×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Bima ya kahawa yapunguza uchungu wa hali ya hewa kwa wakulima nchini Kenya

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Friday, 18 July 2014 07:30 GMT

Kathuni Ntaari picking coffee at his farm in Muiru village, Kenya. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

Insurance is helping Kenya's farmers stick with coffee - a good money maker - as growing it becomes more difficult

MURANG’A, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Kahawa, ambayo ilikuwa zao la biashara nchini Kenya imekuwa na shinikizo za mabadiliko ya hali ya hewa. Baadhi ya wakulima wamebadili na kilimo cha mazao yanayovumilia hewa sugu; wengine wapambana, na bado hawapati lishe tosha la kuishi.  

Lakini kwa wengi wa wakulima wa kahawa nchini Kenya, bima inayolinda mavuno dhidi ya hasara inayoletwa na hewa sugu imefanya kilimo cha kahawa kuwa jambo lisilo na unchungu mwingi.

Kwa kushirikiana na taasisi za kimataifa kama vile Kituo cha Maendeleo Endelevu, Benki ya Dunia, Kituo cha Rockefeller, na Idara ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa, makampuni ya bima nchini Kenya yamewekeza kwa bima inayoshughulikia wakulima ambao hupoteza zao lao kutokana na mafuriko, ukame, au majanga mengine ya hali ya hewa tatanishi.

“Bima ya kilimo ni muhimu hasa nchini Kenya na maeneo mengine Afrika kwa sababu mitindo inayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa inaleta shinikizo kwa uzalishaji wa chakula na hata bei yake,” alisema Wilson Songa, katibu mkuu wa wizara ya kilimo, Kenya.

Tangu mpango huu ulipozinduliwa mwaka wa elfu mbili na kumi na moja, mamia ya wakulima nchini Kenya wamepata faida.

Mwaka jana Peter Chege, mkulima kutoka kijiji cha Gacharaigo huko kati Kenya, alipoteza mavuno yake wakati kahawa ilipatwa na maradhi yanayoletwa na fangasi, baada ya mvua mkubwa kunyesha shambani mwake. Lakini kama mwanachama wa mpango wa bima, alilipwa fidia, hivi kwamba hakupata hasara kubwa.

“Pato la kahawa hapa ni duni sana kwa sababu ya magonjwa yanayoletwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema Chege. “Hata wakati hali si mbaya vile, sisi bado lazima tununue madawa ya kuyazuia magonjwa, na wengi wetu hatuwezi.”

Miongo miwili iliyopita, shamba la Kathuni Ntaari lingekuwa limejaa watu msimu wa kuvuna kahawa. Wanakijiji walimiminika kwa wingi nyumbani kwa Ntaari kwa sababu alijulikana kama mkarimu kwa yeyote aliyetafuta kibarua shambani mwake.

Lakini kwa sasa, mzee huyu huvuna kahawa peke yake, na pato analouza haliwezi kutosheleza familia yake kwa milo mitatu kwa siku.

Katika kilele chake katika mwaka wa elfu moja mia tisa na themanini, kahawa ilikuwa moja ya zao bora Kenya, huku nchi ikiuza tani elfu mia moja na thelathini katika soko ya nje kila mwaka.

Tangu wakati huo, mabadiliko ya hali ya hewa yamesababisha kushuka kwa pato la kahawa. Sasa Kenya ina karibu ya ekari elfu moja na sabini za ardhi ambazo hukuzwa kahawa, huku pato lake likiwa tani elfu hamsini kila mwaka.

‘NILIKUWA TAJIRI.. LAKINI SI TENA

“Nilikuwa tajiri wakati mmoja kwa sababu ya kahawa lakini si tena,” alisema Ntaari. “Lakini siwezi wacha kuilima kwa sababu bado nina matumaini kwamba zao hili litakuwa na fedha.”

Uamuzi kama huu ni nadra sana katika kijiji cha Ntaari huko Muiru, mashariki mwa Kenya. Idadi ya majirani wake wamekata tama na hata kufyeka kahawa ili wapande vyakula vya lishe kama vile mahindi na maharagwe. Kwa wale bado wameamua kundelea kulima kahawa, fedha kidogo wanazopata hutumika kununua chakula na kulipa ada ya shule.

Kwa vile idadi ya Wakenya yaendelea kuongezeka, wakulima wengi hawana ardhi ya kutosha ya kulima vyakula, asema Dennis Maina, afisa ambaye anashirikiana na makampuni kama vile Sygenta Afrika Mashariki, kuamua jinsi bima ya kahawa inafaa kusambazwa. Wale wako na mashamba “hujikuta zao lao limefeli kutokana na majanga ya hali ya hewa kama vile maporomoko ya ardhi na baridi,” aliongeza.

Kuwekeza kiasi kidogo cha mapato kwa bima kunaweza kusaidia baadhi ya wakulima wa kahawa Kenya kutoka maisha duni hadi yale ya faida, Maina alisema.

“Kile tu mkulima anachohitaji kujiorodhesha na mpango huu ni kipande cha ardhi, kahawa, na akiba ya kununua bima,” alisema. “Lakini kuna changamoto, kama vile kuamua ni kiasi gani cha bima mkulima anafaa kulipa kwa ekari na hata kiasi anachofaa kulipwa mkulima, kulingana na jinsi msimu umekuwa mbaya.”

MATATIZO YA HALI YA HEWA DUNI, AU MICROCLIMATES

Kuhesabu gharama sahihi inakuwa ngumu kwa sababu ya hali ya hewa duni Kenya inayoitwa kwa kimombo microclimates - ambayo inapatikana kilomita chache tu - na ambayo ni tofauti na hali ya hewa ya maeneo jirani.

Kwa mfaano, kijijini mwa Chege hali ya hewa ni baridi, huku ile ya kijiji cha Ntaari kama umbali wa kilomita mia mbili, ni joto sana.

Kwa mujibu wa ripoti ya mwaka wa elfu mbili na kumi na mbili inayoshughulikia ukulima wa bima, na ambayo ni mradi wa serikali ya ya Kenya na Ujerumani, hali mbaya ya hewa inaleta madhara kwa mazao katika vijiji zote mbili.

Kahawa aina ya Arabica, na ambayo ni asilimia tisini na tisa ya kahawa Kenya, inahitaji joto ya nyuzi kumi na nane hadi ishirini na moja ili kuzalisha vizuri, ripoti yasema. Juu ya hapo, kahawa yaweza kupatwa na uvimbe na kupoteza maua yanayoleta zao.  Joto chini ya kiwango hiki yaweza kuleta ugonjwa unaoitwa kwa kimombo, coffee berry disease.

Huku hali ya hewa duni ikisababisha tofauti ya joto katika maeneo madogo Kenya, wanabima bado wanajitahindi kuendeleza bima fanisi, ambayo kwa kawaida malipo yake hutegemea baadhi ya joto au mvua kizingiti kufikiwa.

Vincent Nduati, afisa wa kampuni ya bima ya UAP, alisema kwamba kwa sasa kahawa hutegemea hesabu za mvua ili kuamua malipo.

Hata hivyo mfumo uliopo sasa unasaidia wakulima ambao wamekataa kuachana na kahawa.

“Bima ya kahawa ni mzuri kwa sababu hata wakati zao ni la chini nina uhakika wa kupata kitu cha kutegemea hadi msimu ujao wa mavuno,” Chege alisema.”

Kagondu Njagi ni mchangiaji wa kujitegemea kwa Thomson Reuters Foundation, mjini Nairobi na huandika juu ya masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->