×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Mwanasheria nchini Kenya aonya kuwa,Uchimbaji wa mafuta unakiuka malengo ya hali ya hewa

by Pius Sawa | Thomson Reuters Foundation
Monday, 26 May 2014 13:30 GMT

Will the push to extract Kenya's fossil fuels undermine an anticipated new law to promote low-carbon development?

NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) - Kenya iko katika hatua ya kuunda sheria mpya ya hali ya mabadiliko ya tabia nchi, ambayo inatarajiwa kuhidhinishawa hivi karibuni. Wakati huo huo, sekta ya kibinafsi inajiandaa kuanza kuchimba mafuta kaskazini mwa nchi. Je, uchimbaji wa mafuta utaathiri juhudi za Kenya za kupunguza kiwango cha hewa chafuzi?

Baada ya uchunguzi wa mwaka 2007 uliotazamia jinsi mabadiliko ya hali ya tabia nchi ingeathiri taifa la Kenya, mkakati wa kitaifa wa kukabiliana na hali hiyo ulizinduliwa katika kongamano la Umoja wa Mataifa la mabadiliko ya hali ya hewa la mwaka 2009, jijini Copenhagen. Baada ya hapo serikali iliunda mpango wa hatua ya kutekeleza uchunguzi huo ambao ulikamilika mwezi machi mwaka 2013.

Mpango huo unaashiria kuonyesha jinsi ya kukabili hali ya tabia nchi kuanzia kiwango cha mashinani hadi kitaifa. Hatua ifwatayo ni kuuweka mpango huo kwenye sheria. Mwakilishi wa eneo bunge la Emuhaya kutoka Kaunti ya Vihiga na ambaye pia ni muhusika kwenye mswada wa sheria wa hali ya tabia nchi bungeni, Dr. Wilbur Ottichilo, alisema kwamba taarifa iliyokusanywa inatosha kuanza kubuni sheria kwa sababu inaathiri sekta zote. Kutokana na hiyo, kuna haja ya kutunga sheria itakayoshughulikia mambo kuhusu hali ya mabadiliko ya tabia nchi.

Kando na kwamba sheria za nchi ya Kenya zinalenga kuinua hali ya hewa nzuri, serikali ya sasa inazingatia pia uchimbjia mafuta. Mafuta yamegunduliwa maeneo ya Turkana, Nyanza, ziwa Victoria na ufuo wa Bahari Hindi. Mkaa umegunduliwa eneo la Kitui katika mashariki, na madini ya chuma eneo la Taita kwenye ufuo wa bahari. Serikali imebuni mswada wa kuchimba mafuta na kuikabili sekta hii wizara mpya.

Kampuni ya Uingereza ya Tullow imevumbua visima saba vya mafuta kaskazini Magharibi mwa  nchi katika kaunti ya Turkana. Katika taarifa yake ya hivi karibuni mwezi Januari mwaka huu, kampuni hiyo ilisema imegundua hifadhi ya mafuta kiasi cha zaidi ya milioni mapipa 600, na kuongezea kwamba, kwa jumla eneo hilo linaweza kutoa kiwango cha zaidi ya mapipa bilioni moja. Mkurugenzi mkuu wa kampuni hiyo, Angus McCoss, alisema kwamba matokeo yanaonyesha kwamba eneo hilo lina uwezekano wa kuwa mkoa mpya wa gesi ya hydrocarbon.

Nchi ya Kenya inatarajia kwamba matumizi ya rasilmali hii itabuni nafasi za kazi na utajiri. Hata hivyo, Ottichilo anaamini kwamba haya yanaenda kinyume na juhudi za kukabiliana na hali ya tabia nchi. Aliongeza kusema kwamba matarajio yao kama wataalamu wa mazingira ni kuona kwamba uchafuzi wa hewa unapungua, kiwango cha matumizi ya nishati safi yanaongezeka na yale ya mafuta ya ardhini yanapungua.

Jaribio la kwanza la kupitisha mswada wa sheria ya hali ya tabia nchi lilianza mapema mwaka uliopita, wakati raisi alipokataa kutia sahihi mswada huo kutokana na madai kwamba wizara ya mazingira haikuwa imehusishwa katika uundawaji wa sheria hiyo. Lakini wale waliohusika wakati huu wanaamini kwamba kumekuwa na mazungumzo ya kutosha kuhusu mswada huo ambao utawasilishwa bungeni mwezi Juni.

Mswada unataja vitendo ambavyo vinasababisha kuongezeka kwa uchafuzi wa hewa kukiwemo viwanda, moshi kutoka kwa magari, uchomaji mkaa na ukataji ovyo wa miti kwa ajili ya kuni.

Baadhi ya njia zinazokusudiwa ni kuwapiga faini na kuwafunga jela wanaochafua hewa, kuweka mitambo ya hali ya juu ya kuhifadhi nishati katika majumba mpya na maduka ya kijamii ya huduma za nishati ya jua.

Kulingana na sheria hii mpya, wamiliki wa mashamba watatakiwa kupanda miti kwenya asilimia kumi ya mashamba yao na wakulima watasaidia katika kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi hasa kwenye sehemu kavu za nchi.

