×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Mpango wa mazao wa Afrika Mashariki wakusudia kupunguza hasara, kuimarisha biashara

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 2 June 2016 12:00 GMT

A woman weeds her maize plantation in Akia village, outside Lira town in the northern region of Uganda, in this Nov. 11, 2009 file photo. REUTERS/Hudson Apunyo

Image Caption and Rights Information

Na Kizito Makoye

KILOSA, Tanzania, Juni 2( Thomson Reuters Foundation)- Shehena kubwa ya mahindi ambayo Jumanne Masele  aliyohifadhi mwaka jana ilikuwa inatosha kukidhi mahitaji ya chakula kwa familia yake na kuiepusha na baa la njaa pamoja na kumpatia kipato kulipa madeni yake—na kadhalika alifikiri.

Muda mfupi wakati Masele alipomaliza kusheheni mahindi ghalani, aligundua kwamba mengi tayari yalikuwa yameharibiwa na vimelea  kutokana na unyevunyevu ardhini uliosababishwa na mvua kubwa  iliyopenyeza maji chini ya kihenga  kilichojengwa kwa majani fito na udongo mkavu.

Richa ya Mavuno mengi, mkulima huyo, mwenye miaka 44 kutoka kijiji cha Mbumi katika wilaya ya mashariki mwa Tanzania ya Kilosa, alipoteza mazao yake mengi  na kutishia usalama wa chakula wa familia yake.

“Ningali sijui namna bora ya kutunza mazao yangu—njia za asili za utunzaji  si stahimilivu tena kwa kuwa nafaka huharibika tunapopata mvua za ghafla.”

 Kilimo ni uti wa mgongo wa  uchumi wa Tanzania, ukiajiri zaidi ya robo tatu ya watu. Sekta ya kilimo inachangia zaid ya nusu ya pato la taifa na mapato ya nje, kwa mujibu wa takwimu za taifa.

Hata hivyo, huku wakulima wa Tanzania wakihangaika huku na kule kutafuta soko la mazao yao, takribani asilimia 40 ya nafaka kupotea bure kutokana na utunzaji hafifu na hali mbaya ya hewa , inayolighalimu taifa $ 332 million every year, serikali inasema.

Kuna jitihada zinazofanyika kudhibiti hasara hiyo. Tangu Mwaka 2013, wakulima wadogo wa nchi za kiafrika wamekuwa wakisaidiwa kupata masoko  ya mazao ya chakula  nje ya mipaka na kuhifadhi mazao yao vizuri chini ya mpango wa miaka mitano unaoratibiwa na shirika la Development Altenative Inc.(DAI)—la marekani linalo fanya kazi na sekta binafsi kuondoa vikwazo kwenye maendeleo.

Ikiwa ni sehemu ya  FoodTrade East and Southern Africa programme, unaofadhililwa na serikali ya Uingereza,  mkopo wa pauni  milioni 3 ( Dola milioni 4) ulitangazwa mwezi wan ne  kuwezesha  wakulima wadogo 70,000 Tanzania na Uganda kufikia  masoko ya nje.

Nchi hizo mbili zinazalisha  ziada ya nafaka  takribani kila mwaka , huku Kenya ikizalisha chakula cha kutosha  kulisha wananchi wake  kwa mwaka  mmoja, kwa mujibu ya shirika la Farm Africa.

HATUA KATIKA KUJITOSHELEZA

Mpaka hivi karibuni, gharama kubwa za biashara ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki zilimaanisha  kwamba ilikuwa ni nafuu kwa Kenya kununua mahindi nje ya  Afrika , hata hivyo mapinduzi ya sera ya hivi karibuni yameondoa vikwazo vya kibiashara eneo la afrika mashariki, Farm Africa ilisema kwenye taarifa yao.

Tangu mwaka 2012, sera za nafaka chini ya Umoja wa Forodha wa Afrika mashariki, zimerahisisha mno kwa wakulima  kuuza mazao yao kwenye nchi za jirani.

Steve Ball, Mkurugenzi wa Farm Africa Tanzania, amesema  mradi mpya  unaolenga kukuza biashara ni hatua kubwa  kwenye kilimo ili kutosheleza chakula eneo lote na kuinua maelfu ya wakulima  wadogo kutoka kwenye umaskini.

Wakulima hao huzalisha asilimia 80 hadi 90 ya mazao ya chakula eneo la Afrika Mashariki, Farm Africa ilisema.

