Struggling herders sell off ancestral land to raise money for basic needs, pay off debts or invest in real estate
NAIROBI (Thomson Reuters Foundation) – Katika soko ya Kiserian iliyo kusini magharibi na kingoni mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, Lemarpe Sonkoyo amekuwa akiomba kwa zaidi ya mwaka moja.
Wapita njia humuonea huruma na kumchangia sarafu chache katika bakuli lake huku wakisikiza hadithi yake. Alikuwa na mfugo kubwa wa ng’ombe ambazo alikuwa akichungia shambani mwake ya ekari mia sita.
“Ukame wa mwaka wa elfu mbili na nane ulinimalizia ng’ombe zangu zote na kunibidi niuze shamba langu ili kulisha familia yangu,” alisema baba huyu wa watoto sita, ambaye sasa hana hela, kwa vile alitumia baadhi ya fedha zake kwa pombe.
Kulingana na kikundi cha vijana kisicho cha serikali, YESS, wafugaji wengi kama Sonkoyo wanaendelea kuwa na maisha duni kwa sababu ya shinikizo za mabadiliko ya hali ya hewa.
Kulingana na ripoti iliyotolewa na YESS mwezi wa Novemba, inayoangazia uuzaji wa ardhi na kabila la Wamasai katika kata ya Kajiado iliyopakana na Nairobi, watafiti walionya kuwa jamii ya wafugaji inang’ang’ana kuishi kwa sababu ukame unamaliza vyanzo vya maji na lishe la mifugo, na kufanya kuwa vigumu kuweka mifugo.
Ripoti hiyo iliyofadhiliwa na wafadhili ikiwa ni pamoja na Uingereza na Swedeni yasema wafugaji wanazidi kuuza ardhi ya mababu wao ili kupata fedha za kujikimu kwa mahitaji kama vile afya na elimu, kulipa madeni au kuwekeza mahali pengine. Baadhi yao wanatumia mapato haya kununua bidhaa kama magari na simu.
Zaidi ya nusu ya ardhi imenunuliwa na watu wasio Wamasai na makampuni ikiwa ni pamoja na wawekezaji, licha ya marufuku inayokataza uuzaji wa ardhi, ripoti ya YESS yasema.
Mara nyingi mauzo haya hufanywa na mawakala ambao huwadanganya wateja thamani kamili ya ardhi, kulingana na Nchani Melita, kiongozi wa jamii huko Kajiado.
Kutoka ekari laki mia tao thelathini na nne elfu na mia moja ishirini na tatu za ardhi ya wafugaji huko kata ya Kajiado, elfu hamsini na tisa na mia sita na tano, ama asilimia kumi na moja, imeuzwa katika miaka mitano iliyopita, huku uwekezaji wa manyumba ukizidi kuongezeka.
Wafugaji waliouza ardhi yao wanabaki bila mahali ya kulisha mifugo, na karibu asilimia kumi na tisa huhamia mijini, huku asilimia nyingine tano ikitafuta ajira ya kawaida, ripoti ya YESS yasema.
“Wengi wao hubaki maskini zaidi kwa sababu wawekezaji ambao wanauziwa ardhi hii mara nyingi hununua kwa bei duni,” alieleza ofisa wa YESS, Beneah Mutsotso.
MAJI HUSAIDIA WAFUGAJI KUKAA
Licha ya hali ya maisha kuzidi kuwa ngumu, baadhi ya wafugaji wanagundua njia bunifu za kuhifadhi maisha yao, kwa kulinda rasilimali, kama vile kuhifadhi mimea, misitu na vyanzo vya maji.
Parksian Lenayiesta alikuwa akitumia angalau masaa matano kupeleka mifugo yake kwa chanzo cha maji kilicho karibu, lakini siku hizi yeye hutembea kwa bawa la mchanga lililo kijijini mwake Silango huko kaskazini mwa Kenya.
Lenayiesta anafurahia kwamba yeye hasafiri mbali kutafutia mifugo yake maji na lishe, na anaweza kukaa na familia yake kwa muda zaidi, huku mifugo yake ikiepuka hatari ya wanyama pori ambao hunywa kwa vituo vya maji kichakani.
“Mimi sasa naweza kukaa na familia yangu kwa muda zaidi na kushiriki kwa shughuli za kijiji bila hofu kwamba mifugo yangu haitapata lishe,” alisema baba huyu mwenye umri wa miaka hamsini na nne, huku akitabasamu.
Bawa hili la miaka miwili linatumikia wanakijiji mia nane na hukusanya maji ya mvua wakati wa msimu wa kiangazi, na kuiweka kama akiba kwa miezi. Limetengenezwa na kizuizi halisi ambacho kimejengwa juu ya mto kavu, hivi kinaweza kushikilia maji wakati wa mvua. Mchanga ulio chini ya mto huzuia maji kutiririka chini.
Bawa hili pia limewezesha jamii kuanza mradi wa kupanda nyasi ambayo inavumilia hali sugu ya hewa, kando yake.
Lenayiesta alijitolea kusaidia ujenzi wa bwawa hili, na anasema sasa anaelewa umuhimu wa kulinda rasilimali za asili kama maji.
Joshua Parmeresi, kiongozi wa kiraia katika kata la Kajiado, asema kwamba ujenzi wa mabawa ya mchanga na kuta unaweza kupunguza uhamiaji vijijini wa wafugaji, huku wakiweza kukaa manyumbani mwao.
Katika kikundi chake cha kijiji cha Mello, jamii ya Wamasai imetenga vipande vya ardhi kwa ajili ya ufugaji, huku sehemu zilizo na maji zikitengewa kilimo cha umwagiliaji.
Baadhi ya watalaam wasema jamii zinazopitia shida kama vile wafugaji zinafaa kuacha mila zao ili kukabiliana na shinikizo za hali ya hewa, lakini si wote wanaamini hivi.
“Si lazima wafugaji kubadili mila zao ili kujikimu kimaisha,” alisema Patiricia Kameri Mbote, mtafiti mkuu katika Chuo Kikuu Cha Nairobi.
“La muhimu kwanza ni kuhakikisha wanajua jinsi ya kutumia haki zao za ardhi,” aliongeza.
Hii itawawezesha kuelewa thamani ya ardhi yao bila ya kutumiwa vibaya na mawakala, alisema.
(Taarifa na Kagondu Njagi, uhariri na Megan Rowling)
Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.
