×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Adui anayewaua mbuzi ageuka kuwa nishati safi vijijini Kenya

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 16 September 2015 08:35 GMT

Turkana women sit with their goats in Loyoro village of Turkana district in North-western Kenya, October 1, 2009. REUTERS/Thomas Mukoya

Image Caption and Rights Information

The toxic bane of the Rift Valley is now being harvested to produce renewable energy

MARIGAT, Kenya, Septemba 16 (Thomson Reuters Foundation) – Mmea sumu uliokuwa unaua mbuzi huko bonde la ufa una jukumu mpya: unatengeneza nishati safi zinazotumiwa manyumbani na kuwapa wanakijiji hela ya hadi dola elfu moja kwa mwaka.

Jane Chirchir ni mmoja wao ambaye kageuza mmea huu unaoitwa kwa kimombo, Prosopis juliflora, kutoa nishati. Mmea huu ambao unaweza kurefuka hadi mita kumi na mbili, ulikuwa ukienea mno katika maeneo haya na kusababisha upungufu wa ardhi ya malisho ya mifugo, huku ikiwaua.

Sasa mathenge, kama inavyojulikana kwa lugha ya kienyeji, inavunwa na kuuzwa kwa kituo cha umeme ambacho kwa mara ya kwanza kimeleta nishati kwa baadhi ya manyumba na kupunguza malipo ya nguvu za umeme kijijini.

“Kampuni hununua malighafi kwetu,” alisema Chirchir mweye furaha. “Hii imesaidia familia yangu kujikinga na hasara tulizopata wakati mbuzi zetu zilikufa baada ya kula mathenge.” Alisema alipoteza wanyama kumi na tano.

Mmea huu umesaidia wanakijiji, ambao miaka mitano iliyopita walikabiliwa na shinikizo za kiuchumi baada ya mahakama kukataa mashtaka yaliyokuwa yakiuliza serikali ifyeke mmea huu na kutolea wafugaji fidia kwa hasara walizopata.

Idadi kubwa ya wakaazi ambao wamefika mia tano na sitini elfu huko kata ya Baringo, na ambayo ina ukubwa wa kilomita elfu kumi na moja za mraba, ni wafugaji.

Mmea huu uliletwa maeneo haya miaka ishirini na tano iliyopita na serikali ya Kenya ikishirikiana na kituo cha umoja wa mataifa, FAO, ili kuzuia upepo, mmomonyoko wa udongo na jangwa kuenea.

Lakini ulileta matokeo yasiyotarajiwa. Wazee wa kijiji walisema mbuzi walipokula maganda ya mathenge, mbegu zilikwama kwa ufizi wa wanyama na kuwapea sumu.

Wengine walidai kwamba mizizi ya mmea huu ilitambaa kwa misingi ya nyumba zao na hatimaye kuziharibu.

Hata hivyo, kuenea kwa kasi kwa mmea huu kunaleta hela nyumbani mwa Chirchir na wengine wengi, wanakijiji wanapouvuna huu mmea na kuuza kama majani ya mafuta kwa kampuni moja ya uzalishaji wa umeme huko Marigat.

NISHATI NA MAPATO

Kampuni inayojiita Cummins Cogeneration Kenya Ltd, ikishirikiana na serikali kujenga mtambo katika ekari kumi na tano za ardhi kijijini. Kituo hiki ambacho hutumia mathenge kutengeneza nishati, huuchoma mmea huu na kuubadilisha kuwa umeme.

Maafisa wa kampuni wasema kwamba, zaidi ya familia elfu mbili kijijini mwa Chirchir wamesajiliwa kwa ugavi wa mathenge, lakini wengine zaidi watashirikishwa. Kampuni inatarajia kuwalipa wanajamii dola milioni nne kwa mwaka.

Kampuni huwalipa shilingi mbili za Kenya kwa kilo ya mathenge na inalenga kila muuzaji wa mathenge kupokea dola elfu moja kwa mwaka.

Mradi huu unalenga kuzalisha megawati kumi na mbili za umeme kila mwaka kwa miaka ishirini ijayo, maafisa walisema.

Kampuni hii inawekeza karibu dola ishirini na mbili elfu kwa mtambo huu wa mathenge katika kanda, ikiwa ni pamoja na kanda ya pwani, Kenya, na Sudan Kusini. Maafisa walisema wanalenga kuzalisha asilimia sitini za umeme kutoka kwa mmea huu sumu.

Katika kata ya Baringo, ambapo utapata Marigat, nishati hii itasambazwa kupitia usimamizi wa serikali mtaa.

“Kampuni hii imeshirikiana na sisi na imekubali kutoa baadhi ya nishati kwa jamii kupitia mpango wa kata,” alisema kamishina wa kata ya Baringo, Benard Leparamarai. “Sisi tumesaidia na rasilimali kama ardhi, malighafi na ukarimu wa kisiasa.”

Kampuni inatarajia kuzalisha nishati ya thamani ya dola milioni nane kwa mwaka. Taka inayobaki baada ya mathenge kuchomwa itatengeneza makaa ya kuuza, maafisa walisema.

Si familia tu zinasherekea. Madaktari katika kata ya Baringo wanatumaini mradi huu utapunguza uhaba wa nguvu za umeme katika vituo vya afya.

Kutokana na uhaba wa mitandao ya umeme vijijini, kiliniki na mahospitali hukaa kwa wiki bila umeme, alisema Robat Rono, daktari katika kituo cha Marigat. Vituo vilivyo mbali na mjini hutumia nguvu za jenereta, aliongeza.

“Mradi huu utageuza uchumi wa mkoa huu,” alisema. “Sisi tunapanga kuongeza vitanda vya wagonjwa hospitalini kama chanzo hiki cha nishati kitakuwa cha kuaminika.”

(Taarifa na Kagondu Njagi; uhariri na Laurie Goering; James Baer. Tafadhali tembelea Thomson Reuters Foundation, mkono hisani wa Thomson Reuters, unaoripoti shughuli za misaada, mabadiliko ya hali ya hewa, haki za wanawake na biashara rushwa. www.trust.org/climate.)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->