×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Katiba mpya ya Tanzania yatambua haki za wanawake kumiliki ardhi

by Kizito Makoye | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 8 October 2014 15:33 GMT

Female entrepreneurs from Mndolwa village in Tanzania's Korogwe district dance after their group qualified for soft loans from the Vodacom Foundation in August this year. PHOTO/Zuberi Mussa

Image Caption and Rights Information

Few Tanzanian women own the land they farm, as customary laws trump their official rights

DAR ES SALAAM, Tanzania (Thomson Reuters Foundation) - Sakina Mzava alikuwa angali akiombeleza msiba wa marehemu mumewe alipofukuzwa na baba mkwe kwenye nyumba aliyokuwa akiishi kijiji cha Vikindu Mkoa wa Pwani. Wakati huo huo akimnyang’anya hata kipande cha ardhi walichokuwa wakilima mazao.

“Nilivunjika moyo kabisa, sikua na jinsi yoyote, niliacha tu. Nilijua hiyo ndiyo tamati ya maisha yangu,” aliiambia Thomson Reuters Foundation.

Sheria za kimila kwenye kijiji chake wilaya ya Mkuranga zinasema kwamba wanawake watapata ardhi kupitia kwa waume zao au ndugu wa kiume, na baada ya kifo cha mumewe undungu kati ya Mzava na shemeji zake uliishia hapo.

“Walikuwa wakali sana, ilinibidi nikimbie na watoto wangu kuomba hifadhi nyumbani kwa dada yangu,” alisema mjane huyo mwenye umri wa miaka 35.

Mama huyo wa watoto wawili amekuwa akitishiwa na shemeji zake. Wakimshutumu kusababisha kifo cha kaka yao, aliyefariki baada ya kuugua kidogo ili waweze kuridhi mali za familia na shamba.

“Walichukua kila kitu,” alisema. “Hawakuniacha na chochote cha kulisha watoto wangu. Sikuweza kuzalisha chochote, wachilia mbali mbogamboga.”

Katiba inayopendekezwa ya Tanzania inatoa matumaini mapya kwa wanawake katika msimamo ule ule, kwa kuwa ina lugha inayoeleza kinaganaga kwa mara ya kwanza kuwa wanawake wana haki sawa kutumia na kumiliki ardhi.

Mzava aliyeolewa kwa ndoa ya kimila, alipoteza karibu kila kitu kwa kuwa ndoa za aina hiyo huwa haziandikishwi ikiwa na maana kwamba ni nadra sana kupata haki yake iliyoporwa.

Mkasa wake unaelezea masaibu yanayowakumba wanawake wengi vijijini, ambao licha ya kubeba dhamana kubwa ya majukumu ya kifamilia, hawapati chochote wanapopewa talaka au waume zao wanapofariki.

 KUTAMBULIKA KWENYE NGAZI YA JUU

Huku sheria rasmi zikibainisha haki sawa kwa wanawake wa Tanzania kupata na kumiliki ardhi, sheria za kimila na mila potofu- ambazo bado zinatawala kwenye maeneo mengi nchini-zinazuia upatikanaji wa haki hizo.

Kukosekana kwa chombo cha usimamizi na ujinga uliokithiri husababisha, wanawake ambao ni zaidi ya nusu ya nguvu kazi kwenye kilimo, kushindwa kumiliki ardhi wanayotumia kulima.

Katiba mpya inayopendekezwa, iliyoidhinishwa na bunge wiki iliyopita, bila shaka, itakuwa sheria bila ya mabadiliko yoyote. Ilikabidhiwa rais wiki hii, atakayeitisha mchakato wa kuipigia kura. Kwa mujibu wa waziri mkuu Mizengo Pinda, Tanzania itapata katiba mpya kabla ya uchaguzi mkuu Octoba mwakani.

Ibara ya 22 ya katiba inayopendekezwa inasema, “kila mwanamke ana haki sawa kupata, kumiliki na kutumia ardhi kwa masharti yale yale kama ilivyo kwa wanaume.”

