×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

MAKALA-Simu za kisasa zasaidia wanawake wa Tanzania kulinda haki zao za ardhi

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 25 August 2015 09:12 GMT

Jacqueline Nyantalima, a resident of Ilalasimba village, is one of a group of young people running a new land mapping process. TRF/Kizito Makoye

Image Caption and Rights Information

Young villagers are using mobile technology to map land, enabling widows and others to get property ownership

Na Kizito Makoye

ILALASIMBA,Tanzania, Aug 25(Thomson Reuters Foundation) - Yolanda Ngunda ana kila sababu ya kutabasamu kwa kuwa amepata hati yake ya kumiliki ardhi iliyokuwa ikigombaniwa nyanda za juu kusini nchini Tanzania.

Kwa karibu muongo mmoja sasa, mjane huyo mwenye umri wa miaka 51, anayeishi kijijini Ilalasimba wilaya ya Iringa vijijini, alikabiliwa na mzozo mkubwa wa familia kwa kuwa shemeji zake walijaribu kumnyang’anya ardhi na kumfukuza kwenye nyumba yake ya matofali aliyojenga na marehemu mumewe aliyekufa kwa ugonjwa mfupi.

 “Nimekuwa nikiishi kwa hofu kwa miaka yote hiyo kwa kuwa sikuwa na nyaraka zozote zinazothibitisha kuwa mimi ndiye mmiliki halali.Sasa nimeshinda vita,” aliiambia Thomson Reuters Foundation, huku akionyesha cheti chake kilichochapishwa kwenye karatasi ya kijani.

Ngunda, mwenye watoto wanne ni miongoni wa mamia ya wanakijiji wa Ilalasimba waliopewa hati zao za kumiliki ardhi ikiwa sehemu ya mradi wa majaribi uliofadhiliwa na shirika na maendeleo la marekani USAID.

Ngunda alisema shemeji zake walimtishia kuchoma nyumba yake. “ Nilisimama kidete kutetea mali ya watoto wangu,” alisema kwa furaha.

Iringa ni moja ya maeneo mengi  nchini Tanzania yanayokabiliwa na kesi nyingi za unyakuaji ardhi zinazowahusisha wajane , wanaharakati wamesema.

Kuongejeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi kwenye mji huo yamefanya wajane wengi wawe kwenye hatari ya kuporwa adhi zao  na baadhi ya wanandugu wanaojua kidogo kuhusi ugonjwa huyo na wanaowatuhumu kwa kuwaua waume zao ili warithi mali

Sheria za ardhi za Tanzania zinatoa haki sawa kwa wanawake  na wanaume kupata, kumiliki na kusimamia ardhi na kuwaruhusu kushiriki kwenye vyombo vya ngazi za maamuzi kwenye mambo ya ardhi.Hata hivyo ni asilimia 20 tu ya wanawake wanamiliki ardhi kwa majina yao wenyewe kwa mujibu wa USAID

Mila na desturi kandamizi zimefanya kuwa vigumu kwa wanawake kupata ardhi. Badala yake wengi humiliki ardhi kupitia wenza wao au ndugu wa kiumi, ikiwa na maana hatimaye huishia kupeteza haki zao waume wao wanapokufa

Katika jituhada za kusaidia mamlaka za Tanzania kupima ardhi ya kijiji, USAID imezindua  mradi kupima taarifa ya kijiografia na za kidemografia  kwa kutumia  teknolojia ya simu za mkononi, ikiwa na lengo la kuharakisha utambuzi wa haki za ardhi.

 

Mradi huyo unaojulikana kama Mobile Application to Secure Tenure(MAST) unawezesha wanakijiji tutambua mipaka ya maeneo yao na kukusanya taarifa zinazohitajika na mamlaka husika  ili wapatiwe nyaraka za umiliki

WAPIMAJI WENYE UJUZI WA TEHAMA

Mradi huo ulioanzishwa mwaka 2014, na kugharimu $1 milioni, unatekelezwa na shirika la marekani la Cloudburst, umerahisisha mchakato wa uwekaji kumbukumbu za ardhi  na kufanya mchakato kuwa wa wazi na wenye ufanisi, USAID officials said.

