×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Kabechi zaizidi uzalishaji wa kahawa kwa wakulima wa Tanzania wanaokabiliwa na Ukame

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Monday, 18 May 2015 09:32 GMT

Bernadeta Meela and her neighbour Tumaini Masawe gather vegetables on Meela's family farm in Kanji village, Tanzania. PHOTO/Zuberi Mussa

Image Caption and Rights Information

Higher temperatures and erratic rainfall push farmers to swap coffee and cotton for more lucrative horticulture

KANJI, Tanzania May 18 (Thomson Reuters Foundation)– Katika kijiji kidogo cha Kanji kilichopo kwenye tambarare za mlima Kilimanjaro, Ludovick Meela anajiandaa kukata miti yote mikongwe ya kahawa shambani mwake na kurudishia mboga za majani.

“Hivi ndivyo ninavyoweza fanya kujipatia kipato cha kujikimu, mibuni haileti tena faida kwa kuwa mazao yake yangali yakiporomoka kila kukicha,” alisema. ”Nahitaji mazao yanayokua kwa haraka ili niuze nipate pesa.”

Mkulima huyo mwenye umri wa miaka 72 aliyepo wilaya ya Moshi, vijijini mkoa wa Kilimanjaro, amekua akitegemea kilimo cha kahawa kwa maisha yake. Hata hivyo, mabadiliko ya tabia nchi, pamoja na ugonjwa wa kutu unaofanya mimea kusinyaa and kutoweza kuzaa, vimeharibu kabisa uzalishaji wa kahawa.

Mamia ya wakulima kaskazini mwa Tanzania wanatelekeza mazao ya asili ya biashara, yakiwemo kahawa na pamba kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kuporomoka kwa bei na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji.

Wengi wao kwa sasa wanalima mboga za majani na maua.

“Watoto wangu walivyokuwa wanakua, kahawa ilikuwa ndiyo kila kitu. Nilikuwa nauza na ninapata hela nyingi sana iliyoniwezesha kupiga hatua ya maendeleo, hata hivyo, hayo yote yamebaki kuwa historia,” Meela aliiambia Thomson Reuters Foundation.

Tangu mwaka 2011, mkulima huyo mkongwe amejikita kwenye kilimo cha mboga kwenye shamba lake la eka tisa analolimwagilia –miongoni mwa mboga ni pamoja na kabechi, vitunguu, sukumawiki na viazi ulaya –pia anafuga ng’ombe wa maziwa nyuma ya nyumba yake.

Mzee huyo anaamini huo ni uwekezaji mzuri kwa fedha na muda wake na unatoa fursa nzuri ya baadaye ikilinganisha na kahawa.

“Mahitaji ya mboga za majani na maziwa ni makubwa sana na soko lake linatia moyo sana,” alisema baba huyo mwenye watoto sita.

Meela alisema mvua imekuwa haitabiliki na haiwezi tena kukuza mazao asilia kama vile kahawa, chai, mahindi, maharage na viazi vikuu—na hiyo ndiyo sababu kubwa ya kutafuta mpango wa kilimo cha ziada.

Wakulima wengine Kilimanjaro wanajaribu mazao yanayostahimili ukame kama vile muhogo na alizeti.

 

USIKU WA JOTO

Utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na chuo kikuu cha Witwatersrand juu ya madhara ya mabadiliko ya tabia nchi kwenye uzalishaji wa kahawa ya Arabica, mkoani Kilimanjaro, ulionyesha kwamba joto kali nyakati za usiku lilikuwa ndiyo sababu haswa ya kupungua kwa uzalishaji wa zao la kahawa mkoani humo.

Kwa kila nyuzi joto 1 ya selisiasi ya ongezeko la joto, wakulima wa kahawa walikuwa na uwezekano wa kupoteza kilo 137 za kahawa kwa hekari, ulisema utafiti huo.

Taarifa ya Banki kuu ya Tanzania ya mwezi Machi mwaka huu imeonyesha thamani ya kahawa inayosafirishwa nje ya nchi imepungua kwa takribani asilimia 29 mwaka uliopita, huku zao la pamba likiporomoka kwa asilimia 33.

Kuporomoka kwa uzalishaji umewalazimu wakulima wengi kujikita kwenye mazao ya mboga yanayolipa na maua, huku wengine  wakijaribu kutafuta kipato kwenye shughuli zingine zisizohusiana na kilimo, wataalam wamesema.

Meela amesema pembejeo za uzalishaji wa kahawa zimekuwa ghali mno, huku bei ya kahawa kwa mkulima anayeuza kwenye chama cha ushirika ikiwa imeporomoka maradufu.

Alikuwa akivuna mpaka kilo 250 kwa eka, ambazo aliuza kwa shilling 2500 kwa kilo. Hata hivyo, mazao yameporomoka mpaka kufikia kilo 100 kwa eka na bei ya shilingi 750 kwa kilo.

Kwa sasa, Meela anauza mboga za majani kwa kampuni binafsi za usafirishaji mjini Arusha, na kuongeza kipato chake maradufu.

Faida moja kubwa ya kuzalisha mbogamboga ni kuweza kupanda aina mbalimbali mwaka mzima . Meela kwa sasa anapata wastani wa shilingi milioni 3 kila baada ya miezi mitatu, alisema.

 

PAMBA NJE, VITUNGUU NDANI

Uzalishaji wa pamba, zao linaloajiri zaidi ya watu milioni 14 nchini Tanzania hasa maeneo ya Ziwa Victoria na maeneo ya kati na pwani, pia limeanguka kiuzalishaji.

Wilayani Bariadi, kaskazini mwa Tanzania, mamia ya wakulima wameacha kulima pamba, sasa wanalima vitunguu, vinavyowapa faida kubwa na pia vinaweza kustahimili ukame.

Daniel Manyerere amesema aliacha kuzalisha pamba kutokana na ukame uliokithirii, uliokuwa unaathiri uzalishaji, pamoja na kupanda kwa gharama zingine za uzalishaji. Vitunguu, kwa maneno mengine vinastawi na kupata bei nzuri sokoni, alisema.

Mazao ya mboga, matunda na maua yanazidi kuwa chanzo kikuu cha fedha za kigeni nchini Tanzania. Sekta hiyo ilikuwa kwa takribani moja ya tano mpaka kufikia dola 447 million, na kwa sasa inachangia asilimia 38 ya mazao yote ya kilimo kwenye soko la kimataifa, kwa mujibu wa Tanzania Revenue Authority.

Pamoja mafanikio haya, wataalam wanasema kitendo cha wakulima wengi kukwepa kuzalisha mazao asilia ya biashara na chakula kutokana na athari za tabia nchi hayawezi kutishia hali ya usalama wa chakula.

Hata hivyo, Henry Mahoo, Profesa wa uhandisi wa kilimo chuo kikuu cha Sokoine, amesema sera za kuuza bidhaa ya kilimo nje ni lazima ziendane na mabadiliko ya hali ya uzalishaji ili kuzuia athari kwa wakulima.

Kwa mfano, wakulima nyanda za juu kusini huzalisha ziada ya mahindi na mchele, kwenye maeneo yanayo kumbwa na ukame nchi za jirani za Msumbiji na Malawi.

“Nafikiri ni swala la sera ya serikali kwa kuwa mara nyingi wakulima wanaozalisha mahindi ya ziada hawaruhusiwi kuuza nchi za jirani kutosheleza mahitaji yao mengine,” alisema Mahoo. 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->