×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Mizinga ya kisasa ya nyuki nchini Ethiopia yatoa taswira nzuri kwa maisha ya usoni ya vijana wa Ethiopia

by Pius Sawa | Thomson Reuters Foundation
Tuesday, 22 March 2016 11:43 GMT

Abush Asafar, 22, who was trained in beekeeping under an ICIPE project, holds a frame from a beehive, in Tolay, Ethiopia, Feb. 26, 2016. PHOTO/The MasterCard Foundation/Brendan Bannon

Image Caption and Rights Information

Project to create business opportunities for 12,500 young people will also protect forests and reach out to women

NAIROBI, March 22 (Thomson Reuters Foundation) - Ayenalem Ketema ni mfugaji wa nyuki nchini Ethiopia ambaye anajivunia mizinga yake mitatu ambayo imemletea faida hadi kujenga nyumba nzuri yenye umeme wa jua na pia kununua mifugo.

Ketema, anayeishi mkoa wa  Jimma Kusini Magharibi mwa  Ethiopia, hakuweza kuendelea na masomo yake baada ya kumaliza sekondari akiwa na umri wa miaka 17, na amekua akifuga nyuki kwa miaka mine sasa.

"Nimefaidika sana kutokana na hii mizinga ya kisasa," alisema mkulima huyo mchanga, ambaye sasa ana umri wa miaka 22. Yeye ni mwanachama wa kundi la Boter Boro Cooperative, ambalo wanachama wake wanamiliki mizinga 50 ya nyuki.

Faida anayopata kutokana na kilo 60 za asali anayovuna kutoka kwa mizinga yake minne kila msimu,  Ketema amenunua ngombe wa maziwa, kondoo watatu, mbuzi sita, na ameweza kuweka umeme wa miali ya jua kwenye nyumba yake, na sasa ana ndoto kubwa.

"Napanga kufungua duka la jumla la kuuza asali ya kiwango cha juu kwa wingi kwenye soko kubwa," alisema.

Ketema alinufaika kutokana na mradi unaoongozwa na kituo cha kimataifa cha maumbile ya wadudu (ICIPE), ambalo lilizindua mradi mpya mwezi Machi ili kutoa ajira kwa takriban vijana 12,500 nchini Ethiopia katika ufugaji wa nyuki na ufugaji wa nondo wa hariri  au silkworm.

 Kituo cha ICIPE chenye makao yake makuu jijini Nairobi na Wakfu wa MasterCard Foundation wenye makao yake makuu nchini Canada, wanapanga kuwekeza $10.35 milioni katika mradi wa miaka mitano ambao utawasaidia vijana walio nje ya shule na wale wanaokosa ajira kati ya umri wa miaka 18 na 24, kwa kuwapa mafunzo na pesa za kuanzishia ukulima huo.

Jitihada hii inayojulikana kama  Young Entrepreneurs in Silk and Honey initiative itawahuzisha pia watu  25,000 zaidi katika kukuza, kuongeza thamani na kuuza bidhaa hizo mbili.

Wataalam wanasema kwamba, Ethiopia inaongoza barani Africa katika kuzalisha asali na nta lakini uzalishaji huo ni wa kitamaduni na ni asili mia 10 peke ya uwezo wa nchi hiyo wa kuzalisha asali.

Taifa hili kwenye pembe ya Africa, hutoa asali tofauti ambayo huenda kikawa kivutio kwa soko la kimataifa, alisema Mkurugenzi mkuu wa ICIPE Segenet Kelemu, raia wa Ethiopia ambaye alishinda tuzo ya L'Oréal-UNESCO "Ya wanawake katika sayansi.

"Mradi huu utasaidia kuhakikisha kwamba kuna usalama wa chakula, utainua upanzi wa miti badala ya ukataji, na kuhimiza mipango ya ukuzaji misitu kuenea," alisema Kelemu.

Nyuki huzalisha aina nyingi ya mimea na mazao, hivyo kuchangia kiwango muhimu katika utoaji wa lishe na chakula. Nyuki pia huzalisha chakula cha mifugo na kuchangia kwa njia nyingine utoaji wa maziwa na nyama.

"Bila nyuki na wadudu kama hao, maisha yetu yangeathirika vibaya. Kazi hii itakua ikitoa faida kubwa ambayo italinda nyuki na maslahi yake,” alisema Kelemu.

