×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Bei duni ya kaboni yakataliwa na Wakenya vijijini wakidai malipo ya uhifadhi

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 13 February 2014 11:57 GMT

Amid disappointment over thin revenues from carbon credits, experts say initiatives that pay communities to protect ecosystems could be a good alternative

NAROMORU, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Purity Irungu na wanawake wengine kijijini Kamangura huko Kenya ya kati, walikuwa wakitembea umbali wa kilomita kumi kukusanya kuni za kupikia.

“Nilikuwa nahitaji kuni kiasi cha lori ndogo kila mwezi,” alielezea mama huyu wa umri wa miaka thelathini na nane. “Lakini kuni hazikuwa zinatosha, hivyo tulikata miti.”

Siku hizi, shukrani kwa jiko linalookoa nishati, Irungu hatembei kwa msitu sana kukusanya kuni. Yeye amejiunga na mradi mbunifu unaoitwa malipo kwa ajili ya mfumo wa ikologia, ama PES, ambao huwatia wenyeji moyo kwa kulinda maliasili.

Kwa mujibu wa Tony Simons, mkurugenzi mkuu, wa kituo cha maswala ya misitu, huko Nairobi, ama ICRAF, PES hufanya kazi kwa njia tatu.

Jamii inaweza kulipwa ili kuacha shughuli ambazo huhatarisha mazingira, zaweza kulipwa kutenda kitu kipya ambacho kinasaidia mazingira. La tatu ni kwamba, jamii inaweza kushirikiana katika shughuli zinazofaidi mazingira, kama vile jiko zilizo na nishati fanisi.

“Shughuli hizi lazima zikuwe na mabadiliko kwa wakulima, mkuu wa kijiji, ama mkaazi wa msitu,” Simons alisema. “PES yaweza kulipwa kama fedha, au kutoa motisha na kusambaza ujuzi.”

Wataalam wasema PES yaweza kuwa njia mbadala ikilinganishwa na miradi inayolenga kuzalisha mapato kupitia uuzaji wa kaboni. Hii miradi imekuwa si ya kutegemea, kwa sababu bei ya kaboni imetumbukia katika kipindi cha miaka michache iliyopita.

Huko Kamagura, shirika lisilo la faida, ama Nature Kenya, likishikana na kikundi cha kulinda msitu wa Gathiuru, kilibembeleza wanakijiji kuacha uvunaji wa kuni katika msitu na badala yake wakapewa meko inayotumia nishati ya chini, na ambayo ni ya bei ya chini.

Wanachama waliweza kununua meko kwa bei iliyopunguzwa ya dola moja nukta saba, huku ikiwa ni bei ya chini ikilinganishwa na ya soko ambayo ni dola thelathini, alieleza Harriet Gichuru, meneja wa Nature Kenya huko Gathiuru. Fedha hizi hutumika kununulia wanachama wapya meko zaidi, na ambayo huundiwa vijijini.

Chini ya mpango huu, wanakijiji huruhusiwa tu kukusanya kuni katika maeneo waliotengewa ili kuhakikisha uhifadhi wa msitu.

Siku hizi mimi hutumia kuni ninazokusanya kutoka shamba langu kwa sababu sina haja sana,” alieleza Irungu. “Mimi hutumia muda niliokuwa nikikusanya kuni kwa msitu kufanya kazi kama kulisha mifugo, kuchota maji, na hata kufanya kibarua.”

KUPOTEZA MITI NI TISHO KWA CHAKULA, NDEGE

Gichuru, wa Nature Kenya, alihusisha uporaji wa msitu wa Gathiuru na kushuka kwa mazao ya chakula ya lishe huko kijijini mwa Irungu.

Ikiwa kiunoni mwa msitu wa mlima wa Kenya, kijiji kimepoteza chakula kupitia hali mbaya ya hewa na ukame wa muda mrefu – hali ambayo wazee wa kijiji hulaumu kwa upotevu wa miti katika msitu wa Gathiuru.

Gichuru alisema kuwa msitu duni pia unatisha Ndege inayoitwa Abbott Starling, ambayo hupatikana tu katika msitu wa mlima wa Kenya na sehemu za Tanzania, na sasa inakabiliwa na kutoweka.

Msitu huu - ambao pia unasimamiwa na kikundi cha uhifadhi wa mlima wa Kenya na ambao ni wa kijamii - ni muhimu kwa kuhifadhi ndege baadhi ambazo ni za kipekee duniani, ikiwa ni pamoja na Abbott Starling.

