Vituo Vya Kawi Vyakuza Matumizi Ya Kawi Endelevu Nchini Kenya

by Justus Bahati Wanzala | Thomson Reuters Foundation
Monday, 24 March 2014 15:30 GMT

A trainer from Ushirikiano, a women's group in Kenya, shows women in Busia County how to make fireless cooking baskets. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Justus Wanzala

Image Caption and Rights Information

Popular regional centres train women, young people for jobs in producing efficient cookstoves and other clean energy technology

Katika jitihada za kupunguza shinikizo kwa misitu ambayo tayari imepungua kutokana na mahitaji ya kuni, serikali ya Kenya imebuni mtandao wa vituo vya kukuza matumizi ya majiko ya kisasa yasiotumia kuni nyingi.

 

Kando na kusambaza majiko hayo na kutoa mafunzo kwa watu kuhusu jinsi ya kuyatumia na kutengeza, vituo hivyo 17 ambavyo idadi yake itaongezwa hadi 21 hivi karibuni, hutoa mafunzo kwa wakaazi wa maeneo ya mashambani kupanda miti ambayo inafaa kutoa kawi na lishe kwa mifugo. Mpango huo ni sehemu ya azma ya serikali ambayo tayari imepewa uzito kwenye rasimu ya sera kuhusu kawi endelevu ya mwaka huu kwa lengo la kukuza matumizi ya kawi ya jua, biogas, na ile inayotokana na maji ikiwemo matumizi endelevu ya makaa na kuni.

Rasimu hiyo ya sera inaeleza kuwa serikali itawajibika kutoa mfumo wa matumizi ya kuni, kuunga mkono upanzi wa miti kwa minajili ya biashara, na pia upanuzi wa teknolojia kuhusu kawi endelevu.

 

Chris Onyango, afisa katika wizara ya Kawi na Mafuta anaeleza kuwa vituo hivyo vimestawishwa kutoka vilivyokuwa vituo vya kutoa mafunzo kuhusu kiklimo cha upanzi wa miti kinachojumuisha ukuzaji wa mimea na ambacho kilianzishwa mwaka 1980 ili kukuza upanzi wa miti pamoja na mimea. Hatua ambayo ilitokana na ongezeko la haraka la idadi ya watu na mahitaji ya kawi.

 

Kulingana na Jeconiah Kitala wa shirika linalokuza matumizi ya majiko ya kisasa la Clean Cook Stoves Association of Kenya, theluthi mbili ya watu nchini Kenya wangali wanategemea kuni kwa minajili ya upishi. Onyango anasema kuwa wataalam waligundua kuwa tatizo la kawi halikuwa tu kwa sababu ya ukosefu wa kuni bali pia kutoweza kupika vyema kwa meko ya kitamaduni na majiko yaliyokuwa yakitumika ambayo hayangehifadhi joto kwa muda mtefu.

Vituo hivyo huandaa maonyesho na mafunzo kwa vijana na wanawake katika maeneo  ya mashambani ili wapate ujuzi wa kutengeza vifaa vinavyotumia kawi endelevu na pia kutoa mafunzo kwa wenzao ili kubuni nafasi za ajira na kutunza mazingira.

 

Katika Kaunti ya Busia, kwenye eneo la Magaharibi mwa nchi, wanawake waliopata mafunzo kwenye kituo cha Kawi cha eneo hilo sasa wameanza kutumia jiko za kisasa ambazo hazitoi moshi huku zikihitaji kuni chache wanapopika. Wengi wamezika meko hizi za kitamaduni ambazo hutoa moshi mwingi katika kaburi la sahau. 

Wanawake hao ambao ni wanachama wa kundi la kujisaidia kwa jina ushirikiano, wamejifunza jinsi ya majiko hayo kutoka kwa vifaa vinavyopatikana kwa kama vile vyuma chakavu, mchanga na tope.  

Kitamaduni, wanawake na wasichana ndio  hutekeleza majukumu ya kupika mara nyingi  wakitumia kuni. Matumizi ya majiko hayo ya kisasa yamewawezesha kutitumia muda mwingi wakitafuta kuni, kumaanisha wasichana wa shule wanapata fursa ya kushiriki shughuli za masomo. 

Beatrice Oduor sasa hutengeza stovu hizo. “Kupitia matumzii ya majiko hayo, uhitaji kukaa jikoni unapopika kwasababu yanaweza kuendelea kupika hata baada ya moto kuzima,” alidokeza. “Cha kuvutia ni kwamba, unaweza kuondoa chakula hicho mekoni na kukiweka kwenye kikapu maalum kinachohifadhi joto huku ukiendelea na shughuli zako.”

Matumizi ya majiko hayo yamepunguza visa vya maradhi ya mapafu hasa miongoni mwa wanawake na wasichana ambao huathirika na moshi wanapopika kwa kutumia kuni kwenye meko ya kiasili. Huu ni ujumbe wa kuvutia ikikumbukwa kuwa watu elfu 14,300 huaga dunia kila mwaka nchini Kenya kutokana na moshi wa kuni.

Hellen Inziani, ambaye ni mwanachama wa kikundi cha Ushirikiano anasema majiko hayo ni ya viwango tofauti na yanadumu kwa muda mrefu huku yakiweza kupika haraka.

“Tunapata hela kupitia kuyatengeza na kuyauza, hali inayopunguza umaskini miongoni mwetu sisi wanawake,” anasema.  Majiko ya kiwango cha chini huuzwa kwa shilingi 300 za Kenya au Dola tatu za Marekani. 

Mkurugenzi wa Maswala ya Mazingira katika Kaunti ya Busia, Ezekiel Moseri  anasema Kauti hiyo ina kiwango kikubwa cha umaskini  na asilimia 80 ya familia hutegemea kawi ya kuni. 

Wakuu wa Kaunti hiyo wanasema matumizi ya majiko hayo imechangia uhifadhi wa mazingira  hasa misitu.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.