×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Teknolojia ya gesi anuai yabadili mtazamo wa kijinsia Tanzania

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 2 July 2014 10:45 GMT

Aloycia Mndenye prepares cow dung before discharging it into a biogas digester, with Abdallah Musa, a researcher from Sokoine University of Agriculture, looking on. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Kizito Makoye

Image Caption and Rights Information

With families turning to biogas for household energy, men are getting involved, freeing women from collecting firewood

NJOMBE, Tanzania (Thomson Reuters Foundation) - Aloycia Mndenye amekuwa akijaribu kumshawishi mumewe kumsaidia kukusanya kuni—hata hivyo, jitihata zake ziligonga mwamba kwa kuwa  mumewe anaona kazi hiyo ni ya wanawake.

Hata hivyo, licha ya kuzongwa na majukumu mengi, Mndenye, mwenye umri wa miaka 32 na mkulima kijiji cha Lunyanywi, mkoa wa Njombe, Nyanda za juu kusini, alikuwa akitumia masaa mawili kila siku kukusanya kuni ili kukidhi mahitaji ya nishati nyumbani.

“ Ilikuwa inachosha sana kusema ukweli, nilikuwa natembea umbali mrefu sana kukusanya kuni. Ni baridi sana hapa wakati wa usiku, nyakati nyingine joto linashuka kiwango cha kuganda,” alisema.

Hata hivyo, tangu afunge mtambo wa gesi anuai unaotumia mbolea ya ng’ombe, miaka miwili iliyopita ikiwa ni sehemu ya mradi unaofadhiliwa na chuo kikuu cha sokoine (SUA), kumetokea mapinduzi makubwa sana ya kijinsia kuhusu matumizi ya nishati kwa familia.

Mumewe Mndenye, ambaye alikuwa akidharau kazi za nyumbani, sasa hivi anashiriki kuendeleza mtambo wa gesi anuai, na nyakati zingine hupika kwa gesi—akimwacha mkewe aendelee na majukumu mengine shambani.

“ Mtambo huu umerahisisha sana kazi, mume wangu na mimi tunajivunia sana mradi huu,” alisema. “Yuko makini sana kuhakikisha kwamba unaendeshwa vizuri ili kufidia gharama za kuujenga,” alisema

Licha ya harufu nzito ya mbolea inayooza, mzee Mndenye hufurahia sana kutifua mbolea ya ng’ombe na kuitumbukiza kwenye mtambo uliojengwa nje kidogo ya nyumba yao. Mchakato huo huhusisha kuchanganya maji na mbolea na kuondoa uchafu unaoweza kudhorotesha uzalishaji wa gesi.

“ Natumia nusu saa tu kufanya kazi hii. Ni rahisi sana na yenye heshima kuliko kukusanya kuni. Nachanganya maji kwenye ndoo mbili za mbolea kuzalisha gesi ya kutosha kwa matumizi ya kutwa alisema.

Mtambo huo unauwezo wa kuzalisha gesi ya kutosha kupikia na kuwasha taa za karabai, alisema, na mabaki ya mbolea hutumika kama mbolea kwenye shamba lake la maparachichi.

Matumizi ya gesi anuai Lunyanywi na vijiji vingine Njombe, watafiti wa SUA wanasema, umebadili mwelekeo wa familia nyingi, huku wanaume wakionekana kushiriki kikamilifu kulisha mbolea kwenye mtambo na hata kutumia gesi yenyewe na kurahisisa mzigo wa majukumu yanayowakabili wake zao—hasa kukusanya kuni. Pia inapunguza garama ya kununua nishati mbadala kama vile mafuta ya taa.

Watu wengi waishio vijijini Tanzania ambao hawana umeme, hutegemea kuni na mafuta ya taa kupikia na kuwashia. Kwa mujibu wa serikali, ongezeko kubwa la mahitaji ya kuni limeweka shinikizo kwenye matumizi ya misitu na kuathiri vyanzo vya maji.

“Kabla hatujaanzisha huu mradi, mume wangu alikuwa anatumia zaidi ya shilingi 2500 ($1.5) kila wiki kununua mafuta ya taa—hata hivyo, kwa sasa tunatumia rasilimali zetu wenyewe kupata nishati ya mwanga,” Mndenye alisema.

Shila Lehada, mratibu wa Tanzania Domestic Biogas Programme, mradi unaofadhiliwa na wahisani, amesema kuacha kutumia kuni na mafuta ya taa huwezesha familia zinazotumia gesi hifadhi hadi shilling 600000 ($375) kwa mwaka na kutoa fursa kwa wanawake na watoto kusoma na kufanya shughuli zingine za kuwaingizia kipato kwa familia.

Mndenye kwa mfano, amewekeza akiba yake kwa kuanzisha duka dogo analouza vitu kadhaa vya matumizi ya nyumbani. “Sitaki kupoteza pesa katika kununua nguo kama wanawake wengi wanavyofanya, nawekeza ili nipate kipato zaidi,” alisema.

Watoto wangu wanapata chai asubuhi kabla hawajaenda shuleni. Ni kiasi cha kuwasha tu jiko. Haikuwa rahisi hivyo wakati tukitumia kuni” alieleza.

Ndelilio Urio, profesa wa kilimo wa SUA, amesema mabaki yanayotoka kwenye biogesi yanatumika kama mbolea bora kuliko samadi kavu, kwa kuwa kiwango cha urea kwenye mabaki inaongeza idadi ya naitrojeni kwenye udongo.

Familia zimefundisha kutumia mabaki ya mbolea kwenye bustani zao nyumbani katika kuzalisha mboga na matunda alisema. Na kwa kuwa kuna manufaa ya kiuchumi wanaume wengi sasa wanavutiwa na kazi ya kulisha mtambo wa gesi anuai.

Urio alisema, vijiji Ilulike na Nyumbanitu haswa,  kilimo cha matunda ya maparachichi imekuwa yenye kuleta mapato yakuvutia sana.

Kwa mujibu wa wakulima, kiwango cha gesi kinachozalishwa hukidhi mahitaji ya familia –hata hivyo, baadhi ya watu huendelea kutumia kuni na umeme wa jua kuleta joto na kuwasha taa majumbani kwao, hasa wakati wa baridi. 

“Nataka kutumia gesi vizuri. Sitaki kuipoteza kuchemshia maji ya kuoga, ni bora nitumie kuni kuchemsha maji ya kunywa haina maana kwamba gesi haitoshi.”

Kizito Makoye ni mwandishi aliyepo Dar es Salaam, Tanzania. Anaripoti kuhusu mabadiliko ya tabia nchi na maswala ya utawala.

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->