×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Kufufuliwa kwa vyama vya mashirika kwaleta matumaini kwa wakulima nchini Rwanda

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 8 May 2014 07:00 GMT

Small farmers gain access to bank loans, farm inputs, markets and advice through Rwanda's growing cooperative movement

KIGALI (Thomson Reuters Foundation) – Katika nchi inayoendelea kupona kutokana na mauji ya kimbari iliyopelekea vifo vya asilimia 20 ya idadi ya wananchi miaka 20 iliyopita, wakulima wadogowadogo wamepata matumaini mapya katika wimbi la vyama vya mashirika ambayo tayari zimeimarisha hali ya maisha nchini Rwanda.

Ukuaji stadi wa vyama vya mashirika nchini Rwanda uliadhirika mno kutokana na mauaji ya kimbari mnamo mwaka wa 1994. Hayo ni kwa muujibu wa utafiti wake Espérance Mukarugwiza, uliodhaminiwa na Shirika la Kazi Duniani (ILO).

Lakini kutokana na mazingira mema kisheria iliyowekwa na serikali katika miaka za 2000, na misaada kutoka mashirika endelevu duniani, wakulima kwa sasa wanaweza kupata mikopo za benki kupitia vyama vya mashirika, ambavyo idadi yake inazidi kuongezeka. Pia, wanapata pembejeo za kilimo, soko, na mawaidha.

Mukankiko Odeth, ambaye ni mkulima mdogo kutoka wilaya ya Kirehe Mashariki mwa Rwanda, asema kuwa kutokana na mabadiliko ya tabianchi, sio rahisi kujua mbegu bora ya kupanda, kwakati wa kuzipanda, na jinsi ya kupanda bila ya mafundisho, pembejeo, na soko.

Wakati wa kuvuna, wanachama wa vyama vya mashirika huhifadhi nafaka yao katika ghala. Wakati nafaka hiyo inapouzwa, wakulima hulipwa pesa zao, lakini asili mia kidogo ya pesa hizo husalia katika shirika. Kiwango hicho hutumika kama hisa miliki zinazoweza kutumika kama dhamana ya kukopa mikopo kwa wanachama.

Kulingana na Emma Kombewa wa shirika la AGRA, uzoefu umedhihirisha kuwa benki zaweza kuwapa wakulima mikopo kupitia vyama vya mashirika, ama vikundi vingine kama hivyo bila kuhitaji vyeti kwa dhamana.

AGRA husaidia vyama vya mashirika vipatavyo 214 katika wilaya nane nchini Rwanda kupitia shirika la Rwanda Development Organisation (RDO) na Rwanda Rural Rehabilitation Initiative (RWARRI), kwa kujenga uwezo, kuwafunza usimamizi wa kifedha, mpangilio wa biashara na uongozi bora.

Mnamo mwaka wa 2005, serikali ya Rwanda iliunda jopokazi ili kubuni mfumo wa kuendeleza vyama vya mashirika. Mnamo mwaka wa 2008, jopokazi hilo lilibadilishwa na kuwa Rwanda Cooperative Agency, ambayo hivi sasa hutoa uongozi wa kisheria unaotumiwa kufufua vyama vya mashirika.

Gasirabo Claver wa RDO asema kwamba kutokana na mabadiliko ya tabianchi, idadi ya watu inayozidi kuongezeka, na nyakati ngumu kimaisha, nchi hiyo ilikuwa tayari imekosa chakula cha kutosha. Lakini hivi sasa, wakulima ambao wako chini ya vyama vya mashirika wanazalisha chakula cha kutosha kulisha familia zao na hata kuuza.

RDO, ambalo ni shirika lisilo la kiserikali hufanya kazi pamoja na serikali, na shirika la AGRA kusaidia vyama 122 vilivyo wanachama wapatao 21,500 katika mikoa mine nchini humo.

Nchi hiyo inafwata nyayo za nchi jirani ya Kenya, ambayo inajivunia kwa vyama vya mashirika vipatavyo 15,000 na wanachama zaidi ya milioni 12. Kenya inajulikana kwa kuwa na vyama kama hivyo vikubwa zaidi barani Afrika. Kulingana na takwimu za serikali, wanamashirika wamehifadhi zaidi ya shilingi bilioni 400, ambayo ni asili mia 35 ya hifadhi ya taifa nzima.

Kupitia RCA, ambayo hutambua vyama vya mashirika kuwa halali kisheria, wanamashirika nchini Rwanda, ambao kwa wingi ni wakulima wadogowadogo wanaweza kupata mikopo za benki, na pia wanaweza kuuza mazao yao kwa pamoja, asema Claver. Kuuza kwa pamoja husaidia wakulima hao kupata faida kubwa.

Mukasonga Mediatrice, mwanachama wa chama cha ushirika katika wilaya ya Nyagatare mashariki mwa nchi hiyo asema kwamba masharirika yamewasaidia kupambana na hali ya umasikini kwa sababu ya mafunzo ya kilimo bora. Shirika la Umoja Wa Mataifa kwa Chakula limenunua mahindi yaliyohifadhiwa na shirika la Ejo Heza mara mbili kwa sababu ya uwezo wa kununua kwa jumla.

Tangu kuundwa kwa RCA, zaidi ya vyama vya mashirika 4,000 na idadi ya wanachama zaidi ya milioni mbili vimesajiliwa, kulingana na Mugabo Damien, Mkurugenzi mkuu wa RCA.

Asema kuwa, mashirika ni chombo halisi ambacho wanachama wametumia kuunda nafasi za kazi, kuimarisha hali ya uzalishaji chakula nchini, na kujipatia mapato yao ya kila siku.

Jeanette Mukamapenzi, mwanachama wa chama cha ushirika cha Kwamusiru kutoka Nyagatare, asema kuwa mbeleni, familia yake iliwezewa kuvuna tani moja ya mahindi kutoka shamba lao la ekari moja. Lakini baada ya kujiunga na shirika, ambapo alifundishwa jinsi ya kutumia mbolea, kiwango cha mavuno kimeimarika mara nne.

Mediatrice asema kuwa kwa hivi sasa, anaweza kulipa karo ya mtoto wake katika chuo kikuu. Binti huyo asema kuwa kwa kuchanganya mbolea ya duka na ile ya kujitengenezea nyumbani, na pia kufwata mawaidha ya wataalam, mazao yake ya mahindi yameongezeka kutoka chini ya tani moja katika ekari moja hadi tani 4.5.

Ingawa nchi ya Rwanda ina matatizo yake, Claver wa RDO anaamini kuwa siku moja wataweza kukariri hadithi ya mashirika sawa na ndugu zake katika nchi jirani ya Kenya.

Isaiah Esipisu ni mwandishi wa kujitegemea maarufu kwa maswala ya kilimo na mazingira esipisus@yahoo.com

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->