Ottichilo alionya kwamba uchimbaji wa hifadhi ya mafuta nchini Kenya unaweza kuchangia kinyume baadhi ya kazi hii nzuri. Mataifa ya nchi za Afrika Mashariki yanachangia chini ya asili mia 0.5 ya gesi chafuzi inayotolewa hewani kote duniani, lakini kiwango hicho kinaweza kuongezeka iwapo uchimbaji wa mafuta chini Kenya utaanza kutekelezwa.

“Tumejipata katika hali tata ambapo tumegundua hifadhi kubwa ya nishati lakini kwa wakati huo hali ya dunia inahitaji matumizi ya mafuta asili kupunguzwa. Kwa hivyo, tunavyoyachimba tutakumbana na upinzani mkali.” Alisema mwanasiasa huyo.

Aliongeza kusema kwamba uvumbuzi wa mafuta hakutaisaidia Kenya katika kupiga hatua za maendeleo ikilinganishwa na hali ingelikuwa miaka 20 iliyopita.

Martin Oulu ambaye ni mtaalamu wa maswala ya mabadililiko ya hali ya tabia nchi, alisema uchimbaji wa mafuta nchini Kenya unafaa kupewa mtazamo tofauti.

“Hata kama Kenya inaweza kuonekana kuchangia katika kuchafua hewa kwa uchimbaji wa mafuta, kiwango cha uchafuzi ni ya chini mno ikilinganishwa na mataifa ya kusini yaliyostawi.” Alisema.

Oulu alisema kwamba kiwango cha umaskini nchini Kenya bado kiko juu na hii inasababisha kutofikia malengo ya milenia. Iwapo uchimbaji wa mafuta unaweza kuzalisha mapato kiwango cha kuinua watu kutoka umaskini na ufanyike kutumia teknolojia mwafaka, uchafuzi huo utakubalika.

Aliongeza kusema kwamba ukisimamiwa vyema, uchimabji mafuta hautachangia katika kuongeza uchafuzi ama kwenda kinyume na maadili yaliyowekwa na mpango wa hali ya tabia nchi.

Mpango huo unaashiria kurudisha chini kiwango cha hewa mkaa, maendeleo yanayo stahimili mabadiliko ya hali ya tabia nchi lakini pia inazingatia hali ya sasa ya nchi ikitilia maanani kwamba, nchi ya Kenya ina historia fupi kuhusu mabadiliko ya tabia nchi.

“Kama nchi ya Kenya tuna jukumu letu ndogo lakini tunafaa kuzingatia zaidi mabadiliko ya hali ya kimaisha yanayotendeka katika ulimwengu mzima,” Oulu alisema.

Shirika lisilo la kiserikali linalishughulikia maswala ya kuhifadhi maeneo yaliyokatwa miti, linaamini kwamba uhifadhi wa mazingira na maendeleo, ni maswali yanayofaa kuzingatiwa kila sehemu. Leonard Muhanga ambaye ni mmoja wa maafisa kaitka shirika hili alisema kwamba kuhifadhi mazingira ni jambo tata katika jamii masikini.

“Mtu kutoka jamii maskini hawezi kuamini kwamba miti inaweza kuleta mvua na hewa safi wakati wanapokosa njia nyingine ya kujikimu kimaisha, na hiyo ndiyo sababu tunawapa miradi mbadala kama ufugaji nyuki” alisema.

Muhanga aliongeza kwamba uchimbaji wa mafuta unaweza kuwa njia bora ya kufufua hali ya uchumi ya watu wa eneo la Turkana, kwa sababu uzuri wake unazidi ubaya iwapo uchimbaji mafuta itafanyika kwa njia inyofaa. Kwa mfano, bei ya gesi ya Petroli ya kupikia itakuwa nafuu, watu wataacha kwa ajili ya kupikia.

Mtaalam wa hali ya mabadiliko ya tabia nchi, Martin Oulu, anakubaliana na wazo hili akisema kwamba kutumia gesi badala ya kuni kunaweza kurudisha chini kiwango cha uchafuzi wa hewa, na pia hali ya afya itaimarika kutokana na kiwango cha chini cha moshi.

“Kumbuka, ukataji wa miti ni chanzo kikubwa cha uchafuzi wa hewa nchini Kenya,” alisema. Kulingana na mpango wa hali ya tabianchi wa mwaka 2013-2017, ukataji miti na aina nyingine ya matumizi ya mashamba ilikadiria takriban thuluthi moja ya uchafuzi wa hewa katika mwaka 2010.

Oulu alisema kwamba, athari ya uchimbaji wa mafuta nchini itategemea masharti yanayostahili.

Anatarajia kwamba serikali itaendelea kuekeza katika nishati safi, kama vile biogesi na miradi midogo ya kuzalisha nishati ya maji.

Mwanasiasa Ottichilo alisema kwamba ni heri Kenya ihifadhi mafuta yake kwenye ardhi na badala yake izingatie nishati safi.

Ottichilo alisema kwamba bei ya taa za nishati ya jua inaendelea kupungua kila ujao. Nchi pia iko na uwezekano mkubwa wa kuzalisha nishati ya joto ya ardhi yenye kiwango cha Megawati 10,000. Pia inajenga kiwanda kikubwa zaidi cha nishati ya upepo barani Africa katika eneo la Turkana ambacho kitazalisha megawati 300-400.

“Tukileta nishati hizi zote pamoja, tutapata kwamba hivi karibuni, kwa miaka 10 ijayo Kenya itakuwa na nishati ya kujitoshelez.” Alisema.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->