×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Baada ya kupoteza misitu yao, wamaasai nchini Kenya wakabiliana na hali

by Pius Sawa | Thomson Reuters Foundation
Saturday, 15 March 2014 01:15 GMT

Leonard Leina, who lives in the Rift Valley's Transmara area, stands amid his plot of boma rhode grass, growing as fodder for his livestock. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Pius Sawa

Image Caption and Rights Information

Cutting of trees in the Transmara contributes to changing weather conditions, and changing ways of life

TRANSMARA, Kenya (Thomson Reuters Foundation) – Karibu miaka kumi sasa,Peter Ole Nembo aliacha kuhama hama na mifugo wake akitafuta majani na maji wakati wa kiangazi, baada ya serikali kusitisha umiliki wa kijamii wa ardhi ya wamasai ipatayo kilomita 2,850 mraba na kugawia kila mtu sehemu yake.

Wakati huo eneo hili la Kilgoris, kaunti ya Narok, lilikuwa na misitu yenye miti mikubwa iliyoleta mvua nyingi iliyojaza mito na mabwawa. Lakini wakati ardhi iligawiwa watu, miti ilikatwa ovyo ili kutayarisha mashamba ya kulima kwa sababu hakuna mtu aliyewashauri juu ya umuhimu wa kuhifadhi miti.

“Wenye mashamba waliwaajiri vibarua kukata miti, na hawakujali kuhifadhi hata mti mmoja manake walikuwa tu na haja ya kuchoma mkaa na kupasua mbao,” alisema Nembo anayemiliki ekari 53 za shamba katika kijiji cha Kirkamat, eneo la Transmara.

Matokeo yake ni athari za mabadiliko ya tabianchi kama vile mafuriko, kiangazi, mmomonyoko wa udongo, na mvua zisizotarajiwa.

Nembo anasema kuwa muda wa kiangazi umekuwa mrefu zaidi siku hizi, na ni mara kwa mara.

“Tulikuwa tukishuhudia kipindi kimoja tu cha kiangazi ambacho kilikuwa mwezi wa Octoba. Lakini siku hizi, ni lazima kuwe na kiangazi kila mwezi. Hata mvua ikinyesha, inaweza nyesha kwa karibu juma moja, na siku zilizosalia huwa ni kame.” Alisema.

Samuel Ole Seme, ambaye ni jirani yake, anakiri kwamba hali ya hewa imekuwa ya kutoeleweka.” Tulikuwa tukijua kwamba kuna miezi ya mvua na miezi ya ukame. Sasa ni wakati ambapo Mola akipenda, atatupa mvua, na akipenda atatupa kiangazi,” alisema Ole Seme.

Jamii zinazoishi katika eneo hili zinafahamu kwamba ukataji wa miti ambayo husaidia kudhibiti mvua na mabadiliko ya hali ya hewa imechangia kwa mabadiliko yaliyopo.

“Tulikata miti yote kwa ajili ya kuchoma mkaa, na mvua ikapotea,” alikiri Emily Kokoyo.

UTABIRI BORA WA HALI YA HEWA

Ili kuisaidia jamii kustahimili hali hii ya mabadiliko, taasisi ya utafiti wa kilimo nhini Kenya, KARI, ikishirikiana na Kituo cha kimataifa cha utafiti cha Canada, IDRC, wamefanya utafiti wa miaka mitatu wakikusanya data ili kuweza kutoa utabiri ya miaka mingi ya hali ya hewa na kutoa mikakati ya kuisaidia jamii kukabiliana na hali zinazobadilika.

Uchunguzi wao ulipendekeza kuwa eneo la Transamara litapata mvua nyingi siku zijazo, na hivyo, kuna umuhimu wa aina mbalimbali ya kilimo kuanza kutekelezwa.

Michael Okoti, ambaye ni mratibu wa kitaifa wa utafiti wa mazingira na mabadiliko ya tabianchi katika taasisi ya KARI, alisema kuwa, uchunguzi huo ulitizama hatari zilizokumba familia pamoja na hali ya mazingira na kutoa ripoti kamili yenye suluhu.

Mradi huo wenye kugharimu shilingi milioni 95 sarafu ya Kenya, ulijumuisha maeneo matatu kukiwemo, Transmara, Ijara na Tana Delta, ambayo ni maeneo kame. Baaada ya kutoa taarifa hiyo, kilichofuata ni kusaidia jamii namna ya kukabiliana na hali ingawa haikuwa kazi rahisi, anasema Okoti.

SERA KUBADILIKA, NA TAMADUNI KUBADILIKA

“Sera hubadilika haraka kuliko tamaduni. Tamaduni hujivuta sana,” alisema. Kwa hiyo tuko na sera inayosema kila mtu amiliki ardhi, na sio ya kijamii tena. Kwa hivyo, una shamba ekari 50 na hauwezi kuhamia kwa jirani yako, ilhali bado una ile desturi ya kumiliki idadi kubwa ya mifugo, na malisho ni changamoto.”

Kinachokera sana ni kuwa, huku idadi ya mvua katika eneo hili ikisalia kuwa dhabiti, wakati wa mvua hiyo kunyesha kumebadilika mno.

“Siku za mvua kunyesha zimebadilika. Unaweza kuwa na kiwango kilekile cha mvua, tuseme milimita 1,000 katika msimu wa mvua wa Mwezi Machi na Aprili, lakini mvua hiyo yote inanyesha kwa siku moja. Hii haina manufaa kwa kilimo,” alisema Okoti.

Kwa hivyo, kinachoweza kuwasaidia wakulima kukabiliana na hali hii, ni upanzi wa miti, ambapo tayari wakulima wamepewa mbegu kwa vikundi.

“Tunaona kwamba tutakuwa na mvua nyingi sana siku zijazo, na kwa wakati huu, ardhi iko tupu bila miti,” alisema Okoti. Hii inaleta shida kama mmomonyoko wa udongo-lakini upanzi wa miti utasaidia kudhibiti mchanga, kuboresha mifumo ya maji, na kuzalisha mimea, alisema.

Lengo lingine la upanzi wa miti ni kurejesha hali ya awali ya hewa, ili kupunguza mwendo wa watu kutafuta maji.

UPANDAJI WA MITI NA AINA MPYA YA MIMEA

Benjamin Ole Kipas, mmoja wa wakazi wa eneo hili, ametenga ekari 4 za shamba lake kwa ajili ya miti. Amepanda miti 7,000 ya kizungu, na 3,000 ya kienyeji. Anasema kuwa miti ya kizungu ni ya kuuza na ile ya kienyeji ni ya kudhibiti hali ya mazingira.

Ni sera ya seriakali kwamba kila mtu ni lazima apande asilimia kumi ya miti katika ardhi anayomiliki.

Peter Ole Nembo, kwa upande wake, ana aina tano za majani ya mifugo shambani mwake. Majani haya pia huzuia udongo kusafirishwa na maji wakati wa mvua. Amepanda pia aina tano za maharagwe ambayo yanakomaa upesi na yanarudisha rutuba mchangani.

Emily Kokoyo Naye ametenga karibu ekari moja ya shamba lake kwa ajili ya mimea na anasema hii ni ajira mpya kwa wanawake katika jamii ya kimaasai.

“Mifugo hapa ni milki ya wanaume, lakini sasa hii ni nzuri manake inanisaidia,” alisema. Ameweza kuuza viazi vitamu na maharagwe kutoka shambani mwake na kufungua duka ambalo linamletea kipato cha kila siku. Aina ya viazi hivi hukomaa kwa miezi mitatu,na ni nzuri kwa mvua chache.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->