Ukungu wazalisha maji Kenya licha ya changamoto

by Benson Rioba | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 1 March 2016 01:11 GMT

Contraptions of huge metal and wooden poles that hold mesh-patterned nets trap fog droplets, which trickle into tanks

ILMASIN, Kenya, March 1 (Thomson Reuters Foundation) - Kwa utaratibu Joseph Kipalian anamimina maji kwa kipara cha kijana mmoja ambaye amesimama kando yake. Matangi ambayo yameekezwa katika uwanja wa shule yanapokea maji kutoka chanzo ambacho si cha kawaida: Hewa.

Shule ya msingi ya Ilmasin iliyoko kwenye milima ya Ngong, kusini mwa jiji la Nairobi ina nyavu ambazo zimeshikiliwa na vikingi vya mbao na vyuma. Nyavu hizi hutumiwa kunasa ukungu na kisha kuuelekeza katika tangi hizo kupitia kwa bomba.

Mradi huo ulianzishwa na chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta ili kubaini uwezo wa kuzalisha maji kutokana na ukungu kwa minajili ya kusaidia wakaazi wa maeneo kame ambayo yana uhaba wa maji. Lakini kuimarisha na kuendesha mradi huyo kumekuwa changamoto.

Bancy Mati, profesa wa uhandisi wa maji na udongo katika chuo kikuu cha Kilimo na Teknolojia cha Jomo Kenyatta anasema uzalishaji wa maji kutoka kwa ukungu ni baadhi ya njia rahissi na mwafaka ya kupata maji safi.

Mati alizindua mradi huu baada ya kuona mradi kama huo ambao ulianzishwa na shirika moja lisilo la kiserekali la Ujerumani kunawiri huko Tanzania .Anadai kuwa eneo la mlima wa Ngong ni mwafaka kwa kuzalisha maji masafi ya ukungu kwa Ngong huwa na ukungu asubuhi na usiku kucha ingawa eneo hilo ni kame na hukabiliwa na uhaba wa maji mara kwa mara.

Iwapo nyavu za kutega ukungu zitaongezwa mara dufu, basi huenda zikaimarisha maeneo kame lakini yenye rutuba nzuri kama Ilmasin. Aidha teknolojia hiyo itasaidia katika unyunyuzi mimea,utunzi wa mifugo na hata matumizi ya nyumba aliongeza mati.

Ana imani kuwa nyavu hizo zitatumiwa katika maeneo mengine mengi huku Kenya hasa katika Kaunti ya Marsabit kaskazini mwa Kenya ambako ni eneo kame lakini lenye ukungu nyingi

CHANGAMOTO SI HABA

Huku technolojia hii ikitumiwa katika maeneo mengi kwa ufanisi mkubwa duniani kama vile nchi za chile na Yemen kutunza nyavu na vikingi vya kunasa ukungu kwa muda mrefu umekuwa changamoto katika maeneo mengi.

Katika shule ya Ilmasin nyavu hizo zilitengezwa mwaka wa 2014 ambapo zilikuwa zikizalisha lita 60 za maji kila siku kiasi ambacho ni nusu ya mahitaji ya wamnafunzi 340 wa shule hiyo,

Kipalian ambaye anasimamia mradi huo anasema kuwa baada ya nyavu hizo kuharibiwa na upepo mkali wa katika mwaka wa 2015 na vikingi kuanza kuharibika sasa awanapata kati ya lita 20-30 ya maji kila siku.

Hali hii imelazimu kuwepo mfumo wa utoaji wa maji kwa mgao na Kipalian anawasiwasi kuwa wanawake na wasichana watalazimika kusafiri mbali ili kupata maji safi ya kunywa ama kutumia huku wakilazimika kuyanuanua licha ya pesa kuwa adimu.

Anaongeza kuwa wakati ambapo  nyavu hizo zilikuwa zikifanya kazi sawasawa, wasichana wa shule hawakuwa wakipoteza muda muhimu wa masomo ili kutafuta maji na pia maji hayo yalitumika katika kunwyesha mifugo mara kwa mara.

Mati anadai kuwa hajapata ufadhili wa kutosha wa kuendeleza mradi huo kwani nyavu hununuliwa kutoka nchi ya Chile na bei ya vikingi vya chuma vya kushikilia nyavu hizo pia ni ghali muno ili hali utumizi wa miti badala ya vyuma haujafua dafu kwani miti huoza haraka .

Mati ana imani kuwa serikali itatoa ushuru inayotoza nyavu hizo na kujaribu iwapo zitaweza kutengezwa humu nchini ili kupunguza gharama za mradi huo kwa kiwango kikubwa .Ana nia ya kuhakikisha kuwa kila boma katika eneo la Ilmasin lini nyavu za kuzalisha maji kutoka kwa ukungu.

John Simel, mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ilmasin ana hofu kuwa huenda kukaibuka matatizo ya afya iwapo hakutakuwa na maji safi ya kunywa kwani eneo hilo hupokea mvua chache. Pia, mvua hukosa kunyesha katika eneo hilo kwa kipindi cha miezi sita .

Simel anasema kuwa technolojia hiyo ya kuzalisha maji kutokana kwa ukungu imesaidia wanafunzi kuelewa umuhimu wa mazingira na raslimali katika kuboresha maisha ya wakazi na pia katika kuzalisha ajira.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.