×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Kenya yatazamia nishati ya mvuke kuongeza uzalishaji wa nguvu za umeme

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 20 June 2013 15:31 GMT

With droughts threatening the country’s dominant hydropower, geothermal could also help steady the country’s energy network and create new capacity for industry, experts say

NAKURU, Kenya (Thomson Reuters Foundation) – Kilomita zipatazo kumi kaskazini mwa mji wa Nakuru ulio katika Bonde la Ufa nchini Kenya, kunapatikana volkano iliyo na mojawapo ya kaldera kubwa zaidi ulimwenguni. Kaldera hiyo inayosimama kima cha futi 7,474 kwa usawa wa bahari na kingo ya kuogopesha inatazamiwa na wenyeji kuwa mahali pa kujitoa uhai kwa urahisi. Labda, hivyo ndivyo ilivyojipatia jina lake ‘Menengai’ yaani, maiti – katika lugha ya Kimasaai.

Lakini sasa, kwa ufadhili kutoka mfuko wa uegezaji kwa mazingira kupitia Benki ya Maendeleo Barani Africa, serikali ya Kenya inatumia volkano hii kuzalisha nguvu za umeme kwa kutumia mvuke kutoka arthi ili kuzungusha mitambo.

John Kioli, afisa mkuu katika shirika lisilo la kiserikali la Green Africa Foundation asema kuwa huu ni mwelekeo unaolenga upande mwema, kwani kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa, kunahitajika mbinu mbadala za kuzalisha nguvu za umeme zisizoathiriwa na hali ya hewa.

Katika miaka ya hivi maajuzi, Kenya, ambayo kwa mara nyingi hutumia nishati ya maji, imekumbwa na tatizo la mgao wa umeme, haswa kwa sababu ya upungufu wa maji katika mito zitumiwazo kuzalisha kawi hiyo. Hali mbaya zaidi ilionekana mnamo mwaka wa 2006, ambapo nguvu za umeme zilipungua kwa megawati 90 baada ya mvua kuchelewa. Upungufu huo uliathiri mashule, biashara, hospitali na hata kambi za kijeshi.

Kulingana na takwimu ya kampuni ya kuendelesha nishati ya mvuke iliyobuniwa ili kufanya kazi hiyo nchini Kenya, mradi wa Menengai utaweza kupunguza tatizo hilo la upungufu wa umeme. Inatarajiwa kuwa mradi huo utatoa nguvu zipatazo megawati 400 ifikapo mwaka wa 2017.

Hadi sasa, nguvu za umeme ya juu zaidi kuwahi kutumika nchini Kenya ilikuwa kiwango cha megawati 1,347. Hayo ni kwa muujibu wa msemaji wa shirika la kusambaza nguvu za umeme nchini, Migwi Theuri.

Hata hivyo, Theuri asema, kuwa na kawi ya ziada haimaanishi kuwa sekta hiyo iko salama. Ukweli ni kuwa Kenya imelazimika kugandamiza matumizi ya umeme, hivi kwamba serikali haiwezi kuhimiza uekezaji zaidi utakaohitaji matumizi ya nguvu za umeme.

Kwa kweli megawati 400 zitaingizwa kwenye mtandao, Theuri asema kuwa itavutia waekezaji mara moja. Muekezaji ambaye anahitaji megawati 50 kwa mfano, hawezi kuekeza kabla ya kuhakikisha kuwa kuna nguvu za ziada zenye kiwango hicho. Bure, mashine yake itakosa kufanya kazi itakikanavyo, na hiyo ni hasara.

Nguvu za ziada katika mtandao pia ni muhimu kwa sababu itahitajika kutumika katika mradi wa serikali wa kusambaza nguvu za umeme vijijini kote nchini Kenya.

Kufikia sasa, Benki ya Maendeleo barani Africa imekopesha Kenya dola milioni 124 kuendeleza mradi wa kawi ya mvuke wa Menengai. Msaada mwingine wa dola milioni 25 umetoka kwa Benki ya Dunia, kupitia mradi ujulikanao kama Mfuko wa Uwekezaji katika hali ya hewa.

Kulingana na Mafalda Duarte, msimamizi wa Mfuko wa Uwekezaji katika hali ya hewa, mradi huo utachunguzwa kimakini kwa usaidizi wa sekta ya uadilifu na ile ya kupambana dhidi ya ufisadi ili kuhakikisha fedha hizo zimetumika kwa njia inayofaa.

Nchi ya Kenya imekumbwa na kesi nyingi za ufisadi katika miongo kadhaa zilizopita. Hivi sasa nchi hiyo imo katika nafasi ya 40 kati ya nchi fisadi zaidi ulimwenguni, kulingana na shirika la Uwazi Kimataifa.

Duarte aliambia Thomson Reuters Foundation kwamba Kampuni ya Kuendeleza Nishati ya Mvuke nchini Kenya imedhibitishwa kuwa na uwezo wa kuendesha mradi huo wa Menengai bila tatizo.

Kulingana na Solomon Asfaw wa Benki ya Maendeleo barani Afrika, Mfuko wa Uekezaji katika hali ya hewa umetoa mazingara bora kwa sekta ya kibinafsi kujihusisha na uendeshaji wa miradi za kuzalisha kawi ya mvuke nchini Kenya.

Bwana huyo alisema kuwa kuna uwezekano mkubwa kuwa mradi huo utapunguza bei ya matumizi ya umeme nchini Kenya.

Asfaw alisema kuwa nishati hiyo ya mvuke itaweza kuhudumia watu nusu milioni kote nchini Kenya, wakiwemo 70,000 kutoka vijijini na biashara 300,000. Pia, kawi hiyo iliyo safi itaweza kupunguza kiwango cha hewa chafu ya kaboni kwa kiwango cha tani milioni mbili kila mwaka.

Ingawa mradi huo unatazamiwa kumalizika katika miaka minne ijayo, watu wanaoishi karibu na Menengai wameanza kuhisi dalili za maendeleo katika sehemu hiyo. Wanatumai kutumia umeme huo kujiendeleza hata zaidi.

Dominic Gachie, ambaye ni mkaazi wa Wanyoro, karibu na Menengai asema kuwa mradi huo umesababisha barabara kupanuliwa katika sehemu hiyo. Anaonelea kuwa katika miaka kumi zijayo, sehemu hiyo itakuwa imejijenga hata zaidi.

Maji yaliyo chini ya ardhi ambayo hutoka wakati wa uchimbaji wa visima vya mvuke tayari yanawafaidi wenyeji. Kampuni hiyo pia inatumia maji hayo kunyunyuzia miche za miti, ambazo hupewa wakulima bila malipo.

Kulingana na Benki ya Maendeleo Barani Afrika, Afrika ya Magharibi kwa sasa inazalisha megawati 217 ya nishati ya mvuke, haswa nchini Kenya. Lakini, hii haitoshi, ikilinganishwa na uwezo wa eneo hilo wa kuzalisha nguvu hizo. Wataalam wanabashiri kuwa megawati 10,000 ya nishati ya mvuke inaweza kuzalishwa nchini Kenya peke yake.

Isaiah Esipisu ni mwandishi wa habari maalumu kwakuripoti kilimo na mazingira. Anaweza kupatikana kwa kupitia esipisus@yahoo.com

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

Themes
-->