Huku kiwango cha uzalishaji wa chakula duniani kila mwaka kikitegemea wadudu wanaozalisha kikiwa kati ya dola bilioni 235 na 577, ni lazima nyuki wahusishwe katika mipango ya kulisha idadi ya watu ulimwenguni inayozidi kuongezeka, alisema.

Nyuki wanahitaji mimea yenye kutoa maua ili iweze kusambaza mbegu za hali ya juu za kuzalisha mwaka mzima. Hii inamaanisha kwamba wakulima vijana wa nyuki nchini Ethiopia watapaswa kuhifadhi miti, na kupanda miti zaidi, huku wakipunguza kiwango cha kemikali za kuangamiza wadudu ambazo zinadhuru nyuki, alisema Kelema.

Alemayehu Konde Koira, ambaye ni meneja mkuu wa mipango ya maslahi ya vijana katika makao makuu ya Wakfu wa MasterCard jijini Toronto, alisema mizinga ya kisasa itakayotumika katika mradi huu inaweza kuzalisha kilo 20 za asali asiia ya kiwango cha juu ikilinganishwa na mizinga ya kitamaduni ambayo ina uwezo wa kutoa kati ya kilo 6 na 8 za asali isiyo ya kiwango cha juu.

Mizinga ya kisasa ni ya kiwango kizuri, na ni mipana kuliko ile ya kitamaduni ambayo huwekwa juu ya miti.

"Kiteknolojia, mizinga mizuri yaweza kubadilisha kiwanda cha asali nchini Ethiopia, “ alisema Koira.

Mradi huo pia unainua ukulima wa nondo wa hariri yaani Silkworm, kwa sababu zao hilo linahitajika sana kote ulimwenguni,aliongezea. Ethiopia inakisia kwamba mahitaji ya hariri, yataongezeka kwa asili mia tano kila mwaka.

ICIPE hutoa mafunzo ya kiteknologia, ufugaji na uzalishaji wa hariri.

Wakfu wa  MasterCard unasema kwamba mradi huu utaboresha ueneaji wa masoko ya kitaifa, kanda na kimataifa kwa wafanyabiashara vijana. Pia watapewa huduma za kifedha ili kukuza biashara zao.

"Ukisafari nchini Ethioipa, maeneo ya mikoani yamejaa wakulima wanaouza asali kando ya barabara au vijini, kwa ajili ya kutengeneza aina ya pombe inayoitwa tej. Kinachohitajika kwa haraka ni upanuzi wa nafasi za masoko ya wakulima wa asali na hariri,” alisema Koira.

Vituo vitafunguliwa ili kutoa mafunzo kwa wakulima hawa wachanga ili wasiwe tu wakizalisha, bali pia kupenya katika masoko mapya.

Mradi huu utazingatia mafunzo kutoka kwa mradi wa awali uliofadhiliwa na shirika la Uswizi la  Biovision Foundation for Ecological Development na mfuko wa usitawi wa kimaaifa wa  International Fund for Agricultural Development inchini Ethiopia, Kenya na kwingineko barani Afrika.

Swala muhimu lililogunduliwa ni uwezo wa technolojia mpya katika kuleta mabadiliko. Awali, ni wanawake wachache ndio walikuwa wakulima wa nyuki kwa sababu mizinga ya kitamaduni huwekwa juu kwenye miti mirefu ambapo si rahisi wanawake kukwea na kuvuna asali. Lakini mizinga ya kisasa inawekwa chini kabisa na ni rahisi kwa wanawake kuifikia.

Asili mia arobaini ya wahusika wa mradi huu mpya watakuwa wanawake. Kelemu wa ICIPE alisema kuwa ufugaji wa nyuki pamoja na nondo wa hariri vinahitaji kiwango kidogo tu cha mtaji na ardhi.

Pia mradi huu utajaribu kuvunja vizuizi vya wanawake kushiriki katika Nyanja hizi mbili za kilimo.

"Ilmuradi wawe na vifaa vinavohitajika, kama vile mizinga ya kisasa, wanawake vijana wanaweza kufaidika kutokana na taaluma hii ambayo kwa miaka mingi imekaliwa na wanaume,” alisema Koira.

(Imeripotiwa na  Pius Sawa; kuhaririwa na  Megan Rowling. Tafadhali taja shirika la Thomson Reuters Foundation, the charitable arm of Thomson Reuters, that covers humanitarian news, women's rights, trafficking, corruption and climate change. Visit http://news.trust.org)

 

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->