Uandikishaji wa miliki ya ardhi ni mgumu sana nchini Tanzania, umeghubikwa na rushwa na utawala mbovu, ndiyo maana watu wengi mijini na vijijini hawana miliki ya ardhi , kwa mujibu wa utafiti wa shirika la Transparency International wa 2013

Karol Boudreaux, mtaalamu wa maswala ya haki ardhi wa Cloudburst Group, amesema mradi wa MAST umeandaliwa kuwa shirikishi ili kuongeza ufahamu kwa wanawake juu ya maswala ya kumiliki na kurithi ardhi wakati huo ikiwajengea wanavijiji uwezo wa kutatua migogoro

“Tumetambua kwamba haki ardhi hazijaeleweka vema  kwenye baadhi ya maeneo,”Boudreaux aliiambia Thomson Reuters Foundation, akiongeza wajane wanakabiliwa na shinikizo kumiliki na kurithi ardhi.

Ameongeza mradi huo ulitoa mafunzo kwa kundi dogo la vijana namna ya kutumia simu za kisasa za Android ili kuandikisha haki za ardhi.

“ Tulitaka kufanya kazi na watu waliosoma na wanaopenda kutumia simu za kisasa za mkononi kupima na kuhifadhi kumbukumbu za ardhi” Boudreaux alisema.

Kuepuka migogoro,wapimaji wenye ujuzi wa teknolojia ya kisasa ni lazima wahakikishe kwamba wamiliki wa ardhi husika au wawakilishi wao wanakuwepo wakati wa mchakato wa upimaji. Taarifa zao pia kupakiwa kwenye tovuti maalumu ambapo maofisa ardhi wanaweza kuifikia  na kuthibitisha taarifa na hatimaye kutoa hati za ardhi.

“Nimefurahi sana kupata fursa ya kujifunza namna ya kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi,” alisema Jacquiline Nyantalima mwenye umri wa miaka 23. “ Hili ni zoezi muhimu sana kwa kuwa linasaidia wanawake kulinda haki zao za kumiliki ardhi”

Kwa mujibu wa USAID, vijana hao, waaofanya kazi kwa kushirikiana na viongozi wa vijiji, wameorodhesha miliki za ardhi na kusaidia utolewaji wa hati miliki kwa wakazi 940. Upo mpango wa kupanua mradi huo kwenye vijiji wiwili Zaidi hivi karibuni.

KUJENGA KUJIAMINI

Wanawake kutoka Ilalasimba kwa sasa wana usalama mkubwa kwa mali zao, kwa kuwa asilimia 30 ya ardhi imepimwa na kuandikishwa ka majina yao, maofisa wa USAID wamesema. Asilimia 40 nyingine imeandikishwa  kwa wanandoa na nyingine 30 imeandikishwa kwa wanaume pekee.

“ Nilikuwa mnyonge , ila kwa sasa nina furaha sana baada ya kupata cheti change,”alisema Ngunda. “Najua maisha ya baadae ya watoto wangu yatakuwa mazuri kwa kuwa hamna atakayewadhulumu ardhi yao.

Migogoro hatari ya ardhi  imekuwa ikinguruma kwa miongo nchini Tanzania huku wakulima na wafugaji wakisukumana kugombea maji yanayopungua kutokana na ukame wa mara kwa mara na utunzaji hafifu.

Adam Nyaruhuma, mratibu wa programu ya sapoti ya rasilimali ardhi katika Wizara ya Ardhi amesema upimaji miliki za ardhi kwa kutumia teknolojia ya kisasa una nafasi ya kuepuka migogoro ya mara kwa mara huku ikipanua wigo  kwa watu wa vijijini kurumia ardhi yao kwa manufaa yapana Zaidi.

“Faida ya mradi huu ni kwamba ardhi inapokuwa imerasimishwa, inafungua fursa nyingi mno kwa  wanavijiji husika wanaoweza kuitumia hati zao za ardhi kama dhamana kupata mikopo benki”,Nyaruhuma alisema.

( Mwandishi;Kizito Makoye;mhariri Megan Rowling. Tafadhali tambua  Thomson Reuters Foundation, tawi la ukarimu la Thomson Reuters, inayoandika habari ya uhanga wa binadamu, haki za wanawake, biashara ya binadamu, Rushwa na climate change.)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->