×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Ladha ya uyoga yasaidia wakulima Tanzania kutunza misitu

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Monday, 18 July 2016 09:23 GMT

When harvests fail, farmers turn to cutting forests - but growing mushrooms could be an alternative

Na Kizito Makoye

BABATI, Tanzania,July 18( Thomson Reuters Foundation)- Magdalena Gwasuma anainama kwa makini kwenye kibanda kidogo chenye giza kilichopo nyuma ya nyumba yake, ambapo amepanga uyonga kwenye chanja za mbao.

“ Sikujua chochote kuhusu kukuza Uyoga nyumbani—tulikuwa tukiuokota msituni,”  bibi huyo mwenye umri wa miaka 60 aliiambia Thomson Reuters Foundation

“ Sikujua kukuza uyonga inaweza kuwa chanzo cha kutengeneza kipato”

Gwasuma , anayeishi karibu na mji wa Babati, kando kando ya msituwa Nou katika mkoa wa kaskazini wa Manyara nchinin Tanzania, kwa sasa ametambua anaweza kuishi bila ya kukata hovyo misitu.

Maelfu ya watu wanaoishi eneo hilo kwa muda mrefu wametegemea msitu huyo kupata kuni au kutengeneza mkaa na kuuza ili kupata kipato, wadadisi wa mambo wanasema.

Wengi wao pia ni wakulima maskini, kama vile Gwasuma, ambao wamekuwa wakisumbuliwa na ukame na mazao hafifu.

 

 “ Mvua hazitabiriki tena, na mabadiliko haya ya hali ya hewa  yameathiri uzalishaji na tumekuwa tukipata mazao hafifu na upungufu wa maji kwa mifugo yetu na matumizi ya nyumbani,” alisema.

Kama iliyo kwa majirani zake, Gwasuma amehamia kwenye uzalishaji wa uyoga aina ya Oyster ili kupata kipato chini ya mradi unaoendeshwa na shirika la kimataifa la Farm Africa linalojihusisha na  shughuli za kuondoa umaskini.

Tanzania ni miongoni mwa nchi zenye uharibifu mkubwa sana wa misitu Afrika kusini mwa jangwa la Sahara, takribani heka 372,000 za misitu huharibiwa  kila mwaka, kwa Mujibu wa ripoti ya  Shirika la umoja wa mataifa la kilimo(FAO)

Miti mikongwe—ambayo ni muhimu sana kuzuia mmomonyoko wa udongo, kusafisha hewa na maji, na kuzuia mabadiliko ya tabia nchi  kwa kunyonya hewa ukaa—inakatwa holela kutokana na mahitaji ya kuni, wataalam wanasema.

 “ Misitu inavyokatwa au kuchomwa, sio  tu ufyonzwaji wa hawa ukaa unasimama lakini hata gesi ukaa inayohifadhiwa kwenye misitu na uoto mwingine wa asili inaachwa isambae hewani na kuongeza idadi ya hewa inayochafua hali ya hewa” alisema Lawrence Kileo, afisa wa Farm Afrika.

KUGANGAMAA NA MABADILIKO YA HEWA 

Huku zao la uyoga kiasili limekuwa likiliwa kaskazini mwa Tanzania, wakulima wengi wamekuwa wakiokota msituni na hawakuzalisha kwa ajili ya biashara.

Lakini Farm Africa kwa sasa inawafundisha wakulima kuzalisha uyoga wa Oyster na kupunguza utegemezi kwenye mazao mengine na kufuga wanyama.

Mradi huo ni sehemu tu ya jitihada nyingi za serikali kusaidia uimara dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi kwa kuhimiza wakulima  kuwa na njia mbadala za kupata kipato.

Familia maskini, ambazo kwa miaka kadhaa zimetegemea  misitu  kwa ajili ya maisha yao, sasa wamefundishwa kuzalisha uyoga, kufuma viondo na kuzalisha asali.

Kwa ufadhili kutoka Umoja wa Ulaya, Farm Africa imewafundisha wakulima 700 kulima uyoga na inatumai ubunifu huo utasambazwa maeneo mengine.

