Misaada za kifedha zaimarisha biashara Kaskazini mwa Kenya

by Isaiah Esipisu | @Andebes | Thomson Reuters Foundation
Monday, 11 May 2015 06:45 GMT

Programme to provide cash to help people buy food more efficiently has unexpected consequences

TURKANA, Kenya, May 11 (Thomson Reuters Foundation) – Wakati serikali ya Kenya ilipoanza kupeana misaada za kifedha badala ya chakula kwa watu maskini katika sehemu kame za kaskazini, lengo lilikiwa kuwasaidia ili waweze kujinunulia chakula kwa urahisi.

Lakini mradi huo wa misaada ya kifedha imesababisha matokeo, ambayo hayakutarajiwa. Wapokeaji wengi wa hela hizo wamezitumia kuanzisha bishara ndogondogo, ambazo wanazitumia kama mojawapo wa njia za kustahimili hali mbaya ya anga, inayoendelea kuharibika.

Evelyn Nadio, meneja wa mradi huo kwa kimombo ‘Hunger Safety Net Programme’, asema kuwa walitarajia wapokeaji hao kununua chakula kutokana na dharura iliyopo. Lakini, kwa kuekeza katika biashara, asema meneja huyo, inaonyesha jinsi jamii maskini zinaweza kutumia rasilimali kidogo ili kustahimili ukame.

Misaada hiyo inapeanwa kwa wenyeji wa sehemu kame nchini Kenya ambazo ni pamoja na majimbo ya Mandera, Turkana, Marsabit na Wajir. Wenyeji hao wamepoteza mifugo zao kwa ukame, ambazo huwasaidia kujimudu kimaisha.

Kwa sasa, miaka minane tangu mradi wa ugavi wa hela uanzieshwe, biashara nyingi zimeanzishwa katika sehemu hizo.

Katika soko la Katiko katikati mwa Turkana, Akuom Idieya Katurong'ot, mjane na mama wa watoto saba ameanzisha duka la bidhaa, na kichinjio cha mbuzi. Mama huyo pia amejenga vioski kwa kutumia mabati, ambavyo anakodisha kwa wenyeji. Pesa hizo za misaada ndizo zilimsaidia kuanzisha biashara hizo.

Takribani asili mia 90 ya wapokeaji wa hela hizo za misaada aidha wameanzisha biashara, ama wametumia pesa hizo kununua mifugo ambazo zinastahimili ukame, kama vile mbuzi wa kienyeji.

Lengo la usambazaji wa pesa, asema Nadio, lilikua kupunguza makali ya njaa iliyokithiri na mazingira magumu kwa kupeana shilingi 4,900 kila baada ya miezi miwili kwa kila nyumba iliyolengwa.

Mradi huo ambao unagharimiwa na shirika la U.K. Department for International Development na Australia Aid una lengo la kuzuia familia zilizoathirika kuzama katika umaskini zaidi, ndio wasiuze mali ya katika nyakati za ukame, asema James Oduor, mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ukame Kitaifa (National Drought Management Authority)

Jina la Katurong'ot liliorodheshwa katika orodha ya familia 39,918 zilizobainishwa kama maskini zaidi katika jimbo la Turkana baada ya kupoteza mbuzi 80 kati ya 100 aliyokuwa nao kutokana na hali ya ukame.

Hata hivyo, misaada hiyo ya kifedha imewafikia wengine wengi ambao hawakuorodheshwa. Katika soko la Katiko, Namadak Kalimapus ako na duka la chakula, na bidhaa ambapo anauza vitu tofauti tofauti kama vile mboga, mafuta ya petroli kwa waendeshaji pikipiki, nguo, na hata vinywaji kama vile bia na hata pombe kali.

Mama huyo asema kuwa anauza bidhaa hizo kwa sababu hakuna vituo vya mafuta pembeni, hakuna bar, na hivyo basi, duka lake ni mahali pa kupata mafuta, pombe, chakula na nguo.

Kalimapus alianzisha biashara yake kwa shilingi elfu moja, aliyokopa kutoka kwa marehemu nyanya yake ambaye alikuwa mpokeaji wa pesa hiyo ya msaada mnamo mwaka wa 2013. Hivyo basi, aliekeza pesa hizo katika kununua unga wa ngano na mafuta ya kupika, na akaanza kupika mandazi na mahamri ya kuuza.

Wakati huo, asema mama huyo mwanye watoto sita, yeye ndiye alikuwa anauza bidhaa hizo peke yake katika soko hilo. Hivyo basi wapokeaji wa pesa za misaada walikuwa wakinunua bidhaa hizo kwa ukamilifu, na kumpa faida iliyomuwezesha kusafiri hadi Lodwar ili kununua unga ili kujiendeleza zaidi.

Inakaribia miaka mitatu, biashara za Kalimapus sasa zina dhamana ya maelfu ya shilingi. Hizo nipesa nyingi mno, asema mama huyo, kulingana na hali ilivyo katika sehemu ambayo haina mitandao ya simu, redio, runinga, umeme na hata barabara.

Katika majimbo hayo manne ambayo yamekumbwa na matatizo ya ukame, serikali hutoa pesa kwa jamii 100,000 zilizoathirika zaidi kila baada ya miezi miwili, na nyongeza ya shilingi 2,450 kwa zile jamii zinazohitaji usaidizi wa dharura.

Wapeanaji na wapokeaji wa hela hizo wamebaini kuwa kupeana pesa ni bora zaidi kwa kustahimili hali kame kwa muda mrefu zaidi ikilinganishwa na misaada yachakula.

Nadio asema kuwa ni rahisi kubeba pesa ikilinganishwa na chakula, inaweza kutumika kwa njia nyingi, hivyo basi, wenyeji wanaifurahia kuliko misaada ya chakula.

Hata hivyo, familia zingine zimepata ugumu wa kupokea pesa hizo, ambazo hulipwa kupitia kwenye benki kwa sababu ya kukosa vitambulisho, ambalo ni hitaji kuu katika benki zote nchini Kenya.

Wengine wana matatizo ya majina, ambapo wakati wa uandikishaji hawakuandika majina jinsi ilivyo katika vitambulisho, asema James Lopuya, ajenti wa benki ya Equity ambaye anawahudumia wapokeaji katika Turkana ya Kati.

Lakini, anasema kuwa matatizo kama hayo yanaendelea kushuluhishwa, na mengine yashashugulikiwa na wenyeji kulipwa.

Kulingana na Oduor wa Mamlaka ya Usimamizi wa Ukame Kitaifa, serikali inatarajiwa kuongeza mgao wa fedha hizo katika miaka zijazo.

Wapokeaji wasema kuwa mradi huo umefaulu.

Mary Aking'ol Lokiridi kutoka kijiji cha Eliye, ambaye ako na duka analotumia kununulia watoto wake tisa sare za shule ya msingi ya Kalokol asema kuwa kama angepewa chakula hangekuwa na chochote. Bali, angekuwa akingojea msaada zaidi.

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.