga, mashariki mwa chini ya Kenya.

Badala yake, yeye anakagua shamba lake la maembe lenye miti iliyo na urefu wa futi saba, na ambayo yapapaa na maua ya rangi nyekundu na manjano ikionyesha dalili ya zao nzuri.

Kwa miaka mingi, ukulima wa chakula cha lishe umekuwa mgumu mno kwa baba huyu mwenye umri wa miaka sitini na tatu, na hata majirani wake, kwa sababu ya hali ya hewa isiyo ya uhakika. Hata mazao sugu yanayoweza kuvumilia ukame yaonekana kushindwa, asema, na hivyo akageukia uchomaji makaa ili kujiongezea mapato.

Ni mpaka alipotembelea rafiki yake anayelima maembe huko Malindi katika pwani ya Kenya alipogundua kilimo cha matunda chaweza kumuongezea mapato ya kifedha.

KUBADILISHA NA MAEMBE

Rafiki yake alimueleza kuwa kituo cha utafiti cha serikali, KARI, kiliwaletea aina ya maembe inayoweza kukua katika maeneo kame, kukomaa haraka na kuzalisha maembe makubwa na matamu.

Joseph Njuguna, mtaalam wa matunda KARI, asema maembe haya mapya yaweza kuzalisha mara kumi zaidi ya yale ya kwaida na kutoa maembe elfu moja hadi elfu moja mia mbili, kwa mti kila msimu.

Mutisya sasa anangojea kuvuna maembe yake kutoka kwa shamba lake la ekari mbili.

“Januari ndio uchomaji wa makaa uko juu zaidi lakini mimi nitakuwa nikivuna maembe yangu kwa vile tayari yako na maua,’ asema baba huyu wa watoto watano.

“Niligeukia uchomaji wa makaa kwa sababu ndio wengi wetu hujikimu kimaisha,” asema. “Sikujua ninaharibu mazingira kwa sababu ya kukata miti.”

Kituo cha utafiti wa misitu, KEFRI, chasema kilimo cha maembe kinafaa kwa sababu kina uwezo wa kuhifadhi asili na pia kujaribu teknologia mpya za kilimo zinazoweza kuchangia usalama wa chakula.

Kupanda miti – ikiwa ni pamoja na maembe – inasaidia kunyonya gesi mbaya ya kaboni kutoka kwa anga, huku aina mpya ya maembe ikisaidia kwa mapato katika sehemu kame zinazoshindwa kulima mazao ya lishe kama vile mahindi.

“Kilimo cha maembe ‘kinaongeza misitu’,” asema afisa wa KEFRI, Samson Mogire. “Pia ni njia endelevu ya kuhifadhi unyevu katika ardhi hasa katika maeneo kame.”

Lakini kilimo cha maembe pekee hakiwezi kusaidia familia, wasema wataalam, wakiongeza kwamba wakulima wanafaa kuchanganya kilimo cha matunda na kile cha chakula cha lishe.

“Maembe huiva wakati wa kiangazi na kwa hivyo husaidia wakulima kujipatia mapato wakati hawana chakula,” asema Anne Maina, mshauri wa mambo ya usalama wa chakula, Nairobi.

“Hata hivyo wakulima wanapaswa kuwa waangalifu wasiachane na kilimo cha chakula kwa sababu bado ni muhimu kwa kushikilia lishe bora.”

 Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira mjini Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->