Wadadisi wa mambo ya kisheria wanatarajia kwamba kipengele cha katiba kinachotoa haki ya wanawake kumiliki ardhi kitabadili taswira ya mambo yalivyo kwa sasa, kwa kuwa itatoa nguvu kubwa zaidi kisheria zaidi ya sheria za kimila ambazo ni kandamizi na zenye ubaguzi na kwa sasa zina hadhi sawa mahakamani kama ilivyo kwa sheria nyingine yoyote.

“Ni muhimu kutambua haki za wanawake ili kuwalinda dhidi ya udhalimu wanaofanyiwa na mfumo dume.” Alisema Andrew Chenge, mwenyekiti  wa kamati ya uandishi wa katiba.

Jamii ambayo ardhi yake haisimamiwi vizuri huwa hatarini kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara. Chenge alisema. Sura maalum kwenye katiba mpya inayozungumzia maswala ya ardhi itasaidia kutatua migogoro, hasa kati ya wakulima na wafugaji, wengi wao wakiwa ni wanawake, alisema.

Wanaharakati wa haki za wanawake wanaimani kwamba sheria mpya itasaidia wakulima wanawake kula matunda ya kazi zao za kilimo.

“Katiba inayopendekezwa imeeleza vizuri neno ‘mtu’ kwa kuwa kwenye jumuiya nyingine watu wanaamini mtu ni mwanaume na si mwanamke,” alisema Anna Abdallah, mwanaharakati wa haki za wanawake na mjumbe wa bunge la katiba. “        Huu ndio usawa tuliokuwa tukipigania.”

Usu Mallya wa Mtandao wa jinsia Tanzania (TGNP) alisema usawa wa jinsia ni swala nyeti sana kwenye katiba inayopendekezwa, na bila ya hiyo wanawake wataendelea kukandamizwa.

“Tunauhakika kwamba sasa tunakatiba inayo toa haki kwa wanawake kupata, kumiliki kutumia na kuendeleza ardhi na kunufaika na maliasili,” alisema.

CHANGAMOTO ZA TABIA NCHI

Haki za wanawaki kumiliki ardhi zilinukuliwa rasmi kwenye sera ya taifa ya Tanzania miaka ya 1990’s, ikiwa na lengo la kudumisha usawa katika ugawaji ardhi. Kwa nyongeza, sheria ya ardhi ya mwaka 1999 kwa ujumla inatoa haki kwa wanawake kupata, kumiliku na kutumia ardhi kama ilivyo kwa wanawake, pamoja na haki zao kushiriki katika ngazi za kutoa maamuzi yanayohusu  maswala ya ardhi.

Licha ya haya yote, wataalam wanasema  wanawake wengi-hasa wakulima vijijini, wangali wananyanyaswa na kunyang’anywa haki hizo.

Baadhi yao wanahofu kwamba kuingizwa kwa haki za wanawake za kumiliki ardhi kwenye katiba huenda isibadilishe hali halisi ilivyo kwa kuwa hamna mifumo za usimamizi wa ardhi.

Yefred Mnyenzi wa Haki Ardhi alisema misingi mikuu ya kutambua haki za ardhi nchini Tanzania zingali zikipendelea watu wenye nguvu na wenye mamlaka wakiwemo wawekezaji wa nje?

Kufuatia bashasha kuu ya shughuli za kibiashara kwenye ardhi ya kilimo, katiba ingaliweka mfumo wa kuzuia ardhi ya kilimo kuporwa kutoka kwa wakulima maskini wanaoihitaji kwa maisha yao. Mnyenzi alisema.

Kilimo kingali chanzo kikuu cha kipato kwa wanawake wengi vijijini ambao hawana fursa nyingi za kiuchumi. Hata hivyo, mada haya ya tabia nchi yanachangia kuwadidimiza.

Wakulima wengi wametambua umwagiliaji kama ni mkakati wa kuwasaidia kukabiliana na mabadilikoya tabia nchi. Hata hivyo, wataalam wanasema wanawake wachache wananufaika  na umwagiliaji kwa kuwa wanaume wanaonekana wana haki zaidi za ardhi na shughuli za kilimo kiasi cha kusababisha mzozo.

Imehaririwa na Megan Rowling

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->