×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Ili kuokoa misitu asilia, wakulima wajaribu zao jipya: vipepeo

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 30 December 2015 12:10 GMT

Mwamvua Ali, a butterfly farmer in Pete village in Zanzibar’s Unguja island, puts out ripe mangoes in a netted cage to attract butterflies. TRF/Zuberi Mussa

Image Caption and Rights Information

Switch to fast-growing "crop" is helping curb deforestation for charcoal in Zanzibar, backers say

PETE, Tanzania Dec 30 (Thomson Reuters Foundation) — Vipepeo wenye rangi za kuvutia warukao kwenye msitu wa Jozani kisiwani Zanzibar ni wazuri sana kuwatazama, lakini kwa wakulima na wachoma mkaa kisiwani humo, ni zaidi ya kivutio; ni pesa.

Ikiwa ni jitihada za kulinda msitu unaotoweka kisiwani humo, wenyeji wanafunzwa namna ya kufuga vipepeo, chini ya mradi unao jaribu kukinga janga la uharibifu misitu kwa kuwapa watu kipato mbadala ili waache msitu istawi.

Msitu wa jozani iliopo kati ya rasi iliyosheheni mikoko ya Chwaka na Uzi Kisiwani Unguja, ni msitu mkubwa unaohifadhi viumbe kadhaa vilivyo hatarini kutoweka, ikiwa ni pamoja na Nyani wekundu wajulikanao kama Colobus.

Hata hivyo, pamoja na uzuri wake, msitu huo uko hatarini kutokana na kasi kubwa ya ukataji miti kwa ajili ya kuchoma mkaa na kilimo kisicho endelevu.

Chini ya mradi huo wa kijamii, kituo cha vipepeo cha Zanzibar kinakusudia kubadilisha hali ya mambo kwa kutoa mafunzo kwa wachoma mkaa katika vijiji vinavyo uzunguka msitu wawe wakulima wa vipepeo.

“Hatuna mamlaka ya kumzuia yoyote asichome mkaa. Hata hivyo, tunajaribu kutoa elimu ili watu waelewe madhara ya uchomaji mkaa kwa mazingira,” alisema Natalie Tempel-Merzougui, kiongozi wa mradi huo.

 

PESA KUTOKANA NA LESO INAYORUKA

Mpango huo unatoa mafunzo mahususi na vifaa kwa wafugaji wa vipepeo, na waliofanikiwa sana wanaweza kupata mpaka hata dola 250 kwa mwezi kutokana na mauzo ya vipepeo kwenye kituo hicho ambacho kinafanya utalii na pia kwa wanunuzi wa nje ya nchi, alisema.

Wakulima wa vipepeo wanafanya kazi kwa kukamata vipepeo jike kadhaa na kuviweka kwenye uzio wa wavu ili watage mayai. Baada ya hapo wakulima huokota mayai ili wakuze katapila kwa kuyalisha kwenye mimea mpaka yanabadilika kuwa pupa.

Ni katika hatua hii kwamba wakulima wanaanza kuvuna kipato kwa kuuza mapupa kwenye kituo cha ufugaji, ambacho pia huyauza kwa wanunuzi wa nje na kubakisha baadhi kwa ajili ya kuonyesha watalii.

Kikiwa kimeanzishwa mwaka 2008, kituo hicho cha vipepeo, kilichopo karibu na mbuga ya wanyama ya ghuba Jozani Chawka kisiwani Unguja, ni miongoni mwa vituo vikubwa vya maonyesho ya vipepeo barani Africa vinavyotunza zaidi ya aina hamsini ya vipepeo asilia, ikiwemo aina ya ‘Leso ipaayo’ na nyeusi na nyeupe swalowtail.

Kituo hicho kinachofanya kazi kwa karibu na Chama cha watunzaji mazingira cha Jozani, ni kivutio kikubwa cha watalii wanaopenda kuona na kujifunza kuhusu aina ya vipepeo.

“Lengo kuu ni kuleta ufahamu juu ya umuhimu wa kulinda mazingira na pia kutoa fursa kwa wakaazi kupata kipato,” Merzoughui alisema.

