Mazungumzo ya moja kwa moja yapoza migogoro ya maji vijijini nchini Tanzania

by Kizito Makoye | @kizmakoye | Thomson Reuters Foundation
Thursday, 3 March 2016 10:25 GMT

Tanzania's minister for agriculture inspects the carcasses of goats killed during a confrontation between farmers and pastoralists in Mvomero district, February 2016. TRF/Zuberi Mussa

Image Caption and Rights Information

Bringing farmers and herders together to work out how to share scare water resources heads off violence

Na Kizito Makoye

PAWAGA, Tanzania (Thomson Reuters Foundation)—Daudi Nangole amekaa chini ya mti mkubwa wa mbuyu, akiangalia kundi na ng’ombe wake wakinywa maji kwenye bwawa lililopo jirani huko Ikolongo –sehemu ambaya mpaka hivi karibuni haikuwa rahisi kwa wafugaji kwenda.

Mfugaji huyo mwenye umri wa miaka 56, familia yake  na ng’ombe wake 73, kondoo na mbuzi walisafiri umbali mrefu  kulifikia bwawa hilo

‘Nilikuwa nikiogopa sana kuja hapa kwa sababu wakulima wenye hasira  walikuwa wanaua ng’ombe  wetu’ Nangole alisema, huku majani makavu yakimpeperukia . ‘ Kwa sasa ng’ombe wana uhuru wa kuranda randa’

Ikolongo ni miongoni mwa vijiji vingi  mjini Iringa  nyanda za juu kusini mwa Tanzania, ambapo wakulima na wafugaji wamekuwa wakipigana mara kwa mara kutafuta maji. Ukame wa mara kwa mara  umewalazimu wafugaji, ambao kwa hawaida hukaa maeneo ya milimani, kuja mabondeni  ambapo kilimo kinafanyika. 

Mapigano hayo ambayo wakati mwingine hugeuka kuwa mauaji ya watu kutoka makundi makubwa mawili. Mwezi Februari mwaka huu, mtu mmoja aliuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa , wakiwemo askari polisi, wakati wa mapigano katika kijiji cha Dihida  wilaya ya morogoro vijijini.

Katika divisheni ya Pawaga, hata hivyo wakulima na wafugaji wametupilia mbali tofauti zao za muda mrefu kwa njia rahisi sana—kuzungumza.

Wamekutana pamoja na kuanzisha umoja  kutatua matatizo yao kwa njia ya majadiliano. Umoja huo ukiwa umeanzishwa na shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Natural Resources Foundation(TNRF), umoja huo unajaribu kuleta maelewano miongoni mwa wanachama wake  kuhusu mahitaji yao, na kuwashawishi kutafuta suluhisho mbadala kutatua mvutano uliopo.

Unaonekana kufanya kazi nzuri ‘ Hatuna tena mgogoro na wakuliam,’ Nangole alisema. ‘ tumekubalia a kugawana kile kilichopo kwa usawa’

Tayari makundi hayo mawili yamekwisha kubaliana  kuhusu maeneo ambayo wafugaji wanaweza kupeleka mifugo yao kunywa maji bila ya kuingilia mahitaji ya maji kwa wengine.

Pia wamekwisha kubaliana  kuruhusu wafugaji kupeleka ng’ombe wale mabaki ya zao la mpunga , ambayo huwa yanatupwa  baada ya mavuno, kwa kulipa ada ndogo kwenye serikali ya kijiji. Wafugaji wanapata chakula cha wanyama wao na wakulima wanapata njia salama ya kuteketeza mabaki ya mpunga.

‘Tuliona kwamba makubaliano haya yatasaidia sana kutatua mvutano usio wa lazima  wakati wa kiangazi,’ Alisema Khalfani Lulimi, diwani wa kata ya Itunundu, ambapo ada ya mabaki ya mpunga inatumika kujengea madarasa ya shule ya msingi.

