×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Wanawake wajasiliamali wachangia kuongezeka kwa biashara ya umeme jua Afrika Mashariki

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 6 December 2016 11:07 GMT

With solar power and access to loans, "we are more productive than ever before. On average we can get $25 a day, even more," says one woman

SHINYANGA, Tanzania (Thomson Reuters Foundation) - Huku giza likitanda kwenye uwanda wa kijiji cha Bunambiyu kaskazini mwa mkoa wa Shinyanga, Elizabeth Julius anawasha taa yake ya nguvu ya jua kumalizia kushona nguo za wateja wake.

Si muda mrefu, usiku ungemfanya asitishe kazi yake ya ushonaji na kufunga duka—au kulazimika kutumia taa ya mafuta. Hata hivyo, kwa kuwa ana taa ya umeme jua, Julius anaweza kushona kwa muda mrefu usiku kadiri anavyopenda.

“Nguvu ya jua imebadili kabisa maisha yangu. Naitumia kazini na nyumbani, na hainigharimu chochote,” alisema mjasiriamali huyo mwenye umri wa miaka 29 na mama wa watoto wawili.

“Mara nyingi naamka usiku kufanya kazi kwa kuwa nahitaji pesa kuendeleza familia yangu,” alisema.

Julius na mumewe Zablon walikuwa wana kipato kidogo sana kukidhi mahitaji ya familia yao, alisema.

Hata hivyo, miaka mitatu iliyopita, Julius alipata mkopo wa dola 500 kununua taa za umeme jua ambazo aliziuza kwa wateja wake.  Alipopata kipato cha ziada, akachukua mkopo mwingine ili kuendeleza biashara yake ya ushonaji akiongeza huduma za kinyozi, kuchaji simu na duka la vitu mbalimbali vya matumizi ya nyumbani, vyote vikiwashwa na umeme jua.

Sasa, “Tumepata manufaa makubwa sana ukilinganisha na hapo awali. Wastani tunapata shilling 50,000 ( 25$) kwa siku, na hata Zaidi,” alisema.

MAFUNZO KWA WANAWAKE

Mafanikio ya Julius yametokana na mafunzo aliyopewa na shirika la Energy 4 Impact, lenye makao yake makuu jijini London linalofanya kazi Afrika Mashariki na Magharibu kuimarisha matumizi ya nishati jua. Kazi kuu ya shirika hilo ni kuinua wanawake kiuchumi kupitia miradi ya nishati safi na ujasiriamali.

Kiikundi hiki kipya cha WIRE (Women Intergration intointo Renewable Energy) huuunakusudia kusaidia wanawake 400 wajasiriamali mpaka kufikia 2020, na kusaidia baadhi yao kusambaza bidhaa safi za kupikia na kuwashia za umeme jua kwa watu zaidi ya 360,000 nchini Tanzania na Kenya.

Mradi huu ni sehemu ya Ushirikiano wa wanawake wajasiriamali kwa nishati mbadala (wPOWER) uliozinduliwa na wizara ya mambo ya nje ya Marekani mwaka 2013.

Kando na kusaidia wanawake kukua kibiashara, jitihada hii pia imelenga kupunguza hewa ukaa na ukataji holela wa miti kwa ajili ya kuni, alisema Jerry Abuga, msemaji wa Energy 4 Impact.

Godfrey Sanga, meneja wa program ya Energy 4 Impact alisema kusaidia wanawake kuanzisha miradi ya nishati safi ni jambo la maana, wanawake ni hodari sana kuanzisha biashara vijijini na wana uwezo kueneza matumizi ya nishati salama.

Tangu mwaka 2013, vikundi vya wajasiriamaili wa kati 1200, na vile vya wadogo 200 Afrika Mashariki vilisaidiwa na wameona mauzo yao yakiongezeka maradufu kwa zaidi ya asilimia 32 kwa mwaka, maofisa wa mradi walisema.

Julius alisema mafunzo ya uendeshaji biashara na teknolojia kupitia mradi huo ndiyo chanzo muhimu ya kuendeleza biashara yake na kukuza kipato.

“Sina cha kulalamika. Karibu kila mtu hapa kijijini ana furahia huduma yetu inayotumia mionzi ya jua tu,” alisema.

Nchini Tanzania ambapo asilimia 21 tu ya wananchi wanapata huduma ya umeme, kwa mujibu wa Wizara ya Nishati na Madini, kusaidia wanawake kuwa wajasiliamali katika sekta ya umeme jua ni jambo la maana sana kuboresha maisha ya mamilioni ya watu vijijini, alisema Sanga wa Energy 4 Impact.

Takriban asilimia 69 ya watu Kenya na asilimia 95 ya watu Tanzania wanategemea kuni, mkaa na kinyesi ya ng’ombe  kwa kupikia, Kampuni hiyo imesema.

Moto wenye moshi na taa za mafuta ni vyanzo vikubwa vya uchafuzi wa hewa vinavyosababisha vifo takriban 14,300 kwa mwaka nchini kenya na vifo 18,900 nchini Tanzania, Kampuni hiyo imesema.

 VIFAA VINAVYOAMINIKA

Huku matumizi ya umeme wa nguvu za jua ukiwa umeongezeka nchini Tanzania, kupata vifaa bora kutoka kwa wauzaji waaminifu bado ni tatizo kwa watu wengi, Sanga alisema.

Hamasa kubwa kuwekeza kwenye nishati ya jua imewavutia wauzaji wasio waaminifu, ambao vifaa vyao duni kukatisha tamaa watumiaji wa vifaa vya umeme jua, alisema.

“Ubora mdogo na vifaa visivyo na viwango au visivyo halisia ni moja ya mambo yanayokatisha taama watu kutumia teknolojia za nishati, kutokana na kuharibika kwa mara kwa mara na kufanya kazi hafifu, Sanga alisema.

Jitihada za kampuni hiyo ya Energy 4 Impact zimesaidia kuhakikisha kwamba vifaa bora na vinavyoaminika na ufahamu wa namna ya kuvitunza unakuwepo, alisema.

Jitihada hizo pia zinalenga kuleta nguvu ya umeme wa jua vijijini nchini Tanzania ambapo watu wengi wangali hawajui teknolojia hii mpya. Ili kuleta hamasa, mradi huo pia unalenga kuwasaidia wajasiriamali kujitangaza barabarani na kupitia makongamano mbalimbali ya vijana na wanawake na pia kupitia vyombo vya habari” alisema.

“Kwa kuzitangaza hizi biashara zilizofanikiwa na kueleza bayana manufaa ya kutumia nishati safi katika kuongeza uzalishaji, kipato na kupunguza gharama, inatarajiwa kwamba watu wengi watavutiwa kutumia bidhaa hizo maishani mwao na kwenye familia zao,” alisema Sanga.

(Reporting by Kizito Makoye; editing by Laurie Goering : Please credit the Thomson Reuters Foundation, the charitable arm of Thomson Reuters, that covers humanitarian news, climate change, women's rights, trafficking and property rights. Visit http://news.trust.org/climate)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->