×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Ratiba ya mchanga nchini Ethiopia yawahami wakulima na mbolea mpya katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi

by Pius Sawa | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 29 September 2016 10:00 GMT

In this Ethiopian wheat field, a new blend of fertilisers is being used. TRF/Pius Sawa

Image Caption and Rights Information

Nationwide survey of soil conditions is leading to more effective use of fertilisers and could boost food security

Na Pius Sawa

ADDIS ABABA, Sept 29 (Thomson Reuters Foundation) - Uchunguzi wa kitaifa wa kidigitali  wa udongo nchini Ethiopia  umethibitishwa kuwa chombo muhimu cha kukabiliana na mazao duni.

Juhudi hiyo ya kitaifa ilizinduliwa na mfumo wa habari wa udongo nchini humo, Ethiopian Soil Information System (EthioSIS) mwaka 2012.

Mradi huu katika nchi ya pembe ya Afrika tayari imeanza kuonyesha matokeo kwa kutumia mchanganyiko mpya wa mbolea ambayo imeongeza mazao ya ngano kutoka tani moja hadi tani tatu kwa hekari moja kwenye zaidi ya asilimia arobaini ya mashamba ya kilimo mwaka uliopita.

Kiongozi wa mradi huo Tekalign Mamo alisema kuwa ubora udongo na tabia nyingine za udongo ni vielelezo ambavyo vinahitaji kueleweka vyema ili taifa liweze kulisha wananchi wake. "Ukuzaji wa udongo Ethiopia kwa miaka mingi, hali ya ubora wa udongo nchini Ethiopia- sawa na mataifa mengine barani Afrika imedidimia, na imekabiliwa na upungufu mkubwa wa virutubishi na udorororaji wa mashamba,” alielezea.

"Kutokana na vitendo vya binadamu kama vile ukataji miti, tumeshuhudia mabadiliko ya mifumo ya mvua na kupelekea mafuriko na mmomonyoko wa udongo,” alisema. Mashamba yameharibiwa na mmomonyoko wa udongo asidi na chumvi nyingi mchangani, hivyo kukwamisha uzaishaji, alisema.

Mazao ya nafaka nchini Ethiopia ni chini ya tani mbili kwa hekari moja ambayo ni chini ikilinganishwa na viwango vya kimataifa.

kukabiliana na hili, EthioSIS ilipendekeza serikali ifanye uchunguzi wa udongo ili kuwezesha mbolea kuafikiana na mahitaji ya udongo wa nchini humo, alisema.

Mradi huu unahusisha picha za satellite na deta za ardhini pamoja na habari za kihistoria ili kuchunguza udongo na mvua katika maeneo tofauti kwa ajili ya kupendekeza mbolea inayohitajika kwa mimea, alisema Mamo.

 “Tulielewa kuwa mbolea ambayo tumekuwa tukitumia hususa DAP haikuwa ya manufaa kwa sababu inakosa virutubishi muhimu. Kwa hivyo tulibadili mtindo huo,” alisema Mamo.

Hali ngumu ya hewa na ukataji miti umechagia kuharibika kwa maeneo ya kilimo nchini Ethiopia TRF/Pius Sawa

Wakati wa uchunguzi wa udongo, wakulima walipewa mbolea mpya ili kuifanyia majaribio. Mitambo mitano ya kutengeneza mbolea ilianzishwa katika maeneo manne nchini ili kutengeneza mchanganyiko wa mbolea.

Kiwango cha mahitaji ya mbolea hii kimekuwa cha juu, alisema Tegbaru Bellete afisa mkuu wa miradi katika shirika la mabadiliko ya kilimo. Serikali inatumai kwamba mradi huu utapelekea huduma ya mawaidha kwa wakulima ili kuongeza mazao na mapato, aliongezea.

Katika mataifa yaliostawi mbolea hutengenezwa sambamba na mahitaji ya udongo, alidokeza.

 “Lishe ni lazima ianzie kwenye chakula tunachokuza mchangani kwa njia ya usawa wa kimbolea, lakini hii haijakua hivyo katika mataifa mengi barani Afrika,” alisema.

Sehemu nyingi mashariki na kusini mwa Afrika kukiwemo Ethiopia, Somalia, Zimbabwe, Malawi na Afrika Kusini ziliathiriwa na mfumo wa mabadiliko ya tabia nchi wa Elnino ambao ulisababisha maeneo mengine kuwa na kiangazi na mengine kupata mafuriko hivyo basi kuathiri mazao.

Lakini nyakati zijazo kuelewa kindani hali ya udongo huenda kukasaidia kukabiliana na njaa katika maeneo yalioathiriwa zaidi na hali mbaya.

Uthibiti bora wa maji ikiwemo uvunaji wa maji ya mvua pamoja na unyunyizaji mashamba maji kutaleta mabadiliko, alisema

Mazao ya nafaka huenda yakaongezeka maradufu au zaidi katika maeneo tofauti  ya Ethiopia kama vile Amhara na Oroma.

“Iwapo tutazidisha mazao tunaweza kuwa na masalia ya chakula cha kulisha maeneo yalioathiriwa na hali ya mabadiliko ya tabia nchi,” alisema.

Tangu mradi huu wa kidigitali uanzishwe, Ethiopia imepata kampuni kadhaa za kimataifa za kutangeneza mbolea kukiwemo ICL ya Israeli na OCP ya Morocco, alisema Mamo

Kampuni ya ICL na IPI pamoja na miradi ya kilimo inayofadhiliwa na mashirika ya kimataifa zimekuwa zikishirikiana na EthioSIS ili kutengeneza na kutoa mbolea mpya inayolenga udongo wa nchi hiyo.

Tayari maafisa wa kilimo wa Tanzania wamezuru Ethiopia ili kujifunza kuhusu mradi huo na hivyo kubuni huduma kama hiyo nchini Tanzania.

Mratibu wa shirika la IPI eneo la Afrika mashariki Lilian Wanjiru Mbuthia alisema uboreshaji wa elimu ya udongo utaleta ustawi wa uzalishaji kwa uharibifu wa kiwango cha chini cha mashamba.

"Hii itapelekea kupunguka kwa athari za hali ya mabadiliko ya tabia nchi na kusababisha kuongezeka kwa matumaini ya kuafikia usalama wa chakula katika eneo la Afrika Mashiriki,"alisema.

 (Uandishi ulitekelezwa na Pius Sawa; Mhairi ni Megan Rowling. Tafadhali unapochapisha makala haya tambua Wakfu  wa Thomson Reuters, Kitengo cha misaada cha kampuni ya Thomson Reuters, kinachochapisha habari kuhusu  huduma za kibinadamu, mabadiliko ya hali ya hewa, haki za wanawake, ulanguzi  na haki za umiliki wa mali. Tembelea: http://news.trust.org/climate)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->