Tanzania ina  jumla ya kilomita za mraba 611,200 za malisho, na asilimia 72 yake inatumika. Inayobaki ipo kwenye benki ya ardhi inayomilikiwa na serikali.

RUSHWA

Wakulima mara nyingi  wanawatuhumu wafugaji, ambao kwa ujumla ni matajiri, kwa kuhonga viongozi wa vijiji ambao huwaruhusu kuleta mifugo yao kwenye maeneo ya wakulima na kusababisha mtafaruku.

Utafiti uliofanywa na TNRF mwaka 2014 ulionyesha kwamba  sababu za nje  zilizosababisha mvutano huo, ni pamoja na  unyang’anyi wa maeneo kwa shughuli za uhifadhi, ongezeko la miradi mikubwa ya kilimo, rushwa na ukosefu wa miundombinu kuendeleza ufugaji kama namba ya maisha.

‘Hao wanao uana  si chanza cha tatizo—na jambo hili linajulikana fika kwao’alisema Godfrey Massay, mratibu wa miradi ya rasilimali ardhi wa TNRF. ‘Kila nionapo wakulima na wafugaji wanapigana, sioni sababu ya kufanya hivyo’

Divisheni ya Pawaga, yenye mabonde makubwa, kwa kitambo sasa imekuwa ni kitivo cha ugomvi kati ya wakulima na wafugaji na wahifadhi wa maliasili, wote wakigombania mambo wanayoyataka.

Hata hivi toka kumeundwa umoja huo mwezi Juni mwaka 2015, wakulima na wafugaji wamepata fursa ya kukutana kwenye mazungumzo na kutoa dukuduku lao la moyoni ‘ bila ya woga au upendeleo’, alisema Massay. Kundi hilo linakutana mara mbili kwa mwezi, na kila panapo kuwa na mgogoro.

Kwa mujibu wa TNRF, kando na makubaliano ya kuleta usuluhishi umoja huo tayari umekwisha ibua rushwa iliyokuwa ikichochea mapigano

Wanavijiji wamewatambua viongozi wa jamii ambao walikuwa wanapokea rushwa  kutoka kwa wafugaji wakati huo huo wakijifanya wanashirikiana na polisi na wakulima kukamata wale wanao ingilia maeneo ya kilimo.

'Wakulima na wafugaji wanahitaji kujua kwamba kuna watu wanaonufaika  kutokana na migogoro hiyo na wasingependa kuona inatatuliwa,’ Massay alisema.

MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI

TNRF ilipoanzisha umoja wa wakulima na wafugaji Pawaga, kitu muhimu cha mafanikio yake ilikuwa ni kwamba makundi yote yalikuwa na viongozi shupavu walioelewa wigo mpana.

Baada ya miezi ya  majadiliano, viongozi walichaguliwa na sheria zilitungwa. Umoja huo pia ulitambulishwa kwa viongozi wa wilaya na kujenga uhusiano wa kikazi  pamoja na viongozi wa vijiji.

Tayari Kikundi hicho kimekwisha andaa sheria ndogo zinazofuatwa na vijiji vyote 12 na vitongoji 60 vilivyoto eneo hilo, kama mwongozo wa kutekeleza maamuzi ya namna bora ya kutumia ardhi.

Matokeo yake ni kwamba, idadi ya mapigano imepungua sana, kwa mujibu wa Afisa ardhi wa Iringa Donald Mshauri.

‘Hii inaonyesha kwamba  haijalishi mgogoro umeshika mizizi kiasi gani, inaweza kutatuliwa.'

Imeandikwa na Kizito Makoye; Mhariri Jumana Farouky na Megan Rowling. Tafadhali itambue Thomson Reuters Foundation, tawi la hisani la Thomson Reuters inayo chapisha habari za majanga ya kibinadamu, haki za wanawake, biashara ya binadamu, rushwa na mabadiliko ya tabia nchi. Tembelea http://news.trust.org

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.