×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Tahadhari Yatangazwa Huku Ugonjwa Wa Mihogo Ukienea Hadi Afrika ya Magharibi

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 16 May 2013 10:15 GMT

Rising temperatures suggest a top climate-resilient crop may not be so resilient after all

NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) – Hatma ya mihogo ambayo ni mojawapo ya mimea zinazostahimili hali mbaya ya hewa barani Afrika, inatishwa na nyuzi za juu zinazosababisha kuongezeka kwa vipepeo weupe ambao hueneza virusi vijulikanavyo kama cassava brown steak virus.

Hapo awali, huu ulionekana kuwa ugonjwa uliokithiri katika maeneo ya Afrika ya Mashariki, na kati. Lakini, virusi hivyo vinaendelea kuenea kwa kasi, huku wanasayanzi wakibashiri kuwa ugonjwa huo wa mimea umeelekea katika nchi inayoongoza duniani kwa upandaji wa mihogo – Nigeria.

Kwa hakika, kulingana na James Legg, mtaalam wa virusi vya mimea katika International Institute for Tropical Agriculture, virusi hivyo kwa sasa vimeenea hadi Angola, Gabon na Jamuhuri ya Afrika ya Kati. Legg amefanya utafiti na kuchunguza kinachosababisha ugonjwa huo Afrika ya Mashariki.

Hata hivyo, wanasayanzi wamefaulu kukabiliana na virusi vingine hatari kama hivyo, vijulikanavyo kama – cassava mosaic disease – vinavyoenezwa na wadudu hao weupe, kisayanzi kama Bemisia tabaci. Hayo yalitendeka kwa kuendeleza mbegu ya mihogo ambayo ni sugu kwa ugonjwa huo.

Lakini, katika mabadiliko ya kiasili, aina zote za mihogo zinaambukizwa ugonjwa huo mpya wa cassava brown steak virus. Wanasayanzi bado hawajagundua aina ya mmea uliyo sugu kwa ugonjwa huo.

Wasiwasi mkubwa kwa sasa ni jinsi vipepeo weupe wanavyoendelea kuongezeka, ikizingatiwa kuwa wadudu hao wanaweza kuenea kote barani Afrika.

Swali muhimu, kulingana na Legg ni kuwa “ Kwa nini wadudu hao wanaongezeka zaidi ya hapo awali?” Aliambia Thomson Reuters Foundation kuwa wadudu hao hunawiri katika nyuzi za juu. Uwezekano ni kuwa nyuzi hizo zinazidi kuongezeka kwa sababu ya mabadiliko ya tabianchi.

Wadudu hao pia wameonekana kuwa na uhusiano wa karibu na virusi vinavyosababisha, ambapo kuna ushahidi kuwa wananawiri kwa mimea zinazougua.

Kwa miaka mingi, mihogo imekuwa mimea mbadala wakati mimeazingine zinavyoangamia kutokana na hali mbaya ya hewa, asema Japheth Akhati, mkulima mdogo katika sehemu ya maghribi nchini Kenya. Lakini, bwana huyo alilazimika kukwepa upandaji wa mihogo mnamo miaka tatu zilizopita. Hii ni baada ya mihogo yake katika ekari moja ya shamba kuambukizwa virusi hivyo kwa misimu miwili mtawalia.

Lilikuwa jambo la kuhuzunisha kuhesabu hasara kutokana na mmea unaojulikana kunawiri wakati wote, asema bwana huyo aliye na miaka 38. Majirani wake katika kijiji cha Esilongo pia wametupilia mbali upandaji wa mihogo.

Virusi hivyo vinaposhambulia matawi ya mimea, zilizoambukizwa zaweza kuonekana kuwa na afya wakati ambapo mizizi zinaoza. Wakati mwingine, rangi ya samawati huonekana kwenye matawi ya mimea zilizoambukizwa huku kikonya kikibadilisha rangi hadi kahawia. Wakati huo, mihogo zote shambani zinaweza kuoza bila ya mkulima kujua.

Wanasayanzi kutoka mtandao wa mashirika matatu – the Global Cassava Partnership, the International Centre for Tropical Agriculture, na the International Institute for Tropical Agriculture – wanafanya kazi pamoja ili kuangamiza ugonjwa huo, na pia kuzuia virusi kuenea zaidi, haswa kuelekea Nigeria, nchi ambayo huzalisha tani milioni 50 za mihogo kila mwaka.

Mashambulizi ya virusi hivyo itakuwa pigo kubwa kwa uchumi wa nchi inayozidi kutegemea mmea huo kwa matumishi ya viwanda na pia kwa chakula. Nigeria hutengeneza nisha kutoka kwa mihogo ambayo inahitajika kote duniani kwa kutengeneza karatasi, nguo na hata tabaka la mbao.

Ruth Amata, mtafiti kutoka taasisi ya utafiti wa kilimo nchini Kenya asema kuwa kuna ushahidi kuwa kutumia mimea zilizoambukizwa kutengeneza mbegu huongeza uenezaji was virusi vya mimea.

Kuepuka hayo, wanasayansi kutoka nchini Kenya wanatafiti jinsi wafanyibiashara wa mbegu wanavyoweza kutengeneza na kuuza mbegu isiyoambukizwa. Majaribio yanaendelea kwa usaidizi wa mpango wa Bio-Innovate, ulio chini ya taasisi ya utafiti wa mifugo kimataifa.

Ili kukuunda mbegu ya mihogo, kikonyo cha mmea huchongwa kwa vipande vidogovidogo, ambavyo hupandwa kama mbegu.  Wanasayansi kutoka Bio-Innovate wanatafiti njia ambazo wafanyabiashara wataweza kutayarisha mbegu hizo kabla ya kuuza.

Mbali na matumishi katika viwanda, mihogo imetambulika kuwa chakula cha siku za usoni katika jamii nyingi, wakati ambapo hali ya hewa inazidi kutishia vyakula vikuu kama vile ngano, mahindi, na mpunga katika baadhi ya maeneo.

Maelfu ya wakulima katika sehemu kame ya mashariki nchini Kenya tayari wameacha kupanda mahindi, na badala yake wanapanda mihogo, mawele, wimbi na mtama kwa sababu mimea hizo zinaweza kustahimili ukame.

Jemimah Mweni, ambaye ni mkulima mdogo kutoka jimbo la Makueni, mashariki mwa nchi ya Kenya aliambia Thomson Reuters Foundation kuwa yeye na wengine sasa wamejua jinsi ya kupika na kula matawi ya mihogo, kutengeneza unga wa mihogo, na kuunda vyakula aina tofauti kutokana na muhogo.

Legg, asema kuwa mmea wa muhogo ni muhimu mno kwa maisha ya baadaye ya Afrika, na hivyo basi, hakuna ruhusa ya mdudu mdogo kuutisha.

Isaiah Esipisu ni mwandishi wa kujitegemea anayependelea maswala ya kimazingira na kilimo. Anaweza kupatiakana kupitia esipisus@yahoo.com.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->