Vijana wa Kenya waacha uhalifu ili kulinda misitu

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 3 November 2015 11:11 GMT

Bicycles are parked under a tree at Muusini primary school, where newly planted trees stand in the background in Kibwezi, east of Kenya's capital, Nairobi June 20, 2014. REUTERS/Noor Khamis

Image Caption and Rights Information
Former drug dealers and thieves alert local chiefs to illegal logging and sell seedlings for reforestation

THARAKA NITHI, Kenya, Novemba 3 (Thomson Reuters Foundation) – Vikundi vya vijana waliorekebisha mitindo ya kuuza mihadarati na wizi kutoka kwa majirani sasa wanasaidia kulinda miti vijijini mwa Kenya kutoka wanaharamu.

Vijana hawa, ambao walikuwa chanzo cha mvutano katika jamii, sasa huripoti tuhuma za magogoro kwa mamlaka ya vijiji. Pia wanachangia katika jitihada za kuongeza misitu nchini Kenya kutoka asilimia saba hadi asilimia kumi ifikapo mwaka wa elfu mbili na thelathini.

Imekuwa kinyume cha sheria kukata miti katika misitu ya Kenya tangu mwaka wa elfu moja mia tisa na tisa, lakini katiba mpya ya mwaka wa elfu mbili na kumi ilielekeza marufuku mashambani isipokua mtu awe na kibali rasmi.

Murithi Ntaru, mwanachama wa kikundi cha mageuzi kwa vijana cha Muiru, ambacho kiko kijijini kavu huko Weru, kata ya Tharaka Nithi, anapendelea wito huu zaidi ya maisha yake ya baadaye ambapo alijishughulisha na madawa ya kulevya.

“Hii ni bora zaidi kuliko wakati nilikuwa najificha kutoka kwa sheria kwa masiku kama muuzaji wa madawa ya kulevya,” alisema Ntaru mwenye umri wa miaka thelathini na nne, ambaye rafikiye ako jela kwa kuhusika na mihadarati.

‘Mimi sasa hutumia ujuzi nilioupata nilipokuwa nikifanya mambo mabaya kuwanasa majangili wa mbao.”

Yeye na vijana wengine walijiunga na uhalifu baada ya marufuku ya ukataji wa misitu ya umma kusimamisha biashara ya usafirishaji wa magogo, ambayo wengi wao waliacha shule ili kujiunga nayo.

Sasa ujuzi waliopata kutoka biashara ya mbao inawekwa kwa matumizi mazuri.

Wanakikundi wamechagua mlio maalum wa simu za mkononi kutoa taarifa wakati onyo la shughuli za ukataji miti zinapowafikia.

“Jumuiya hutueleza wakati wanawakala wa mbao wanapoonekana kijijini au wakati jirani ana mpango wa kukutana na wanawakala. Tunapotoa taarifa, Chifu hutuma maskauti kufuatilia mienendo ya wanawakala,” alisema Ntaru. “Nasikia niko salama kwa sababu mimi tu hutuma ujumbe wa simu kwa Chifu.”

Baada ya kutoa habari kuhusu ujangili wa magogo, kikundi huonyeshwa mahali ya kuuza miche katika maeneo mapya ya upandaji wa miti.

Kwa miaka mitatu iliyopita, vijana wa Muiru wamekuwa na kitalu cha miti karibu na mto Naka kupitia usaidizi wa kata, ambayo ilitambua fursa hii kama ya kulinda miti na kuondoa vijana kutoka mihadarati.

Kundi la Muiru ni mojawapo ya idadi zinazoongezeka ambazo hulima miche ili kuendeleza upandaji wa miti katika eneo hilo.

WANAHALAMU

Kwa siku nzuri, kundi la Ntaru linaweza kutoa miche ya thamani ya hadi shilingi elfu ishirini za Kenya, ama dola mia mbili, na kugawana faida miongoni mwa wanachama wenzake kumi.

