×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Wanabiashara Kenya wapunguza taka ya chakula na mshirika mpya: ngamia

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 7 February 2017 11:39 GMT

Stephen Kariuki’s camel herd digs into the morning helpings of fruit and vegetable waste thrown away by traders at the Githurai market on the fringes of Kenya’s capital, Nairobi. TRF/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

A herd of camels have become a low-carbon food waste recycling system in a Nairobi market - and they produce milk

GITHURAI, Kenya, Feb 7 (Thomson Reuters Foundation) – Muuzaji Jacinta Nyokabi alikuwa akihuzunika wakati nyanya zake zilianza kuoza kibandani chake huko sokoni ya Githurai.

Yeye angezitupa kwa mtaro unaopitia kwa soko, au angeziacha tu zikae kwa kibanda. Vyovyote angechagua, yeye angepigwa faini na mamlaka ya soko.

“Nikitupa taka maafisa wa kata watanishtaki kwa kuchafua soko kwa sababu matunda na mboga zinazooza hunuka na kuvutia panya ambazo hueneza magonjwa,” alilalamika mama huyu mwenye umri wa miaka thelathini na tatu na watoto wawili.

Lakini sasa ana wateja wapya wa nyanya zake zinazooza: Fugo la ngamia ishirini ambazo zililetwa kutoka kaskazini mwa Kenya ili kukabiliana na taka ya chakula sokoni.

“Ngamia hula kila kitu tunachowapa na hivyo chakula haitupwi bure,” alisema Nyokabi, ambaye amekuwa akiuza matunda na mboga katika soko hili la kata ya Kiambu, kaskazini mashariki mwa Nairobi, kwa miaka miwili.

Mfumo huu wa taka ya chakula ya soko ulio na kaboni ya chini ni kwa hiari ya Stephen Kariuki, ambaye ni mwenye wanyama hawa na ambaye huwafuga kwa soko kila asubuhi.

MCHAKATO WA MIGUU MINNE

Kujikimu kimaisha, Kariuki alikua akichokora mizizi kutafuta chupa za plastiki, ambazo aliuzia wanabiashara wanaochakata taka.

“Kila mtu anataka plastiki ili kuunda bidhaa zingine,” alisema kijana huyu mwenye umri wa miaka 32 ambaye amalelewa makaazi duni ya Mathare yaliyo kingo la mji mkuu wa Nairobi. “Hakuna mtu anashughulika na chakula zinazooza.” 

Hali hii ilibadilika wakati alipewa kibarua cha kazi ya mkono  na mfanyi biashara wa mbao kaskazini mwa Kenya. Akiwa huko, yeye aliona maisha sugu ngamia hupitia wakati zinatafuta malezi kwa vichaka vinavyokauka.

“Nilikumbuka matunda na mboga mbovu zinazopotea Nairobi na kuamua kujaribu bahati yangu na ngamia,” anakumbuka.

Akitumia akiba yake ya kuuza plastiki ya dola mia moja ishirini alinunua ngamia ya kwanza na kusafirisha sokoni Githurai Januari mwaka wa elfu mbili na kumi na sita. Kutoka wakati huo, Kariuki amerudi kaskazini mwa Kenya na kuongeza ngamia ishirini na tano, pamoja na ng’ombe na mbuzi wachache.  

“Napendelea ngamia kwa sababu haziendi kuharibu mali za watu,” alisema. “Pia ngamia wanapenda taka ya soko kuliko mimea kavu ya hali kame.”

Ngamia pia huleta maziwa ambayo Kariuki huuza, pamoja na mapato mengine.

“Ngamia nono kama huyu anaweza kuchota kama kiasi cha dola elfu moja za Marekani,” alisema huku akitabasamu. “Maziwa yake ni bora sana. Mwisho wa wiki, mimi huzivalisha kistarehe na kulipisha watoto wa mitaani ada kidogo ili waendeshwe.”

Kwa sasa, Kariuki ana wapinzani wachache kwa biashara hii mpya. Na wanabiashara wanashukuru kwamba ngamia zake zimewawezesha kuhifadhi fedha na kuwapunguzia wasiwasi.

Stephen Kariuki’s camel herd digs into the morning helpings of fruit and vegetable waste thrown away by traders at the Githurai market on the fringes of Kenya’s capital, Nairobi. TRF/Kagondu Njagi

SIO YA NG’AMBO

Akiwa kwa kibanda chake kilichotengenezwa na mabaki ya madebe na makaratasi, Nyokabi alisema kwamba ngamia zina umuhimu sana katika soko ambayo haina hifadhi za baridi au mfumo rasmi wa taka, licha ya wanabiashara kulipa ada ya centi hamsini za Marekani kila siku.

Wanabiashara wa soko wanaweza kutozwa faini ya hadi dola moja ya Marekani kila siku wakitupa taka ovyo, alisema.

Kwa mujibu wa Asaah Ndambi, mtafiti wa kituo cha kimataifa cha utafiti wa mifugo, ILRI, Nairobi inazalisha angalu tani 3,200 za taka kila siku. Taka ya mazao ya kilimo huwa ni tani 2000 ya takwimu hii.

Kiwango cha taka hili linatoka kwa mashamba ambayo huzalisha mboga, matunda na maua kwa ajili ya kuuza ng’ambo.

Ripoti ya mwaka wa 2015 ya Feedback Global, shirika lanalokabiliana na taka ya chakula lililo na misingi ulaya, ilisema wakulima wengi hukuza matunda na mboga wakitarajia kuuza soko ya EU, kwa vile ina bei ya kuvutia.

Hata hivyo, zaidi ya asilimia 30 ya chakula hukataliwa ikiwa bado kwa shamba kutokana na kanuni za EU ambazo hukataza chakula kutoka nje kama si sahihi kwa ukubwa, rangi, au sura, ripoti ilisema.

“Chakula hiki huishia kuuzwa kwa masoko ya miji ambapo mahitaji ya matunda na mboga bado iko juu,” alisema Robert Mudida, profesa wa uchumi wa kisiasa katika shule ya biashara ya Strathmore, jijini Nairobi. 

“Barabara mbovu hufanya chakula kubondwa na hivyo kinapofika sokoni kimeanza kuwa mbaya. Mbinu duni ya kuhifadhi huaribi ule usawa uliobaki,” aliongeza. 

(Taarifa na Kagondu Njagi; ukarabati na Laurie Goering:; Tafadhali pigia debe Thomson Reuters Foundation, mkono hisani wa Thomson Reuters, unaoripoti hali ya misaada, haki za wanawake, ulanguzi, haki za mali, na mabadiliko ya hali ya hewa. Tembelea http://news.trust.org/climate)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->