×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Nchini Kenya, wakulima wageukia ndizi badala ya kahawa

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Sunday, 30 March 2014 16:30 GMT

A woman carries bananas to market in Kenya. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Isaiah Esipisu

Image Caption and Rights Information

As middle-men reduce the profits from coffee, some farmers are turning to growing bananas, even though their need for water may make them less than climate-smart

KIRINYAGA, Kenya (Thomson Reuters Foundation) — Baada ya miaka mingi ya kukuza kahawa bila mafanikio, wakulima wadogowadogo katika eneo la Mlima Kenya wamegeukia mmea wa ndizi na kuekeza katika kilimo cha unyunyizaji wakiwa na matumaini ya kuuza mazao ya mmea huo wenye kiu katika soko za nnje.

Kwa mda mrefu, mmea wa kahawa umetegemewa katika eneo hilo kwa kutoa mazao ya fedha, huku ukikuzwa pamoja na mahindi, ambayo ndio chakula kuu nchini Kenya.

Lakini kutokana na mvua isiyotegemewa, ambayo imedhuru mazao ya mahindi, pamoja na mawakala ambao wamekata mtiririko wa fedha za kahawa, wakulima hao wameamua kukuza ndizi, ambayo huwapatia pesa za kulinda familia zao na chakula kwa watoto wao, kulingana na Jacinta Mugo, mwenyekiti wa kikundi kiitwacho Ramini Banana Farmers Association.

Ndizi ni chakula kikuu katika jamii mablimbali nchini Kenya, lakini hadi hivi maajuzi, mmea huo haukuzingatiwa kuwa na uwezo wa kibiashara, huku wakulima wakiukuza kwa madoadoa katika mashamba yao kama chakula cha nyumbani.

Mugo aliamua kujaribu upanzi wa ndizi katika ekari moja ya shamba lake mnamo mwaka wa 2009. Baada ya kugundua uwezo wa kibiashara katika zao hilo, binti huyo aling’oa miti za kahawa katika kipande cha shamba kilichosalia ili kukuza ndizi.

Ingawa ndizi hutumia maji mengi kuliko kahawa, wakulima wasema kuwa mmea huo una mapato ya kutosha kulipia unyunyizaji, kununua mahindi kwingineko, na kushugulikia mahitaji ya jamii kwa jumla.

Canon Jean Munene asema kuwa mapato ya kila mwezi kutokana na mazao ya ndizi ni mara kumi zaidi ya kahawa.

Ili kujiendeleza na kilimo cha mmea huo, wakulima wa ndizi nusu milioni kutoka vikundi 86 kutoka jimbo la Kirinyaga, wamejiunga pamoja ili kuchukua mkopo wa benki wa shilingi milioni 11 ili kuekeza katika kilimo cha kunyunyiza kitakachogarimu shilingi milioni 23.

Mugo asema kuwa kunyeshe au kusinyeshe, wameamua kuongeza kilimo cha ndizi.

Chini ya mradi wa Karia Water Project, vikundi hivyo vimelipa asili mia 10 ya mkopo huo kama malipo ya mbele. Pesa zingine za mradi huo zitatolewa na shirika lisilo la kiserikali.

Flecia Wambui, mwenyekiti wa Banana Growers Association of Kenya – tawi la Kirinyaga, asema kuwa mradi huo utaimarisha mapato ya wakulima zaidi. Banana Growers Association of Kenya hufundisha wakulima hao kilimo bora pamoja na kuwaunganisha na soko.

Binti huyo asema kuwa vikundi hivyo tayari vimeanzisha mazungumzo na wizara ya maswala ya nje huku wakitazamia masoko ya nje.

Nchini Kenya, Kahawa – ambayo ilielezewa kuwa dhahabu nyeusi kutokana na mauzo mema mnamo miaka za 1980 – imepoteza umaarufu wake kwa wakulima, kwani vikundi vya ushirika vinavyouza zao hilo ng’ambo vimedunisha bei kwa wakulima.

Joseph Muhe, ambaye ni mmoja wa wakulima waliong’oa kahawa ili kukuza ndizi na makadamia miaka sita zilizopita, asema kuwa mmea wa kahawa ulikuwa na ungali dhahabu ambayo haitatizwi na mabadiliko ya hali ya hewa. Mkulima huyo analipa karo ya shule kwa watoto watano kutokana na mazao ya ndizi. “Mawakala wamenyonya utamu wa kahawa wakamaliza,” asema Muhe.

Uuzaji wa ndizi katika eneo la Mlima Kenya umevutia watafiti kutoka chuo kikuu cha Jomo Kenyatta University of Agriculture and Technology, ambao wanatafiti na kuzindua miche ya ndizi kwa kutumia mbinu za kilimo cha tishu, huku wakiwafunza wakulima jinsi ya kutunza mimea hiyo.

Mbegu hizo, ambazo zinakuzwa ili kuunganisha sifa za uzalishaji bora, kukua kwa haraka na kustahimili hali mbaya ya hewa, zimewavutia wakulima wengine wengi wanaotazamia kuekeza katika kilimo cha ndizi haswa katika eneo la Kenya ya Kati.

Mmea wa ndizi unaendelea kuwa maarufu nchini Kenya hivi kwamba serikali imezindua mkakati endelevu wa kitaifa, utakaosaidia kuimarisha kilimo cha zao hilo ifikiapo mwaka wa 2016.

Mmea huu kwa siku nyingi umekua mmea wa kusaidia wanawake kujipatia hela kidogo, asema Munene, ambaye ni mkulima kutoka kijiji cha Ndieni. Lakini, asema mkulima huyo, juhudi za kuuza zao hilo kwa kupitia vikundi kumevutia wanaume, ambao wamejiunga na wanawake kutokana na pesa tamu ya ndizi.

Isaiah Esipisu in mwandishi wa kujitegemea maarufu kwa maswala ya kilimo na mazingira. Anaweza kupatikana kupitia esipisus@yahoo.com

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->