Mahitaji ya chakula vijijini yaweza changia Kenya kuondoa marufuku ya GM

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Monday, 13 January 2014 12:36 GMT

Kenya banned the import and distribution of genetically modified foods in November 2012, but the retraction of a scientific study and food insecurity in rural areas could cause a rethink

NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) - Serikali ya Kenya inaonekana kubadili msimamo wake uliopiga marufuku teknologia ya GM kufuatia itikadi ya wakulima wanaoonekana kuikubali hii teknologia ili kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kati ya mwaka wa elfu mbili na tisa na elfu mbili kumi na mbili, kituo kinachoshughulikia teknologia ya GM Kenya, NBA, kiliruhusu mashirika ya msaada kuagiza chakula ya GM kama msaada wakati wa msimu wa ukame.

Lakini mwezi wa Novemba mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili, serikali ilipiga marufuku bidhaa za GM baada ya kuchapishwa kwa utafiti uliodai kuwa mahindi ya GM ilisababisha saratani kwa panya. Ripoti hii ilichapishwa kwa jarida la chakula na kemikali.

Kuna dalili kuwa Kenya inajiandaa kurekebisha msimamo wake juu ya vyakula vya GM, tangu utafiti huu uliofanywa na mwanasayansi wa kifaransa Gilles-Eric Séralini et al kukanushwa mwezi Novemba mwaka wa elfu mbili kumi na tatu.

Serikali ya Kenya haipingi hii teknolojia, waziri wa Kilimo, Felix Kosgey, aliambia Thomson Reuters Foundation mwezi uliopita wakati wa uzinduzi wa kituo cha mafunzo ya sayansi huko World Agroforestry Center (ICRAF), Nairobi.

Kosgey alieleza kwamba kukanushwa kwa ripoti ya Seralini kuwa ni “Mzuri kwa Afrika”, huku akisema kuna umuhimu wa kuelewa uzuri na ubaya wa hii teknologia. “Kenyaitaendelea kupitisha sifa nzuri katika GMOs (mazao yenye vinasaba) na kutengana na zile mbaya,” alisema.

Kwa sasa, kuuza, kusambaza au kutumia bidhaa za GM, bado ni kinyume cha sheria katika Kenya, kulingana na msemaji wa NBA.

Tangu ilianzishwa mwaka wa elfu mbili na tisa, NBA imepitisha nauli ishirini na saba za kuagiza na kupitisha bidhaa za GM kupitia Kenya, lakini shughuli hizi zilisitishwa mwaka wa elfu mbili kumi na mbili.

Hata hivyo, serikali bado hufadhili utafiti wa hii teknologia, ikiwa ni pamoja na GMOs, kupitia baraza la kitaifa la sayansi na teknologia.

MATATIZO YA CHAKULA VIJIJINI

Wakati huo huo, viongozi wa umma katika sehemu kame nchini wanawahimiza wakulima kuanza kupanda mazao ya GM kama jitihada moja ya kuhifadhi kapu la chakula vijijini.

Charles Waturu, anasimamia mradi wa serikali wa pamba za BT huko Kari Thika - ambayo inafanya majaribio ya pamba za GM na ambazo zaweza kupandwa na wakulima mwaka wa elfu mbili kumi na nne.

Yeye asema kuna ongezeko ya wakulima wanaolenga mazao ya GM katika wilaya kame za Kenya kwa sababu inaaminika yana uwezo wa kuboresha usalama wa chakula.

Chini ya katiba mpya ya Kenya, iliyoanza kazi mwezi wa Agosti mwaka wa elfu mbili na kumi, serikali za kaunti zinaweza kuunda sheria zao zinazolenga ajenda ya maendeleo na utoaji ushuru.

Hii imewezesha baadhi ya mikoa yenye uwezo wa kilimo kufinyilia maeneo kame kwa kutoza chakula kodi kulingana na umbali inayosafirishwa, alielezea Odenda Lumumba, mratibu wa kitaifa wa kituo cha maswala ya mashamba.

Changamoto lingine ni kwamba Wakenya zaidi wanawekeza katika kaunti zao, Lumumba alibainisha. Hii inaongeza wananchi vijijini na kuleta shinikizo katika ardhi kutokana na ushindani kati ya ukulima na ujenzi.

Pia inasababisha ukosefu wa ustadi wa chakula vijijini. Wakenya maskini lazima walipie hii gharama ya chakula ghali, au watafute njia mpya za kujilisha wenyewe, Lumumba alisema.

GM INA MAVUNO YA JUU

“Mazao ya GM yanaweza kupunguza uhaba wa chakula kwa sababu yana mavuno ya juu,” alisema Margaret Karembu anayefanya kazi na kituo cha ISAAA.

Kwa mujibu wa Karembu, zaidi ya Wakenya milioni tatu nukta nane wana utapiamlo, wakati zaidi ya milioni kumi na tano wana njaa ya mara kwa mara.

Mazao ya GM yana uwezo ya kuongeza mavuno kwa asilimia kumi na tano hadi ishirini na tano kwa ekari ikilinganishwa na mazao ya kawaida, alibainisha.

Said Silim, mkurugenzi wa kituo cha ICRISAT alisema watafiti wanajitahidi kuboresha mazao, ikiwa ni pamoja na matumizi ya mbinu za GM. “Lakini teknologia hizi lazima zikuwe salama,” alisisitiza.

Lakini si Wakenya wote wanaamini mazao ya GM yana faida.

Mkulima sugu Justus Lavi kutoka kijiji cha Kilome huko mashariki mwa Kenya, ana hofu kwamba mazao ya GM yanaweza kuharibu kilimo asili.

“Maeneo kame ya Kenya yanahitaji teknologia kama vile uvunaji wa maji kuendeleza kilimo vijijini”, alisema.

Wengine kama Wanjiru Kamau kutoka KBioC wasisitiza kwamba hakuna ushahidi unaoonyesha mazao ya GM huongeza mavuno, huku akionya kwamba hii teknologia inaweza kuleta wadudu sugu.

GMOs pia zaweza kuwa hatari kwa mazingira kama vile hasara ya viumbe hai, na zinaweza kuharibu uzalishaji wa chakula, Kamau aliongeza.

“Ushindani wa kimataifa kwa ajili ya kushiriki soko ndio inasukuma GMOs - si kweli zinashughulikia uhaba wa chakula,” alisema.

Kwa sasa, bado haijulikani ni pande gani yaonekana kushinda kwa mapambano ya GM. Lakini wakati changamoto za kulisha familia zaonekana kuongezeka, maeneo maskini vijijini yaonekana kuikubali hii teknologia. 

Kagondu Njagi ni mwandishi wa mazingira mjini Nairobi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.