GITHURAI, Kenya, Feb 7 (Thomson Reuters Foundation) – Muuzaji Jacinta Nyokabi alikuwa akihuzunika wakati nyanya zake zilianza kuoza kibandani chake huko sokoni ya Githurai.

Yeye angezitupa kwa mtaro unaopitia kwa soko, au angeziacha tu zikae kwa kibanda. Vyovyote angechagua, yeye angepigwa faini na mamlaka ya soko.

“Nikitupa taka maafisa wa kata watanishtaki kwa kuchafua soko kwa sababu matunda na mboga zinazooza hunuka na kuvutia panya ambazo hueneza magonjwa,” alilalamika mama huyu mwenye umri wa miaka thelathini na tatu na watoto wawili.

Lakini sasa ana wateja wapya wa nyanya zake zinazooza: Fugo la ngamia ishirini ambazo zililetwa kutoka kaskazini mwa Kenya ili kukabiliana na taka ya chakula sokoni.

“Ngamia hula kila kitu tunachowapa na hivyo chakula haitupwi bure,” alisema Nyokabi, ambaye amekuwa akiuza matunda na mboga katika soko hili la kata ya Kiambu, kaskazini mashariki mwa Nairobi, kwa miaka miwili.

Mfumo huu wa taka ya chakula ya soko ulio na kaboni ya chini ni kwa hiari ya Stephen Kariuki, ambaye ni mwenye wanyama hawa na ambaye huwafuga kwa soko kila asubuhi.

MCHAKATO WA MIGUU MINNE

Kujikimu kimaisha, Kariuki alikua akichokora mizizi kutafuta chupa za plastiki, ambazo aliuzia wanabiashara wanaochakata taka.

“Kila mtu anataka plastiki ili kuunda bidhaa zingine,” alisema kijana huyu mwenye umri wa miaka 32 ambaye amalelewa makaazi duni ya Mathare yaliyo kingo la mji mkuu wa Nairobi. “Hakuna mtu anashughulika na chakula zinazooza.” 

Hali hii ilibadilika wakati alipewa kibarua cha kazi ya mkono  na mfanyi biashara wa mbao kaskazini mwa Kenya. Akiwa huko, yeye aliona maisha sugu ngamia hupitia wakati zinatafuta malezi kwa vichaka vinavyokauka.

“Nilikumbuka matunda na mboga mbovu zinazopotea Nairobi na kuamua kujaribu bahati yangu na ngamia,” anakumbuka.

Akitumia akiba yake ya kuuza plastiki ya dola mia moja ishirini alinunua ngamia ya kwanza na kusafirisha sokoni Githurai Januari mwaka wa elfu mbili na kumi na sita. Kutoka wakati huo, Kariuki amerudi kaskazini mwa Kenya na kuongeza ngamia ishirini na tano, pamoja na ng’ombe na mbuzi wachache.  

“Napendelea ngamia kwa sababu haziendi kuharibu mali za watu,” alisema. “Pia ngamia wanapenda taka ya soko kuliko mimea kavu ya hali kame.”

Ngamia pia huleta maziwa ambayo Kariuki huuza, pamoja na mapato mengine.

“Ngamia nono kama huyu anaweza kuchota kama kiasi cha dola elfu moja za Marekani,” alisema huku akitabasamu. “Maziwa yake ni bora sana. Mwisho wa wiki, mimi huzivalisha kistarehe na kulipisha watoto wa mitaani ada kidogo ili waendeshwe.”

Kwa sasa, Kariuki ana wapinzani wachache kwa biashara hii mpya. Na wanabiashara wanashukuru kwamba ngamia zake zimewawezesha kuhifadhi fedha na kuwapunguzia wasiwasi.

Topics
Climate Change General Climate Change General