Ushujaa wao unampendeza Doreen Cianjoka, mjane huko Weru ambaye alipoteza miti ya shamba lake kwa wanaharamu.

Wageni waliovaa vizuri walimtembelea nyumbani mwake na kumhakikishia kwamba angepata soko nzuri kwa miti yake, alisema.

Baada ya siku chache, mawakala walirudi na timu iliyobeba mashini za kupasua mbao na kukata miti yote, lakini hakupokea malipo yoyote.

“Niliwaona mwisho walipokuwa wanasema kwaheri kutoka kwa lori lililokuja kubeba miti yangu,” alikumbuka. “Mimi natumaini vijana wetu na Chifu watanisaidia kufuwatilia watu hawa wabaya siku moja.”

Kama matumaini yake yatatimizwa au la, wakaazi wengine hawana furaha kuhusu sheria inayopinga upasuaji wa magogo, ambayo wanalaumu kwa uhaba wa mbao.

INATISIHA BIASHARA

Katika duka la samani la Jasho huko Chuka, mji uliopo kata ya Tharaka Nithi, mmiliki Justin Wanyanya anabishana kwa ukali na mmoja wa wafanyikazi wake. Wanyanya, kama mafundi wengine wa mbao na wauzaji, wamekuwa wakipunguza baadhi ya wafanyikazi wake.

“Siwezi kuwalipa kwa sababu biashara ni mbaya sana kutokana na uhaba wa mbao,” alisema.

Ushujaa wa vijana unaweza kuwa moja ya sababu biashara ni mbaya kutokana na uhaba wa mbao. Lakini sio hii tu.

Maendeleo ya manyumba inanawiri mijini kama Chuka, na licha ya udhibiti juu ya ukataji wa miti, malori yaliojaa mbao huonekana mara nyingi yakielekea kaskazini mwa Kenya.

Mugambi Ngece, ofisa katika kituo cha utafiti wa mazingira, Kenya, alibainisha mahitaji makubwa ya mbao katika miji kama Isiolo pamoja na mradi wa muundombinu wa LAPPSET.

Hii imesababisha ushindani wa mbao na biashara ndogo kama ya Wanyanya. Lakini Ngece alisema mazingira yananufaika.

Katiba mpya inaunga ushiriki wa wananchi katika usimamizi na uhifadhi wa mazingira.

Chifu wa kijiji Kinyua Karagwa, alisema shughuli za vijana wa kundi la Muiru, “linafanya miti yetu kukaa muda mrefu.”

Katika miaka hamsini na nne alioishi Weru, Karagwa ameona mazingira ya mlima Kenya yakidhoofika, hasa kufuatia kuenea kwa magogo katika miaka ya elfu moja mia tisa na themanini.

Hii ilisababisha serikali kupiga marufuku watu kuingia kwa misitu bila ruhusa kutoka kwa ofisi ya misitu katika miaka ya elfu moja mia tisa na tisa.

Wanabiashara wa mbao, ambao walikuwa wametengeneza faida kubwa walipata njia mbadala katika mashamba ya vijiji kama ya Cianjoka, hadi udhibiti mkali wa ukataji miti ulipopitishwa mwaka wa elfu mbili na kumi.

Stephen Gitonga, ambaye alipata lishe kama mpasuaji wa mbao alisema kazi yake mpia ya kuendesha teksi ya pikipiki haimpei hela nyingi kama kitambo.

“Sheria si haki, kwa sababu biashara kubwa za mbao bado zinanufaika wakati zinatoa ugavi kwa ajili ya ujenzi,” alisema.

(Taarifa na Kagondu Njagi; uhariri na James Baer na Megan Rowling. Tafadhali tembelea Thomson Reuters Foundation, mkono hisani wa Thomson Reuters, unaoripoti shughuli za misaada, mabadiliko ya hali ya hewa, haki za wanawake na biashara rushwa. www.trust.org/climate.)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.