Misitu takatifu huenda zitahatarishwa na waegezaji, wanasayanzi wameonya

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Friday, 4 October 2013 08:52 GMT

The ever-growing appetite for land among global investors is a threat to sacred forests, which have been protected by the beliefs of indigenous people and are rich in biodiversity

NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) – Misitu takatifu, ambazo zimehifadhiwa na jamii mabalimbali kutokana na imani ya jadi ni mojawapo mazingira chache ya misitu zilizoachwa na wakata miti. Lakini kwa sasa, wanasayansi waonya kuwa zimo hatarini.

Ushahidi umeonyesha kuwa watu wengi, wakiwemo waharibifu wa misitu kwa miaka mingi wameheshimu au kuogopa kuenda kinyume na imani za kidini – na hilo limesaidia kuhifadhi misitu mingi takatifu kwa muda mrefu kote duniani, asema  Prasit Wangpakapattanawong, ambaye ni profesa msaidizi katika kitengo cha utafiti wa misitu, katika chuo kikuu cha Chiang Mai nchini Thailand.

Aina nyingi ya misitu takatifu hupatikana katika nchi za Asia, haswa India, ambapo kwa miongo mingi zimehifadhiwa na wafuasi wa Buddhi, ambayo ni dini ya kiasili nchini India. Wangpakapattanawong alisema hayo katika maonyesho ya sayanzi ya World Agroforestry Centre mjini Nairobi, mwezi jana.

Lakini, hamu kubwa ya mashamba ya uekezaji kote ulimwenguni ni hathari kubwa kwa mazingira hayo ambayo yamekuwa salama, mwanasayansi huyo aliambia Thomson Reuters Foundation.

Mfano mmoja uliotolewa na Wangpakapattanawong ni ekari 500, sehemu ya msitu takatifu wa Arvali ambayo imetengewa waekezaji na serikali ya Jimbo la Haryana. Serikali hiyo imeunda mpangilio maalum unaoruhusu juhudi za uekezaji katika msitu wa Arvali, Wilaya ya Guargaon hadi mwaka wa 2031. Hata hivyo, hatua hiyo imepingwa vikali na jamii asili katika sehemu hiyo.

Nchini Kenya, msitu takatifu wa Mrima ulioko pwani ya nchi hiyo pia umo hatarini kutokana na wachimba migodi wanaotazamia kuchimba madini aina ya niobium, muhimu kwa kutengeneza chuma, vifaa vywa umeme, na hata vile vya matibabu. Lakini wazee wa Kaya ambao wanaogopewa sana katika sehemu hiyo wameaapa kumlaani mtu yeyote atakayejaribu kunyakua msitu huo.

Msitu takatifu wa Mrima ulichapishwa katika gazeti la serikali kama sehemu iliyohifadhiwa mnamo mwaka wa 1961, kwa sababu ni hifadhi kwa aina ya miti iliyo nadra, ndege na hata wanyama wadogowadogo.

Utafiti wa hivi maajuzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Nothern Forestry nchini China ulionyesha kuwa misitu takatifu ni muhimu kwa sababu ni hifadhi haswa kwa wanyama na mimea zilizo hatarini, ijapokuwa misitu hizo zapatikana kwa vipande vidogo vidogo.

Ripoti hiyo ilikadiria kiwango cha hewa aina ya kaboni iliyohifadhiwa katika msitu takatifu wa Sem Mukhem huko Garhwal Himalaya, katika jimbo la Ittarakhand nchini India, ambapo matokeo yake yalibainisha kuwa msitu huo unahifadhi tani 775 za kaboni kwa kila ekari moja.

Kulingana na watafiti, misitu huhifadhi tani 20 hadi 100 zaidi za hewa aina ya kaboni ikilinganishwa na mimea zingine. Hilo hufanya misitu kuwa chombo muhimu cha kupunguza hewa hiyo katika anga.

Wangpakapattanawong akisia kuwa India ina mamia ya misitu takatifu, ingawa hakuna utafiti uliofanywa kubaini hesabu kamili ya misitu kama hizo nchini India na sehemu zingine ulimwenguni.

Kila nchi yafaa kuweka sera zinazofaa ili kukatisha tamaa za waekezaji wanaonyakua misitu takatifu. Hilo ni kwa manufaa ya dunia nzima, asema Meine Van Noorwijk, mshauri mkuu wa kisayanzi katika shirika la World Agroforestry Centre.

Nchini Kenya, imani ya jamii ya Wamaasai inakataza mtu yeyote kukata mti kwa sababu ya kuni ama sababu nyingine yoyote. Pia, ni hatia mtu kudhuru mzizi mkuu wa mti, au kutoa ngozi yote ya mti kwa ajili ya kutengeneza dawa ya kiasili.

Kulingana na imani ya jamii hiyo, ni matawi peke yake yanayoweza kukatwa ili kutoa kuni, na mizizi midogomidogo kwa kutengeneza dawa ya kiasili. Kama dawa hiyo inapatikana katika ngozi, basi jamii hiyo inahimiza mtu kukata sehemu ndogo tu, kwa kuunda sura ya ‘V’. Kidonda hicho kisha kinafunikwa kwa kutumia tope.

Juhudi kama hizo zimeweza kuhifadhi msitu wa Loita katika jimbo la Narok inchini Kenya. Msitu huo una ukubwa wa ekari 33,000 na ni hifadhi ya mimea na wanyama waliohatarini.

Juhudi zingine zinazozingatiwa na jamii ya Wamijikenda katika pwani ya Kenya zimesaidia kuhifadhi ekari 2,000 za msitu wa Kaya.

Msitu huo wa Kaya ni hifadhi ya nusu ya aina zote za mimea katika pwani ya Kenya. Lakini, mimea zingine zinaendelea kuathirika kutokana na mabadiliko ya tabianchi, kulingana na Hifadhi ya Kitaifa nchini Kenya.

Nigel Crahall wa Indigenous Peoples of Africa Coordinating Committee aliambia Thomson Reuters Foundation kuwa jamii mbalimbali za Kiafrika zina ujuzi wa jadi wanaotumia kuhifadhi misitu na mazingira. Kwa hivyo, juhudi kama hizo ni sharti zitambuliwe kitaifa, na kimataifa.

Wangpakapattanawong alisema kuwa misitu mingi takatifu kote duniani zinapatikana milimani, hivi kwamba zinakuwa hifadhi ya maji yanayotumiwa na jamii za karibu, jambo linalowahimiza kuendelea kuzihifadhi.

Jamii nyingi zina elimu ya ndani ya jadi, ambayo ikijumuishwa na sayansi itasaidia kuongeza hesabu ya misitu kote duniani, asema bwana huyo.

Isaiah Esipisu ni mwandishi wa kujitegemea mkaazi wa Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.