Uhamiaji unaotokana na hali ya hewa waongeza magonjwa Ethiopia

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Monday, 3 November 2014 06:45 GMT

Ethiopian farmers make their way towards agricultural plantations in search of work as migrant laborers. THOMSON REUTERS FOUNDATION/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

As crops fail, highlanders look for new work – and end up contracting HIV and kalaazar

GONDAR, Ethiopia (Thomson Reuters Foundation) - Wakati hali ya hewa duni iliharibu zao lake la mahindi, ngano na shayiri huko Maksegni, mkulima huyu mwenye umri wa kati alihamia Metemma huko kaskazini-magharibi mwa Ethiopia kutafuta kazi kwa mashamba ya ufuta na pamba.

Yeye alipata zaidi ya kazi. Leo, raia huyu mwenye umri wa miaka thelathini na tisa ameambukizwa na visceral leishmaniasis – ugonjwa unaoitwa kwa kawaida kalaazar - na ukimwi.

Baba huyu wa watoto wawili ambaye anatibiwa katika chuo kikuu cha Gondar, ni miongoni mwa raia elfu mia tatu wa Ethiopia ambao huhamia mashamba makubwa karibu mpaka wa Sudan kila mwaka, kutafuta lishe huku mashamba yao yakiendelea kupunguza mazao.

Lakini wanapokimbia kutokana na njaa, wao huingia eneo la usubi, na kuumwa na mdudu anayeeneza kalaazar, ugonjwa ambao ni hatari kama haujatibiwa. Upweke wa kuwa mbali na familia pia huwaweka hatarini ya kupatwa na ukimwi, watafiti wasema.

“Ni eneo la kalaazar,” alieleza Ermias Diro, mtafiti katika kiliniki ya chuo hicho. “Wengi husafiri kutafuta kazi na katika shughuli hizo, wao huumwa na usubi.”

“Baada ya kazi siku nzima katika mashamba, wao hupumzika kwa kivuli cha mti,” aliongeza. “Ni mahali joto sana ambapo wengi wao huwa hawajavaa kikamilifu, hivyo kupata kuumwa.”

MIMEA KUFELI, UHAMIAJI KUONGEZEKA

Wataalam wamehusisha ukosaji wa mvua na mazao kufeli, kwa ongezeko la wafanyikazi wahamiaji nchini Ethiopia. Watabiri wa hali ya hewa wasema Maksegnit hurekodi kiasi cha milimita elfu moja na hamsini na tisa msimu wa kilele, lakini kwa miaka michache iliyopita, mvua imekuwa chini kama milimita mia tatu kumi na saba.

Hii imesababisha kushuka kwa kilimo cha vyakula, wakati kilimo cha zao la biashara katika maeneo tambarare chavuta maskini kutoka nyanda za juu, na kuelekea kwa vitisho vipya vya afya.

Mabadiliko ya hali ya hewa pia yanabadili usambasaji wa wadudu hawa, alisema Daniel Argaw Dagne, wa mpango wa kudhibiti ugonjwa huu katika Shirika la Afya Duniani (WHO).

“Kalaazar ni ugonjwa ambao husambazwa na wadudu ambao husukumwa na mabadiliko ya hali ya hewa,” alisema. “Kuongezeka kwa joto duniani husababisha ukuaji wa wadudu hawa.”

Fabiana Alves, meneja wa mradi unaohusika na magonjwa haya ama Drug for Neglected Disease Initiative, kuambukizwa kwa wahamiaji mara mbili na ukimwi na kalaazar “ni mzigo wa magonjwa ambao hatujaona nchi zingine na hata Afrika mashariki.”

Mradi katika kliniki ya kulevya kwa magonjwa yaliyosahaulika Initiative, alisema mara mbili kuambukizwa na wahamiaji wenye HIV na kalaazar "ni mzigo wa magonjwa kwamba hatuoni katika nchi nyingine hata katika Afrika Mashariki." La kushangaza zaidi, “matibabu na madawa yaliyopo yamekuwa magumu,” alisema.

Katika Chuo Kikuu cha Gondar zaidi ya asilimia kumi na tano ni wagonjwa, na utafiti wa matibabu mapya unaendelea. Lakini upimaji na tiba vijijini pia unahitajika, wasema wataalam, na itakuwa vigumu.

HAJA YA VITUO VYA MATIBABU VIJIJINI

Hasrat Hailu Mekuria wa chuo kikuu cha Addis Ababa alisema umbali wa safari na kutengwa kijiografia inamaanisha wahudumu wa afya hawawezi kufikia baadhi ya vijiji, wakati wengine wanakosa miundombinu ya msingi.

"Ukosefu wa maji, usafi na nishati katika vijijini ni tatizo kubwa kwa sababu uchunguzi wa kalaazar wahitaji majokofu au hifadhi baridi,” alisema Mekuria.

Wataalam wasema kuanzisha kliniki za msimu na kuweka wafanyakazi wa afya katika jamii kunaweza kusaidia wakaazi wahamiaji.

Kenya, wakati huo huo, ina matatizo yake kutibu kalaazar, alisema Anderson Chelugo, afisa wa kliniki katika kituo cha tiba, Kimalel, ambapo mtandao wa barabara, nishati na mawasiliano ni mbaya.

Kukatika kwa umeme katika kituo hicho ambacho hutibu na kuchunguza wagonjwa wa kalaazar hutokea kwa siku mzima kama mara tatu kwa wiki, alisema.

Kituo hiki ambacho kiko sehemu kame ya nchi, bado hakijawekeza vyanzo mbadala vya nishati, kama vile nishati ya jua. Hata jenereta ya kutegemea wakati umeme unapopotea haijafanya kazi kwa muda wa miezi mbili iliyopita, Chelugo alisema.

“Wagonjwa ambao hatuwezi kufikia katika vijiji hupendelea matibabu kama matumizi ya dawa za mitishamba na utakaso wa kiroho wa jadi,” alisema. “Wengi hufa kwa sababu ya ukosefu wa, au kukosa matibabu ya mapema.”

Madaktari wasema kwamba serikali lazima iwekeza nishati mbadala kama jamii ambao wameathirika zaidi na mabadiliko ya hali ya hewa na uhamiaji wataweza kukabiliana na magonjwa.

Kagondu Njagi ni mchangiaji wa kujitegemea kwa Thomson Reuters Foundation, mjini Nairobi na huandika juu ya masuala ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.