Wataalamu wanatumaini Mradi huo wa FoodTrade utapunguza hasara wakati wa mavuno na kuongeza kiwango cha mazao ya nafaka yanayoingia sokoni nje ya msimu wa mavuno.

“Utasaidia wakulima maskini ambao hawana rasilimali za kuwekeza kwenye njia bora za uhifadhi mazao” Alisema Edith Kija mtaalam wa kilimo na afisa ugani.

Lucy Mtemvu, Jirani yake Masele huko Mbumi, ambaye pia amahifadhi mahindi, mchele na maharage huku akisubiri bei kupanda, alipoteza mazao yake mengi  mwaka jana  na mwaka uliopita baada ya kuvamiwa na jeshi la panya.

Wakulima wa kawaida wanapata shida sana kutafuta masoko ya mazao yao kwa kuwa wanunuzi waliokuwa wakija siku za nyuma  hawaji tena  baada ya barabara kuharibiwa na mvua, alisema.

Gunia la kilo 90 liliuzwa kwa shilingi 140,000 miaka michache iliyopita. “kwa sasa si rahisi kuuza kwa shilingi 90,0000 hata kama unabahati sana ya kuua,” alisema

 MIKOPO KWA WAKULIMA

Vita dhidi ya  njaa nchini Tanzania  imehimarika miaka ya karibuni baada ya serikali  kuanzisha mfumo wa Matokeo Makubwa Sasa, uliolenga kuongeza uzalishaji wa nafaka  kutoka 100,000 ekari hadi  350,000 ekari kwa mwaka kufikia 2016. Hata hivyo ni hivi sasa tu madhara ya uhifadhi hafifu yanaanza kuonekana, wadadisi wa mambo wanasema.

Tanzania kupitia  Shirika la Akiba ya Chakula, ina maghala 33 ya kuhifadhia  yenye uwezo wa kuhifadhi tani za ujazo 246,000, hata hivyo wahusika wanasema hazitoshi.

Farm Afrika na washirika wake itasaidia wakulima wadogo wadogo  nchini Tanzania na Uganda  kutunza nafaka ya mpunga, mahindi na maharage.

Wakulima kwa kuanzia  watauza mazao yao kwenye zaidi ya maghala ya kisasa 100 yenye uwezo wa kuhifadhi zaidi ya tani 500 kila  moja  na kufanya ukaguzi wa ubora kila mara.

Wakulima hao pia watatumia mfumo wa kielektroniki wa G-soko unaoendeshwa na Baraza la Nafaka la Afrika Mashariki, ambao watautumia kuuza mahindi na maharage yao  Kote Afrika mashariki

Pindi wapewapo risiti maalum kutoka ghalani, wakulima wanaweza kuitumia kama dhamana ya kukopa fedha . Hatua hiyo itawaepusha kuuza mazao yao kwa bei nafuu baada ya mavuno na kununua ghali hapo baadae

Mradi huo pia utasaidia  wakulima wadogo kuanzisha vyama vya ushirika  kuuza mazao yao kwa ujumla, na kuimarisha uhusiano na wanunuzi, kitu kitakacho wapa motisha  kuzalisha zaidi.

Jacob Kilasi, anayeishi na familia yake kwenye nyumba ya udongo huko Mbumi, alipoteza mazao yake mengi  miaka miwili iliyopita kijiji hicho kilivyo vamiwa na mafuriko, na kuharibu shehena ya nafaka.

Kuepuka hasara Zaidi, Kilasi—anayelima mahindi, mpunga na mananasi—aliamua kuuza mazao yake kwa bei chee ili yasiharibike.

“Kama nikisubiri, mazao haya yataingiliwa na wadudu na sintapata kitu,” alisema.

 Mpango  mwingine  wa  FoodTrade nchini kenyha umeandaa maghala 10 na benki tano ambazo tayari zimekwisha toa mkopo wa takribani shilingi za Kenya 150 million.

“Siwezi kusubiri kunufaika na mpango huu bunifu—pengine utanisaidia kuuza  mazao yangu huko Kenya  kabla hayajaharibika,” alisema Masele nchini Tanzania

(Imeandikwa na Kizito Makoye; Imehaririwa na Megan Rowling. Tafadhali nukuu shirika la Thomson Reuters Foundation, tawi la hisani  la shirika la  Thomson Reuters, linaloandika habari za majanga , haki za wanawake, biashara haramu ya binadamu, ardhi na mabadiliko ya tabia nchi. Tembelea http://news.trust.org)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->