Shule tembezi zatia juhudi kuelimisha wasichana vijijini mwa Kenya

by Kagondu Njagi | @DavidNjagi | Thomson Reuters Foundation
Wednesday, 15 July 2015 13:28 GMT

Girls bond during a school break in Northern Kenya. TRF/Kagondu Njagi

Image Caption and Rights Information

Tent schools with classes that follow rainfall patterns enable girls in pastoralist communities to study

LAISAMIS, Kenya, Julai kumi na tano (Thomson Reuters Foundation) – Akiwa mwenye umri wa miaka kumi na sita, Nagirasia Lengima, tayari ni mama wa watoto wawili. Lakini uzazi haujamuachisha kujikimu kimaisha kwa njia aliyogundua hivi karibuni: shule.

Kama wasichana wegine kutoka jamii ya wafugaji kaskazini mwa Kenya, Lengima anakataa ubaguzi wa kitamaduni na shinikizo za hali ya hewa, kupata elimu kupitia shule tembezi.

Kupitia vikundi visivyo vya faida, shule hizi hupeleka mafunzo kwa wasichana ambao wanalazimika kuzunguka na familia zao ili kujipatia lishe.

Huko kijijini Laisamis, kata ya Marsabit, shuleni inayoendeshwa na kikundi kama hiki kilicho na makao mjini Nairobi, ni zamu ya Lengima kuonyesha ni nini alilosoma kutoka kikao cha asubuhi.

Baada ya kucheza na baadhi ya namba ubaoni, yeye ashangiliwa na wanafunzi wenzake hamsini na tisa, kwa vile anatoa jibu kwa ustadi.

“Hesabu na Kiswahili ndio napenda zaidi,” asema Lengima. “Nataka kufanya biashara katika siku zijazo.”

Lakini hali sugu yafanya njama dhidi yake. Kiasi kikubwa cha waalimu kimeepuka eneo hili kwa sababu ya kutishwa na kikundi cha Al Shabaab.

Hali ya hewa isiyo ya uhakika, nayo inasukuma familia za wafugaji kutoka kwa makaazi yao, ili kutafuta maji na lishe ya mifugo, hivi, watoto hawapati elimu rasmi.

Joto katika Kaskazini mwa Kenya inaweza kufikia zaidi ya nyuzi thelathini, huku kanda hii ikikabiliwa mara kwa mara na ukame na mafuriko.

Adeso humulika hali hii ya hewa kutoa elimu kwa wasichana, ambapo haingewezekana kwa hali ya kawaida.

“Kalenda ya shule hutegemea mwelekeo wa mvua,” alisema Saadia Maalim Mohamed, afisa wa mradi wa Adeso, ambao unafundisha wasichana mia tatu walio na umri kati ya kumi na tatu na kumi na nane, katika kijiji cha Laisamis.

Adeso pia inaendesha shule zingine kama hizi nchini Kenya.

“Mafunzo hufanyika wakati wa msimu wa mvua wakati watoto hawahitajiki sana kazini na harakati za jamii ni nadra.”

KUKATAA HALI SUGU

Kulingana na maafisa, kata ya Marsabit ndio iko na hali duni zaidi ya elimu Kenya, ambapo asilimia ishirini tu wakijua kusoma na kuandika, huku asilimia tisini na mbili ikiwa maskini.

Chini ya asilimia kumi na tano ya wasichana wenye umri wa zaidi ya miaka sita wamewahi kuhudhuria shule, na wale wamewahi, wengi wao huacha. Huku wakikosa njia ya kujikimu kimaisha, wengi wao huolewa na kuanzisha familia.

“Katika jamii ambazo zinakaa maisha ya kawaida, wavulana ndio hupelekwa shuleni,” asema Jonathan Kulmisha, mwanaharakati wa kijamii huko Marsabit. “Wasichana hupewa wajibu wa kazi za nyumbani na kulinda mifugo.”

Lakini baadhi, kama Lengima, huamua kuanzisha upya masomo yao, huku shule tembezi zikiwapa nafasi ya kuendelea.

Kila siku Lengima huamuka saa kumi na moja asubuhi, anahudhuria majukumu yake ya nyumbani, na baadaye anaelekea darasani iliyotengenezwa na hema - na kujazwa na ubao wa chokaa, madawati na viti - ambazo hushughulikia matumishi ya wanafunzi.

Yeye ajua kwamba baada ya wiki chache, mvua itaacha kunyesha na msimu wa ukame utafanya ardhi kukauka.

“Mimi hujaribu kujifunza kadri iwezekanavyo kwa sababu baada ya mvua sisi tutahamia maeneo ya mbali kutafuta malisho,” alisema. Shule zitaungana nao mpaka umbali uwezekanao.

“Walimu wetu hawataweza kukaa baadhi ya maeneo haya ya mbali,” alisema Lengima.

Shule hii ilizinduliwa mwezi wa Februari mwaka wa elfu mbili na kumi na nne, na itaisha mwaka wa elfu mbili na kumi na sita wakati fedha zitaisha.

Kundi hili linatafuta fedha kwa matumaini ya kupanua mradi, lakini inakabiliwa na changamoto kama vile ukosefu wa usalama wa kisiasa, mitandao duni ya barabara na simu, na utamaduni unaokataza elimu ya wasichana, alisema Mohamed wa Adeso.

Kwa sasa, Mohamed ana matumaini kuwa shule hizi zitasaidia jamii, kwa kupitisha waliojifunza kwa jamaa zao.

Lengima anaporudi kijijini mwake baada ya shule, yeye hupenda kutafakari juu ya masomo ya siku, huku akishirikiana na wanawake wengine wanapohudhuria shughuli zao za jioni. 

Lengima hupenda kuongea juu ya mazingira na mabadiliko ya hali ya hewa. Haya ni masuala mapya hapa kijijini, lakini Lengima huyaeleza vizuri na jinsi yana uhusiano na maisha yao.

“Huko shuleni, wanafunzi hujifunza jinsi ya kukabiliana na hali ya hewa ambayo haitabiriki kutokana na ongezeko la joto duniani,” alisema mwanaharakati, Kulmisha.

“Watu kijijini walikuwa wakidhani ukame na mvua kubwa ilikuwa ni kazi ya uchawi. Baada ya mazungumzo na wanafunzi, sasa wanajua vizuri zaidi.”

(Taarifa na Kagondu Njagi, uhariri na Jumana Farouky na Megan Rowling)

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.