Nyumba za kisasa za polystyrene za tia fora nchini Kenya

by Benson Rioba | Thomson Reuters Foundation
Monday, 30 May 2016 13:36 GMT

Work underway on polystyrene housing in Kandisi, Kajiado County, Kenya. TRF/Benson Rioba

Image Caption and Rights Information

Na Benson Rioba   

KAJIADO, Kenya (Thomson Reuters Foundation) - Justus Opiyo  anaishi katika chumba kimoja kilicho miongoni mwa nyumba zaidi ya hamsini zinazojengwa na paneli zilizotengezwa kutoka  plastiki laini almarufu polystyrene  katika kaunti ya Kajiado, Kusini mwa Kenya. Opiyo anasema kuwa  chumba hicho kina manufaa kuliko vyumba vyote ambavyo amewahi kuiishi.

Chumba hicho  huhifadhi joto  hata wakati kiwango hicho kinapobadilika nje kinyume na  nyumba nilizokuwa nikiishi hapo awali, opiyo asema. Aliongeza kuwa nyumba hiyo ilimkukinga kutokana na viwango vya juu vya joto  vilivyoshuhudiwa mapema mwaka  huu.  

Ujenzi wa nyumba kwa  kutumia polystyrene ni teknolojia mpya ya ujenzi ambayo imeanza kutia fora katika sekta ya ujenzi nchini Kenya. Paneli zinazotumiwa katika ujenzi huu zimetengezwa kwa plastiki nyepesi ambazo huzalishwa mafuta yanaposafishwa na huwa na asilimia 98 ya hewa.

Ili kujenga  nyumba hizi za kisasa, polysterene huwekwa katikati ya nyaya mbili zenye matundu kisha kumwagiliwa simiti ili kuusimamisha wima na kuupa ukuta nguvu.

Kwa vile polysterene ina hewa,  nyumba hizi huweza kudhibiti mabadoliko ya  hali ya anga kuliko zile nyumba zilizotengezwa na mawe ama mbao. Hii ni kwa sababu hewa haina uwezo wa kupitisha joto hivyo nyumba hizo huwa joto wakati nje kuna baridi na husalia baridi wakati kuna joto nje.

Romanus Otieno, mhadhiri wa mipango ya miji katika chuo kikuu cha Nairobi anasema kuwa ingawa polystyrene inazalishwa kutoka kwa mafuta manufaa yake ni mengi hasa ikizingatiwa ujenzi huu unatumia maji kidogo sana. Anaongeza kuwa ujenzi huo utakuwa wa manufaa  katika ujenzi wa nyumba katika miji na maeneo kame ambao kuna uhaba wa maji.

Kwa upande wake, Dennis Muli, ambaye ni  msanifu wa  majengo katika kampuni ya Gem Archplans jijini Nairobi anasema  kuwa uepesi wa Polystyrene unafanya ujenzi wa nyumba kutumia miti michache hivyo kuzuia ukataji miti.

NYEPESI LAKINI DHABITI

Otieno ansema kuwa  nyumba wastani zenye vyumba viwili vya kulala ambazo  zimetengezwa na polystyrene  hugharimu gharimu  Dolla za Kimarekani  6,700, ilihali zile zilizotengezwa na mawe hugharimu maradufu ya kiwango hicho. Hali hii, anasema imechangiwa na idadi ndogo ya wajenzi wanaojenga nyumba za polystyrene kwani paneli hizo ni rahisi kubeba na kuwekeza hivyo mishahara inayolipwa wafanyikazi ni  duni.

Aliongeza kuwa  urahisi wa kujenga  nyumba  za polystyrene huenda  ukachangia pakubwa katika kumaliza uhaba wa  nyumba humu nchini.

Kilomita chache kutoka eneo la  Kandisi ambapo Opiyo anaishi  Kuna Orofa  ya Polystyrene yenye  vyumba 20 katika mtaa wa  Ole Kasasi.

Hii ni baadhi ya miradi ya ujenzi wa  kutumia  Polystyrene ulioanzishwa nchini Kenya na makampuni tofauti zikiwemo orofa zilizojengwa katika jiji la Kisumu na kampuni  ya  Koto Corp kutoka Malaysia.

Lakini teknolojia hii mpya ya ujenzi bado ijaenziwa kikamilifu na kunavbaadhi ya wawekezaji, na wapangaji ambao wanatilia shauku udhabiti wa vyumba vya polystyrene.

Taib Ali, mjenzi katika orofa ya Ole Kasasi anasema kuwa wengi humkejeli kwa kuuliza ni lini orofa hiyo ya makaratasi itakapokamilika kwani watu huamini kuwa orofa hiyo ni hafifu kwani Polystyrene huvunjika kwa uraisi.

Mary Nkatha, ambaye anaishi katika chumba cha mawe karibu na orofa ya Ole Kasasi  bado hajasawishiwa kikamilifu kuwa  polystyrene inaweza kudhibiti uzito wa nyumba  kwa muda mrefu  na anahofu kuwa nyumba  huenda  ikaporomoka. Ansema kuwa atasuburi  na kutazama udhabiti wa nyumba hizo kabla ya kufany uamuzi iwapo ataishi katika nyumba hizo.

Lakini Muli ambaye ni msanifu wa majengo anasema kuwa nyumba zailizotengezwa na polystyrene ni dhabiti kama zile zilizotengezwa na mawe bora tu utaratibu wa ujenzi ufwatwe kikamilifu.

Muli aliongeza kuwa ujenzi wa nyumba kutumia Polystyrene zimekuwa na mafanikio katika nchi ya Japan ambapo hutumiwa kujenga nyumba ndogo zenye umbo la kuba.

USALAMA KWANZA

Muli anazitaka serekali na mashirika yasio ya kiserekali kuwakatika mstari wa mbele kupigia debe ujenzi wa nyumba  wa polystyrene kwani ni ya gharama ya chini na inakuza mazingira.

Aliongeza kuwa  kuna haja ya utendakazi wa hali ya juu kwani teknolojia hii bado ni mpya ilikuzuia majanga kama kuporomoka kwa majengo kutokana na ujenzi mbaya  mbali na kutafuta  njia mwafaka ya kusaga uchafu unayotokana na polystyrene na kutumia upya.

Msemaji wa Koto, Hillary Wesonga alisema kuwa kampuni yake imeanzisha kitengo cha kusaga uchafu unaotokana na polystyrene,   ingawa bado tatizo la uchafu halijakuwa kubwa nchini Kenya kwani teknolojia hii ni mpya. Hata hivyo, mambo huenda yakabadilika katika siku za usoni na kiwango cha uchafu kikaongezeka.

Otieno alihimiza bei za paneli za polystyrene kuteremushwa zaidi iwapo teknolojia hii mpya itaimarika na kutia fora nchini Kenya. Otieno alisema kuwa umuhimu wa ujenzi wa nyumba za bei ya chini ni kumaliza  msongamano wa watu katika maeneo ya miji gharama ya juu ya nyumba itahujumu  mradi huo.

Otieno aliongeza kuwa wajenzi wa nyumba wanapaswa kuzingatia miundo ambayo itasaidia kukuza mazingira kama kutengeza hifadhi za maji ya mvua na kunasa miale ya jua mbali na  kuzingatia vipengee muhimu vya usalama na majanga yanayosababishwa na mabadiliko ya anga.

Mwishoni mwa mwezi Aprili mwaka huu, jumba moja liliporomoka jijini Nairobi na kuuauwa watu wapatao 50 baada ya mvua kubwa kunyesha

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.