×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Uhifadhi Wa Mikoko Wafaidi Vijiji Vya Pwani, Kenya

by James Karuga | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 28 May 2013 11:30 GMT

Once dismissed as the work of “crazy idlers,” mangrove planting is now boosting incomes

DABASO, Kenya (Thomson Reuters Foundation) – Wakati Kahindi Charo alikusanya marafiki wake 30 kupanda mikoko katika eneo lenye kilomita 32 kilomita mraba la Mida Creek, watu katika kijiji chao cha Dabaso Kilifi, walifikiria hawana kazi na wana wazimu.

Charo anakumbuka mwaka wa 2000, mikoko katika Mida Creek ilikuwa inavunwa kiholela na ardhi ilikuwa imeachwa tu na visiki vikioza na miti ya mikoko iloyozeeka.

Leo, Mida Creek ambayo iko kilomita 60 (maili 38) kaskazini mwa Mombasa imejaa mikoko mingi ambayo hupatia samaki, ndege na wanyama wa maji makao. Bado kuna daraja juu ya maji huko kwa mikoko inayoelekea kwa mkahawa wa kimazingira ulojengwa juu ya ziwa la Indian.   

“Kama hakuna mikoko tungekuwa tumekufa kwani wengi wetu ni wavuvi na samaki hutaga mayai na hula chakula chao kutoka kwa eneo hilo lililofunikwa na mikoko,” Charo alisema akiwa amekaa kwenye mkahawa huo.

 Kazi ya Dabaso Creek Conservation Group (DCCG), haikuwa rahisi. Kwanza walikuwa wakipanda mbegu ya mikoko ambayo haikufaa mazingira ya Mida Creek. Mbegu hizo zilikuwa zinafaa mazingira aina nyingine.

Chini ya nusu ya miti iliyopandwa kwanza na hao kurutu wachunga mazingira ndio ilinusurika tu, Charo alisema.

Wengine katika kikundi walikufa roho wakatoka lakini kunao waliachwa. Siku hizi kikundi kina vijana 26 na ni kati ya vikundi zaidi ya 50 katika vijiji ambazo zinatunza mikoko, na zote zina kama watu 1500 ambao wako katika ufuo wa bahari ya Kenya, kilomita 600 (maili 375).

MAPATO MAPYA YA PESA

Katika miaka 10 iliyopita watunza mazingira eneo la Pwani wamepanda kama mikoko milioni 10 na hiyo misitu inanufaisha vijiji hizo. Wakati watalii, wanakuja kwa wingi kutoka mwezi wa nane mpaka mwezi wa tatu mwaka ufuatayo Dabaso Creek Conservation Group hupata zaidi ya shilingi za Kenya 300,000 (kama $3600) kutoka kwa mkahawa wa kimazingira, lkatika kupeleka watalii kuona ndege na kuuza samaki kasha kukaaa katika hoteli zilizoko Dabaso.

Kama macho ya mradi huo, Charo hupata mshahara siku hizi hata aliacha kazi ya kuuza korosho ndio anufaike.

Kama Charo, Mwatime Hamadi ambaye ako na miaka 29 na hufunza watoto wadogo huko Gazi, kilomita 50 (maili 31) kusini mwa Mombasa ameona mapato yake ya pesa ikiongezeka kwa sababu ya kutunza mikoko.

Hamadi huwa kikundi cha Gazi Women Mangrove ambacho kimesajili wanawake 36 ambao wana mradi wa samaki, nyuki na kaa huko kwa mikoko. Pia kuna daraja katika mikoko ipitiayo juu ya maji ya ziwa Hindi.

Kutembea juu ya hiyo daraja watalii wakenya hulipa shilingi za Kenya 50 (kama dola 0.6) na wa nchi za nje hulipa shilingi 300 (kama dola 4). Hao wamama bado wana duka la vinyago kwa watalii.

Hizo pesa zote husaidia kuendesha mradi wa darasa la watu wazima katika kijiji hicho.

Michael Njoroge, mtafiti wa Kenya Marine and Fisheries Research Institute (KMFRI) huko Gazi alisema kituo hicho husaidia kuelimisha vijiji katika upandaji wa miti aina nyingine pamoja na mikoko- kama Casuarina ambayo inakua kwa miaka kama tatu mpaka tano. Watafiti wanatumai hiyo miti itazuia misitu ya mikoko kuharibiwa.