“Inapenda kukaa juu ya miti,” alieleza Gichuru. “Lakini miti mirefu imetoweka kwa sababu ya upasuaji wa mbao na uvamiaji wa msitu.”

Hata hivyo, Gichuru na wanawahifadhi wengine waligundua kwamba ni lazima wawashawishi wakaaji wa vijiji kama Kamangura kuacha kupora rasilimali ya misitu.

Hii haikuwa rahisi kwa sababu kuzuia jamii kutotumia rasilimali yaweza kuathiri maisha yao tele.

Basi waliamua kujaribu PES, huku wakitumai itawashawishi Irungu na wenzake waachane na msitu.

Zaidi ya nyumba mia moja thelathini na sasa zina jiko za kuhifadhi nishati, na zaonekana kutimiza lengo.

“Uvamizi haramu wa msitu wa Gathiuru sasa umepungua,” Gichuru alisema. “Hii inathibitisha kwamba jamii iko tayari kushiriki katika uhifadhi kama wanaonyeshwa njia mbadala ya kutafuta lishe.”

 

 

‘WATU HUTENGA KAZI ISIYOLIPA’

Kituo cha maswala ya misitu Kenya, KFS, chasema miradi ya PES inawekezwa katika minara tano ya maji Kenya - na ambayo ni maeneo ya misitu - shukrani kwa pesa ya wahisani ya mabadiliko ya hali ya hewa na bajeti ya kitaifa.

Kwa mujibu wa Simons wa ICRAF, gharama halisi ya tani ya kaboni inayorushwa kwenye anga ni kama dola hamsini au sitini. Wakati huo huo, inachukua kama lita elfu mbili za maji kuzalisha tani ya kaboni. Hivyo, kama bei ya kaboni ni dola chache, kama ilivyo sasa, hii inaweka maadili ya maji kwa bei duni pia.

“Kwa nini mkulima mdogo au mkaazi wa msitu au meneja wa kijiji adumishe rasilimali inayoleta faida kwa kila mtu kwa bei ya chini hivi? Watu huacha kufanya mambo ambayo haileti malipo,” Simons alisema.

KFS nayo yasema PES inawezekana Kenya kwa sababu viwanda vingi hutegemea mazingira ya misitu kwa njia moja au nyingine.

Mkurugenzi msaidizi wa KFS, Daniel Nbithi, alisema maji na uhifadhi wa misitu ni kati ya sekta ambazo Kenya inatekeleza PES. “Kilimo chetu hutegemea mvua, lakini uundaji wa mvua husukumwa na misitu yetu,” alisema.

UTATA WA KABONI

Wakati huo huo, mawazo yamegawanyika juu ya mustakabali wa miradi ya kaboni huku Kenya. Mwishoni mwa mwezi wa Januari, Benki ya Dunia ilitoa malipo ya kwanza ya kaboni, ikiwa ni kutokana na mradi wake wa Kenya Agricultural Carbon Project.

Hii ikiwa ni ya kwanza tangu kuwekwa upya kwa mifumo ya kaboni inayoendeleza ardhi, mradi huu unatarajiwa kutoa mapato kama dola elfu sitini kabla ya mwaka wa elfu mbili na kumi na saba, ingawa haijulikani ni kiasi gani kitawafikia wakulima zaidi ya elfu sitini wanaoshiriki.

Si wote wanaamini watapata faida. Miaka mitatu iliyopita, Gerald Gwatu alijua kupitia kwa mkutano wa Chifu, angeweza kupata fedha kupitia miradi ya kijiji ya upandaji wa miti. Basi naye akatengeneza shamba lake la msitu huko kijijini mwake, Mwati, Kati ya Kenya.

“Unaona miti hii ni mikubwa na inatosha kuvuna kwa ajili ya kuni na makaa,” alisema baba huyu wa umri wa miaka thelathini na nane. “Lakini mimi sijapata malipo yoyote kutokana na mradi wa kaboni. Itakuwa bora mimi nitumie miti yangu kwa madhumuni mengine yanayoniletea fedha.”

Wafuasi wa ‘malipo kwa ajili ya uhifadhi’ wasema PES inaweza kuwa mbadala wa misingi ya kaboni, hasa bei ya kaboni ikikaa kuwa duni.

“PES ndio mwelekeo kwa sababu inafanya kazi na jamii kwa siku hadi siku,” alisema Joseph Ngondi wa shirika la Kenya linaloshughulikia mazingira na ambalo si la kiserikali.” Miradi ya kaboni haiwezi kunawiri Afrika kwa sababu inatumia misingi ya nadharia.”

Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira mjini Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->