PISHI LA UYOGA

Mfumo wa misitu unakubaliana na  uzalishaji wa uyoga, na wataalam wanawasaidia wakulima kucchagua  maeneo muafaka kujenga vibanda vya kuzalishia uyoga, ambavyo ni lazima viwe na giza, joto na unyevunyevu, Kileo alisema.

Wakulima pia wanafundishwa  namna ya kusindika uyoga ili waweze kuuza ukiwa mbichi au mkavu.

Shirika hilo limeanzisha kituo cha usindikaji na ukusanyaji uyoga ambapo wakulima  wanaweza kuja kuuza  uyoga, Kileo alisema.

Kwa kuwa uyoga  wenye virutubisho vya protein una mzunguko mfupi wa kuzalisha, wakulima wanaweza kuzalisha mwaka mzima  na kupata kipato kizuri, aliongeza kusema.

Kilo moja ya uyoga ni shilingi elf 6000. Gwasuma alisema.

Tangu Farm Africa ianze kutangaza zao la uyoga kwenye jamii ya watu waishio msitu wa Nou miaka saba iliyopita, mahitaji ya uyoga kwa matumizi ya nyumbani yameongezeka, shirika hilo limesema.

Mratibu wa Mradi huo Beatrice Muliahela alisema wakazi wa hapo awali hawakujua namna ya kupika uyoga Zaidi ya kutengeneza mchuzi.

“ Wengi wao pia walihofia kuula kwa kuwa wamekwisha pewa tahadhari kuwa baadi ya aina ya uyonga zina sumu,” alisema.

Ili kuongeza uelewa juu ya zao la uyoga , Farm Africa imekuwa ikiandaa tafrija mbalimbali za chakula  kuonyesha aina mbalimbali za mapishi yatokanayo na zao la uyoga.

That paid off, and to meet growing demand, farmers are being trained to produce mushroom spores so they can expand production.

MUSHROOMING PROFITS

In 2015 around 1,850 bottles of young spores were distributed, and a total of 22,145 kg of mushrooms were produced - of which 10,390 kg were sold fresh and the rest dried.

That earned a net income of 99.26 million shillings (around $49,630), split among 17 groups totalling 300 farmers, Kileo said.

 Hiyo ililipa, na ili kukabiliana na mahitaji makubwa, wakulima pia wanafundishwa  kuzalisha spoa za uyoga ili waweze kupanua uzalishaji

FAIDA ZA ZAO LA UYOGA

Mwaka 2015 zaidi ya chupa 1850 za spoa za uyoga zilisambazwa, na jumla ya kilo 22,145 za uyoga zilizalishwa kati yake kilo 10,390 ziliuzwa zikiwa mbichi na nyinginezo zilikaushwa.

Kilimo cha uyoga kimeleta tofauti kubwa sana ya kipato kwa Gwasuma, watoto wake 9 na familia zao.

Anapata shilingi 480,000 kila mwaka, ambazo ni chanzo kikubwa cha kipato. Kabla ya hapo mumewe ndiye alikuwa akileta mkate nyumbani

“ Kwa kuwa nini kipato cha ziada, tumeweza kusomesha wajukuu wetu, kuboresha lishe zetu na kumudu gharama za matibabu. Pia tumeweza kuimarisha Zaidi mazingira ya nyumbani” alisema Gwasuma

Richa ya mafanikio , uzalishaji wa uyoga  unachangamoto kadhaa, Muliahela alisema. Kuandaa spoa sahihi itakayokuwa vizuri kwenye mazingira ya asili ni  changamoto.

Changamoto nyingine ni masoko kwa kuwa wakulima wanahitaji kuuza uyoga karibu kuepuka usiharibike wakati wanausafirisha kwenye umbali mrefu.

 “Hili ni tatizo kwa sababu wakulima hawapati soko la kutosha na hawana nguvu ya kugalaliza” alisema Muliahela

(Imeandikwa na Kizito Makoye; uhariri na Megan  Rowling:;Tafadhali nukuu Thomson Reuters Foundation, tawi la hisani la Thomson Reuters, linalojihusisha na habari za majanga, mabadiliko ya tabia nchi, haki za wanawake, biashara haramu ya binadamu na haki ardhi. Tembelea www.trust.org)

 

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->