Rungu Hamisi, mmoja wa wafugaji wa vipepeo ambaye alizoea kupata kipato kutokana na kuchoma mkaa amesema kukuza vipepeo kumeongeza kipato chake kwa hali ya juu.

“Ufugaji wa vipepeo ni rahisi sana ukilinganisha na uchomaji mkaa, unaohitaji kazi sana. Napata kipato tosha kuendesha maisha ya familia yangu,” alisema.

Alisema moja ya faida ya kulima vipepeo, kuliko mazao mengine, ni kwamba zinakomaa kwa haraka.

“Pindi mayai yakisha kobolewa na kuwa katapila, inachukua wiki chache tu kuwa vipepeo kamili tayari kwa kuuzwa,” alisema.

Kwa mujibu wa maofisa wa kituo hicho cha vipepeo, mradi huo pia umetoa fursa kwa wanawake kwa kuwa kukuza vipepeo ni kazi inayoingiliana na kazi za nyumbani.

“Napata pesa za kutosha kulisha familia yangu bila hata ya kuharibu msitu,” alisema Mwamvua Ali, 49, anayedai anapenda kufuga aina ya “Leso inayoruka” kwa kua hutaga mayai mengi.

 

BAKSHISHI KWA KUTUNZA MAZINGIRA

Huku aina nyingi ya kilimo kinahitaji ukataji wa miti, unaoweza kusababisha athari za mabadiliko ya tabia nchi na upotevu wa wanyama asili, kilimo cha vipepeo kinahitaji msitu iliofungamana unaotoa bakshishi ya kiuchumi kuulinda, Merzoughui alisema.

Alfred George, meneja msaidizi wa kituo hicho alisema kwamba kupitia mradi huo wakulima wengi kijijini Pete wametambua umuhimu wa kutunza mazingira na wengi wao wananufaika kutokana na kukuza vipepeo.

“Miti mingi sana inakatwa holela ili kutoa kuni za kuchomea mkaa kwa matumizi mbalimbali ya kupikia kwa wana jamii,” George aliiambia Thomson Reuters Foundation.

Hata hivyo, “wakulima wengi tuliowafunza kulima vipepeo hawakati tena mkaa,” alisema.

Safina Omar aliyeanza kuzalisha mkaa baada ya serikali kumzuia kulima mazao karibu na msitu wa Jozani alisema kilimo cha vipepeo kimempa kipato mbadala.

“Nilijua biashara ya mkaa ni mbaya kwa mazingira lakini nililazimika kuifanya kwa kuwa sikufikiria jambo lolote lingine la kuniingizia kipato, wakati huo huo nilikuwa na watoto wengi wa kuwahudumia’ alisema

Ingawa mradi huo si suluhisho la uharibifu wa misitu, umesaidia sana kukuza uelewaji na kuleta hali ya umiliki wa msitu miongoni mwa wakulima, George alisema.

Mradi mwingine kama huo unaendeshwa na wakulima 250 kwenye milima ya usambara , eneo linalojulikana kwa bio-anuai lakini ambapo misitu huharibiwa sana kwa ajili ya kuzalisha mkaa na kulima mazao.

Kwa mujibu wa Kituo cha vipepeo Zanzibar, kiwango cha pesa kila mkulima anapata kinategemea ameleta vipepeo wangapi na ni wa aina gani.

“Tunalipa zaidi kwa aina ambayo ni adimu na ngumu kufuga. Baadhi ya wakulima wetu wakubwa wanapata mpaka shilingi 5,00000 za kitanzania ($250) kwa mwezi,” Merzougui alisema.

Mkaa na kuni ni zaidi ya asilimia 90 ya nishati inayotumika majumbani nchini Tanzania, kwa mujibu wa Benki ya Dunia.

Serikali inakisia kati ya ekari 130,000 na 500,000 za misitu zinaharibiwa kila mwaka kutokana na uzalishaji wa makaa, kilimo duni na ufugaji wa ng’ombe holela.

(Imeandikwa na Kizito Makoye; imehaririwa na Laurie Goering; Tafadhali nukuu Thomson Reuters Foundation, tawi la hisani la Thomson Reuters, shirika la habari linalojihusisha na habari za majanga, mabadiliko ya tabia nchi, haki za wanawake, biashara ya binadamu na rushwa.Tembelea www. Trust.org/climate)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->