×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Uhifadhi nyasi wasaidia Kenya kame kupunguza hasara ya mifugo

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 7 January 2015 10:34 GMT

An old technology is making inroads as a form of climate change adaptation in Northern Kenya

ALAGO ALBA, Kenya, Jan 7 (Thomson Reuters Foundation) - Kwa kawaida, wakati kama huu wa mwaka, Ibrahim Hassan angekuwa akiandaa mifugo yake kwa safari ndefu kutafuta malisho bora huko kando ya mto Tana, kilomita mia moja kutoka kijiji chake huko Dertu, kaskazini mwa Kenya.

Kama wengi hapa, Hassan ajua kwamba mifugo yake itakufa kama hataihamisha kabla kufurukuta kwa msimu wa ukame, ambao huingia kati ya miezi ya Januari na Machi.

Lakini mwaka huu, mzee huyu wa umri wa miaka hamsini na nane ameamua hatahama. Sababu yake ni nyasi iliyokusanywa na kuwekwa kwa kibanda huko nyumbani mwake Alago Alba.

“Wakati wa mvua kuna lishe tosha, mimi hukusanya kiasi kikubwa cha nyasi na kuhifadhi ili kujiandaa kwa msimu wa ukame,” alieleza baba huyu wa watoto sita. “Hii uniokoa kufunga safari ndefu ya hatari kutafuta malisho.”

Teknolojia hii ya zamani - ya kukata na kuhifadhi nyasi - inapokelewa kama aina ya kinga dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa kaskazini mwa Kenya, ambapo kuna ongezeko la ukame na majaribio ya uhamiaji ili kutafuta lishe, na wakati mwingine imesababisha migogoro juu ya uhaba wa maji na nyasi. 

Matatizo yanayokabili jamii wanaomiliki mifugo kaskazini mwa Kenya ni wazi kutokana na kifaa cha kutabiri hali ya hewa huko kituo cha Dertu Millenium Village, ambacho huonyesha kwamba mvua yaweza kuwa nadra kwa siku nyingi wakati wa kiangazi.

Kifaa hiki ambacho chatumia nishati ya jua kinaonyesha kwamba upepo unaweza kuwa zaidi ya kilomita arobaini kwa saa, huku joto ya mchana ikiwa juu zaidi.

Kifaa hiki husaidia kama “onyo ya mapema dhidi ya ukame”, alieleza meneja wa kituo, Samuel Mbalu. Bila msaada kama huu, “wafugaji hupoteza mifugo yao kutokana na ukame huku familia zikikimbia makwao ili kutafuta chakula na maji”, alisema.   

Dertu Millenium Village ni moja ya jaribio ya jamii kukomesha umaskini uliokithiri kwa njia ya maendeleo endelevu. Zilianzishwa na mashirika ikiwa ni pamoja na Earth Institute huko Columbia University na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa, UNDP.

Kwa muongo ambao yeye amefanya kazi Dertu, Mbalu amejaribu kushawishi jamii katika eneo hili kupunguza mifugo wakati msimu wa kiangazi unakaribia. Lakini wachache hufanya hivyo.

“Wafugaji huamini kwamba kupunguza mifugo ni kuwapokonya lishe na heshima katika jamii,” Mbalu alisema. “Wao hushikilia kuwa afadhali mifugo yao kufa badala ya kuuza.”

Hata hivyo, wachache kama Hassan, wamekubali mawaidha ya Mbalu, ikiwa ni pamoja na kuhifadhi nyasi ili wanyama wapate lishe wakati wa ukavu.

FAIDA ZA UHIFADHI NYASI

Kuokoa wanyama wakati wa vipindi vya ukame kunapunguza madhara katika jamii. Katika shule ya msingi ya bweni ya Dertu, madarasa yamejaa watoto masomoni - hii ni kinyume na hapo awali ambapo wavulana wangekuwa nyumbani wakisaidia familia zao kujiandaa kuhama ili watafute malisho, alisema Sofia Ali, mwalimu mkuu wa shule hiyo.

Wasichana, alisema, wangekuwa wameozwa wakati huu ili kupunguza mzigo wa familia wa kukabiliana na ukame.

Mmoja wa hawa angekuwa Halima Hassan, mwenye umri wa miaka kumi na tatu, ambaye angekuwa darasa la nne. Yeye ni bintiye Ibrahim Hassan.

“Nilipata jaribio la kumuoza lakini nina furaha sikufanya hivyo. Yeye anapata elimu kwa sababu ya maisha yasiyo ya kuhama,” alisema baba Halima, huku akigawa konzi za nyasi kwa ng’ombe wake wenye afya huko nyumbani kwake.

Mabadiliko mengine pia yanaendelea. Nunow Rage, mwenye umri wa miaka thelathini na tano, alisema uamuzi wa mumewe wa kupunguza ng’ombe wake na kuhifadhi nyasi umemsaidia kuwekeza kwa biashara ya nguo huko soko la Dertu.

“Mume wangu anapouza mifugo, yeye hunipa sehemu ya fedha ili niendeleze biashara,” alisema mama huyu wa watoto wanne. “Wakati ukame umechacha sana mimi hutumia akiba kununulia familia yangu chakula.”

Nunow alisema maisha yasiyo ya kuhama yamesaidia kupunguza vifo vya watoto wachanga katika eneo hilo, kwa sababu yeye na mama wengine wanaweza kuwapeleka watoto wao kuhudumiwa katika Dertu Health Center, wanapokabiliwa na matatizo.

Sio tu kaskazini mwa Kenya ambapo uhifadhi wa nyasi unapata wafuasi. Katika mradi wa mchele wa Mwea huko kati ya Kenya, vikundi vya vijana wanakusanya majani kavu ya mchele na kuyauza kama lishe la mifugo, alisema David Bundi, mwenyekiti wa kikundi kinachojulikana kama Kiratina Hay Product.

Mzigo moja wa nyasi hii ya uzito wa kilo kumi na nne waweza kuuzwa dola saba za marekani, ama shilling mia saba za Kenya, na baadhi ya nyasi hii imesafirishwa hadi kaskazini mwa Kenya ili kulisha mifugo inayokufa na ukame, alisema.

Yeye ana matumaini kwamba serikali itasaidia ubunifu kama huu, ili kutoa ajira kwa vijana na kusaidia nchi kukabiliana na ukame.

“Tungependa serikali kutupatia zabuni ya ugavi nyasi kwa mikoa kame na pia taasisi za umma ambazo huweka mifugo.”

(Taarifa na Kagondu Njagi; uhariri na Laurie Goering)

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->