×

Our award-winning reporting has moved

Context provides news and analysis on three of the world’s most critical issues:

climate change, the impact of technology on society, and inclusive economies.

Televisheni zinazotumia kawi ya jua zaleta msisimuko vijijini Kenya

by Benson Rioba | Thomson Reuters Foundation
Monday, 1 August 2016 10:15 GMT

Key to the success of M-KOPA's solar digital TV kit is an affordable payment plan using mobile phones

Na Benson Rioba

MACHAKOS, Kenya, Aug 1 (Thomson Reuters Foundation) – Runinga mpya ya Violet Mwikali haikuleta burudani tu bali ilichangia pia kuleta amani katika nyumba yake.

"Lalama zimekwisha sasa kwani hapo awali wanangu wawili walikuwa wakienda kwa majirani kila mara ili kutazama runinga," Asema Mwikali.

Mwikali ni mmoja wa wateja wengi katika eneo la Lukenya Mashariki mwa Nairobi ambao wamenunua runinga inayotumia kawi kutoka kwa miale ya jua kutoka kwenye kampuni ya kutengeza bidhaa zinazotumia kawi ya miale inayojulikana kama M-KOPA.

Runinga hii ya kisasa ya kidigitali ambayo ilizinduliwa mwezi Februari mwaka huu, ina paneli ya nishati ya jua na betri nyepesi ambayo hutumiwa katika kuweka moto kwenye simu na pia kuwasha taa za stima.

Margaret Nduge, ambaye pia anamilika runinga hiyo anasema kuwa amekata tamaa ya kuwekewa huduma za stima katika makao yake. Kabla ya kuanza kutumia nishati ya jua Ndunge anasema alikuwa akitumia jenereta kujipatia kawi lakini ilikuwa na makelele mengi pamoja na moshi mwingi na ilikuwa ikimgharimu muno kifedha.

Ndunge anasema kuwa paneli hiyo ya nishati ya jua hufanyakazi hata wakati hakuna jua jambo ambalo anafurahia. Betri ya runinga hiyo hudumu masaa manne inapotumiwa kuwasha taa za stima na kutazama runinga kwa wakati moja.

Takwimu kutoka kituo cha wakfu wa utafiti wa Kenya Audience za mwaka 2015 zinaonyesha kwamba ni theluthi moja tu ya wakenya wazima wanooweza kutazama vipindi vya runinga huku waliosalia wakikosa huduma za umeme na runinga.

MATUMIZI YA NISHATI YA JUA YA TIA FORA

Kifaa hiki chote pamoja na runinga kinagharimu dola 530 za marekani huku wateja wakilipa dola 79 kama malipo ya kwanza , na hadi dola moja kila siku hadi mteja atakapomaliza kulipia kifaa hicho.

Raphael Makau ambaye pia ana kifaa hicho anadai kuwa dola 148 za marekani ambazo hutozwa na serekali ilikupewa huduma za umeme ni ghali muno. Anaongeza kuwa ingemchukua mda mrefu kuchangisha fedha hizo na huenda angekaa bila umeme kama kifaa hiki cha nishati ya juu hakingemsaidia.

Jesse Moore, ambaye ni mkurugenzi katika kampuni ya M-KOPA anaamini kuwa mataifa ambayo hayajastawi yanaongoza katika matumiza ya kawi safi.

Kulingana na Moore hadi sasa kampuni yake imeuza runinga 6000 na wanataka kuongeza uzalishaji wa runinga hizi zinazotumia nishati ya jua ilikukimu ongezeko la wateja.  Aliongeza kuwa wanalenga familia milioni tatu kati ya milioni tano  ambazo hazijapata huduma za umeme.

Aliongeza kuwa wanawalenga wakaazi wa maeneo ya mashambani kwani wengi wao ni maskini na wanahitaji vifaa vya nishati za jua za bei nafuu.

BETRI BORA

Wateja wemeanza kutambua baadhi ya vitu vinavyopaswa kuboreshwa kwenye vifaa vya nishati ya jua vitakavyo tengeza mnamo siku za usoni. Mwikali anapendekeza kutengezwa kwa betri inayodumu zaidi kwani masaa mnane ni chache sana kwa familia yake.

Maoni ya a Mwikali yaliungwa mkono na Makau ambaye anadai kuwa hulazimika kutumia taa za mafuta wakatik batri hiyo huisha wakati wa usiku.

Moore anadai kuwa M-KOPA inanuia kuimarisha ubora wa runinga hiyo ya nishati ya jua kwa kuongeza vifaa zaidi katika runinga hiyo. Hata hivyo, alionya kuwa bei ya runinga hiyo haiwezi kuteremshwa zaidi kwani gharama yake ni ya chini ikilinganishwa na ubora wake.

Kampuni ya M-KOPA sasa imeanza kudadisi lipi itakalofanyia betri hizo pindi tu muda wake wa matumizi wa miaka tano utakapokamilika na wameanza kushirikiana na kampuni zingine ili kupanga jinsi watakavyo saga batri hizo kama njia moja ya kuhifadhi mazingira.

M-KOPA inanuia kuuza runinga hizo katika nchi jirani za Tanzania na Uganda na kuanza kutengeza vifaa vyote vya runinga hiyo  nchini Kenya .

Our Standards: The Thomson Reuters Trust Principles.

-->