“Siku hizi tunatumia Casuarina kujenga na kama kuni,” alisema Hamadi. “Ukikata mkoko ambao ni mti unaokomaa baada ya miaka 25, miti mingine haitazuia maji ya bahari kutufikia kama mikoko inavyofanya,”

 Mwaka jana kituo hicho kilipatia wakaaji wa Gazi karibu mbegu 3000 za Casuarina kupanda, hicho kijiji kina watu 1000.

Vituo kama shule, shule ya msingi ya Gazi imepatiana shamba ambalo lapadwa miti aina nyingine. Hiyo miti ikikomaa inauziwa wakaaji wajenge au watumie kwa matumizi mengine.

Shamba ambalo Casuarina imepandwa inazuia mikoko kukatwa hata kama kuna wakaaji maskini ambao hukata  mikoko, kwani hawawezi pata pesa ya kununua aina nyingine za kuni za kupikia kulingana na Njoroge

MARUFUKU YA UKATAJI MIKOKO

Utafiti uliofanywa mwaka wa 2010 na Coastal and Marine Resources Development Africa (COMRED Africa) unaripoti kwamba asilimia 70 ya utumizi wa mbao Pwani unatumia Mikoko na asilimia 80 ya miti miembamba katika ujenzi. Lakini mwaka wa 2000 Rais alipiga marufuku ukataji wa mikoko na marufuku ilifanya ukataji mikoko udidimie na upandaji uongezeke.

Utafiti uliofanywa mwaka jana na Landsat, Ocean Coast Management na KMFRI uliripoti kwamba kutoka mwaka wa 2000 hadi 2010 uharibifu wa mikoko Kenya ulikuwa ekari 3310 ukilinganishwa na ekari 12, 230 miaka nane kabla ya hiyo.

Kenya kuna ekari 133,000 ya mikoko ambayo imetambaa eneo 18 ya msitu ambao uko katika ufuo wa bahari Pwani kulingana na Kenya Forest Service (KFS). Huko Gazi na Dabaso, kabla mikoko ikatwe ruhusa ni lazima ipatianwe na KFS baada ya kujadiliana na vikundi za vijiji zinazolinda mikoko huko. Hizo vikundi pia hupatiana walinzi walipwao na KFS.

Utunzaji mikoko ina manufaa kwa kuzuia hewa kubadilika, maji ya bahari kuharibu vijiji na mumomonyoko wa udongo.

Utafiti uliofanywa na Earth Watch uliripoti kwamba hectare 1 ya mikoko inaweza weka tani 1.36 ya kaboni kwa mwaka sawa na hewa mbaya ya magari sita. Mikoko na mimea mingine ya Pwani kama majani bahari, na nyasi ya matope ya chumvi, zote zinazoitwa kaboni samawati ambazo zinaweza weka kaboni mara 100 zaidi kuliko misitu ya kawaida.  Utafiti ulionyesha.

Wakaaji wanatumai uwezo wa kuweka kaboni ya miti itasaidia wapata pesa huko ufuo wa Gazi wakitumia mfumo unao lipa kwa kuhifadhi mazingira, uiitwao Mikoko Pamoja. Huo mradi unangojea kukaguliwa na kupewa kibali na mpangilio Vivo ambao husaidia kudidimisha hewa mbaya, ukataji miti na uharibifu wa misitu.

Kulingana na mwendeshaji wa mradi Noel Mbaru, huo mradi utaendeleshwa sehemu moja kwa tano wa Msitu wa Ngazi unao hekta 615. Huo mradi unatumainiwa utauza kaboni kama tani 3000 kwa mwaka na utaletea kijiji cha Gazi dola 15,000.

Mradi wa Mikoko Pamoja huchunga pahali miti ya Casuarina imepandwa na unawania kupanda mikoko 4000 kwa mwaka katika miaka ishirini ijayo.

“Mikoko ikiharibiwa, hatutapata pesa wala hatutasomesha watoto wetu, tunafaa tuihifadhi sana,” alisema Hamadi wa Gazi Women Mangrove.

James Karuga ni mwandishi anayeegemea maswala ya ukulima na ubdilikaji wa hewa

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->